chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,383
- 24,939
Na Peter Sarungi (The Next Speaker)
Nimepata taarifa ya kuchaguliwa kwa ndugu kuwa mbunge wa viti maalum kutoka Chadema ili kuziba pengo lililo achwa na hayati Dr. Macha aliyekuwa mbunge wa viti malaamu aliyetokana na kundi la wanawake wenye ulemavu.
Kwa taarifa iliyokamilika ni kwamba mbunge aliye teuliwa hana aina yoyote ya ulemavu na kwa maana hiyo hawakilishi kundi la watu wenye ulemavu kama ilivyokuwa kwa Dr. Macha (R.I.P)
Sheria namba 9 ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 iliyoanza kutumika rasmi july 2010 ingawa imekuwa ikiwekwa kandoutekelezaji wake inatoa maelekezo juu ya ushiriki wa watu wenye ulemavu kama ifuatavyo.
Sura ya kwanza inaelezea misingi mikuu ya utambuzi wa haki za watu wenye ulemavu ikiwepo ya Ushiriki na ujumishwaji kikamilifu wa watu wenye ulemavu katika nyanja zote za jamii, siasa na uchumi.
Sura ya pili nayo ina ainisha haki za watu wenye ulemavu ikiwepo haki ya kushiriki katika siasa bila ubaguzi kama kugombea, kuchagua, kupiga na kupigiwa kura, kuchaguliwa na kuteuliwa.
Pia sura hiyo yapili inasisitiza haki ya kutambuliwa na kujumuishwa katika mipango yote ya maendeleo, sera na sheria.
Ingawa mimi sio mbobezi wa sheria lakini kwa msingi wa sheria hii No.9 iliyo anzishwa kwaajili ya kuhifadhi haki za msingi za jami ya watu wenye ulemavu, tunao Chadema Tanzania na Tume ya uchaguzi inatukosea jamii ya watu wenye ulemavu kwa kuvunja sheria hii.
Dr. Macha alichaguliwa si kwa kushindanana wanawake wasio kuwa walemavu bali alichaguliwa kutoka miongoni mwa wanawake wenye ulemavu walioomba nafasi hiyo na inawezekana alipata kura chache ukilinganisha na washindi wengine lakini ushindi wake aliupata kutokana na kundi la watu wenye ulemavu.
Dr. Macha alikuwa amebeba makundi mawili kwa wakiti mmoja, kundi la wanawake na kundi la walemavu na kazialiyopewa ilikuwa ni kuwasemea wanawake wenye ulemavu na jamii yote ya watu wenye ulemavu kwa ujumla.
Dr. Macha aliweza kuitendea haki nafasi hiyo kwa sababu anaishi katika dunia ya watu wenye ulemavu akizijua changamoto zake na fursa zinazo hitajika.
Kwa utaratibu wa Chadema na Tume ya Uchaguzi unao vunja haki ya watu wenye ulemavu kupata uwakilishi bungeni, sasa amechaguliwa Ndugu ambaye hajui na hajawahi ishi katika dunia ya watu wenye ulemavu.
Na kwa maana hiyo anaingia bungeni akiwa amebeba agenda zilezile zilizo bebwa na wabunge wengine wote wa Chadema wa viti maalum.
Hivyo uwakilishi wa hoja na mawazo ya watu wenye ulemavu kutoka upande wa kambi rasmi ya upinzani bungeni utakuwa umekoma.
Hii si sawa kabisa kwa dunia yasasa yenye kuheshimu makundi nyonge katika jamii na tena kwa chama kinacho jinasibu kutetea jamii na kuwa mbadala wa chama tawala wakikosesha uwakilishi wa kundi hili japo kwa uchache.
Historia inaonesha kuwa hii ni mara ya pili kwa jambo kama hili la kupoteza uwakilishi wa watu wenye ulemavu bungeni kupitia Chadema.
Uchaguzi wa mwaka 2010, Chadema walimchagua Bi. Regina Mtema(R.I.P) kuwa mbunge wa vitimaalum kuwakilisha sauti ya watu wenye ulemavu bungeni.
Hata hivyo haikuchukua miaka miwili tukasikia mwakilishi wetu amefariki dunia kwa ajali ya gari eti alilokuwa akiendesha yeye mwenyewe tena safari ya masafa marefu akielekea Dodoma.
Chadema na Tume ya Uchaguzi kwa kutumia kanuni zinazo kandamiza uwakilishi wa watu wenye ulemavu walimchagua mbunge mwingine ambaye hakuwa na ulemavu wowote hivyo kufanya sauti ya watu wwenye ulemavu katika kambi rasmi ya upinzani kufa kifo cha kimya.
Najiuliza, hivi kweli chadema wanaheshimu haki za watu wenye ulemavu?? Au mnawatumia watu wenye ulemavu kama boshen katika kukidhi vigezo vya viti maalum kisha kuwatoa kafara kwa maslahi yenu?????? Kama mliweza kushawishi upatikanahi wa Dr. Macha kwa nini mshindwe kujenga hoja za kupatikana kwa mwakilishi mwingine wa kundi hili??? Logic ya kumchagua ndugu ni ipi ikiwa logic ya mwanzo ya kumchagua Dr. Macha ilikuwa ni kuwakilisha watu wenye ulemavu???? Au mnawaona walemavu wote ni mburula wanao nyamaza hata kama haki zao zita keukwa????? Kweli kamati kuu ya chadema inabariki upuuzi huu???? Mmenikera na wote mnao tutoa kafara watu wenye ulemavu na mnao tetea wote ni mashetani wa kutupwa na Mungu ana waona mjue.
Kumbe ndio maana albino wanaishi roho juu katika nchi yao.
By the way hizi salamu ziwafikie wote mnao watumia watu wenye ulemavu kamangazi katika kufika mafaniko yenu, salamu ziwafikie wajumbe wote wa kamati kuu ya chadema wanao endeleza mchezo huu wakuwatumia walemavu kisha kuwadamp, salama ziwafikie Tume ya uchaguzi na kanuni zao zinazo kandamiza uwakilishi wa walemavu katika siasa za nchi hii, salamu hizi zifike kwa Waziri anaye husika na watu wenye ulemavu kutoka ofisi ya waziri mkuu wakiwa na mikakati hewa kwawatu wenye ulemavu.
Kwa sasa tumebakiza wabunge wawili wanao wakikisha watu wenye ulemavu bungeni na wote wanatoka Chama cha Mapinduzi ambao ni Mh. Stela Ikupa na Mh. Amina Mollel kati ya wabunge zaidi ya300.
Niwatie moyo wabunge hawa waendelee na kazi takatifu ya kuwakilisha na kutetea kundi nyonge la walemavu ambayo kwa imani yangu nikazi yenye dhwawabu kwa Mungu.
Niwapongeze na nawaombea wazidi kuwa na uhai na afya nzuri kwa kipindi chote cha bunge ili hizi nafasi mbili ziweze kuzaa matunda mema kwa jamii ya watu wenye ulemavu.
Hili ni POVU langu binafsi kama mlengwa kutoka jamii ya watu wenye ulemavu, likikuudhi basi na wewe toa povu lako.
Asanteni.
Fikisheni ujumbe kwa wahusika muwaambie tunalaani maamuzi yao.
C&P