Tume ya Taifa ya Uchaguzi mlishampanga mshindi wa Urais?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,410
Tume ya Taifa ya Uchaguzi mlishampanga mshindi wa Urais?
--------------

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejiaibisha kwa mara nyingine tena. Kumuita mgombea wa Chadema Tundu Lissu kwenye Kamati ya Maadili kumtaka ajieleze kwanini anasema lazima atashinda uchaguzi huu ni wazi Tume hiyo Ina mshindi wake mfukoni ambapo wanapata ukakasi wanaposikia mgombea mwingine akisema atashinda uchaguzi huu.

Inafahamika wazi Tume hiyo ya uchaguzi haiko huru na ilichofanya ni maelekezo tu kutoka Chama Cha Mapinduzi baada ya kutishwa na Kasi kubwa ya na Kasi kubwa ya Mgombea wa Chadema.

Wito wa kumuita Tundu Lissu kwenye Kamati ya Maadili Tarehe 29/9 kumeivua nguo Tume hiyo kwani Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole siku moja kabla alishaielekeza Tume hiyo inapaswa kumfanyia Nini mgombea wa Chadema.

Habari za ndani za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinasema tayari CCM ilishawaelekeza kumzuia mgombea Urais wa Chadema kuendelea na kampeni kwa siku 14 kwa hiyo wanachofanya Sasa ni mazingaombwe tu na Utekelezaji wa maelekezo ya CCM.Hata kabla ya Mkurugenzi wa NEC kujitokeza hadharani jana kumuita Tundu Lissu kwenye Kamati ya Maadili Tarehe 29 habari zilishavuja kwamba walishafikia maamuzi na CCM kuzuia kampeni za Lissu kwa siku hizo 14 kuanzia tarehe 1 October.

NEC imeshindwa kuficha mapenzi yake kwa CCM kwani Mgombea wa CCM na chama chake wamekuwa wakivunja waziwazi maadili ya Uchaguzi lakini hawakuwahi kukemewa.

Mgombea wa Urais wa CCM amekuwa akitoa ahadi za Ujenzi wa Barabara Kama Rais na anapiga simu kuelekeza mawaziri katikati ya mikutano ya kampeni kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi.

Mgombea wa Urais wa CCM amekuwa akisema katika kampeni zake kamwe hatapeleka Maendeleo kwenye Jimbo au Kata itakayochagua mpinzani kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi.

Tume inasema Lissu kosa lake ni kusema atashinda Urais lakini Tume hiyo haijaona Kama mgombea wa CCM kusema watu hatawapelekewa maendeleo wakichagua mpinzani tayari ni kujitangaza mshindi.

Waziri Mkuu wa Tanzania amekuwa akipita kila Kona ya nchi kufanya kampeni za Mgombea Urais wa CCM kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi lakini Tume ya Uchaguzi imeweka Pamba masikioni.

Mgombea Urais wa CCM amekuwa akitumia Televisheni ya Taifa kuanzia asubuhi mpaka jioni kujitangaza live mikutano yake ya Kampeni huku wapinzani wake wakikosa Fursa hiyo kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeweka Pamba madikioni.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole amekuwa akirushwa Live na Televisheni ya Taifa akiongea na Waandishi wa Habari na amekuwa akimtukana mgombea Urais wa Chadema matusi makubwa yasiyoandikika hapa kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeweka Pamba Masikioni.

Mpaka ninapoandika hapa wagombea kadhaa wa Upinzani walioenguliwa kwenye uchaguzi hawajapewa taarifa rasmi wanarudishwa au kuondolewa kwenye kinyang'anyiro baada ya kukata rufaa lakini Tume hiyo Wala haijali zaidi ya kumfungulia mashtaka mgombea Urais wa Chadema kwamba kwanini anasema atashinda Urais.

Yapo mengi Sana ya kuandika hapa hayo niliyoweka ni machache tu lakini itoshe kusema Tume hii na CCM hawakujiandaa na Upinzani mkubwa hivi kutoka Chadema ndiyo maana bila aibu wanamshtaki Lissu eti kwanini anasema atashinda Urais.

Hakuna Vurugu yoyote itakayofanyika nchi hii Kama Haki itatendeka katika Uchaguzi huu.Hawa wanaojihami wamepanga kuiba kura na kufanya uhalifu kwenye uchaguzi huu ndiyo maana wanatapatapa wanapoona mgombea akitaka Haki Itendeke.

Nitaandika zaidi tarehe 2/10 baada ya maamuzi ya NEC ya kumzuia mgombea Urais wa Chadema kuendelea na kampeni kwa wiki mbili......
 
Back
Top Bottom