Ex Spy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2007
- 313
- 2,649
Balozi Radhia Naima Mtengeti Msuya ni mdogo wa tumbo moja (ndugu wa damu) wa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM – Mtendaji Mkuu wa shughuli za chama.
Balozi Radhia Naima Mtengeti Msuya ni sehemu ya wajumbe saba wa kinachoitwa “Tume Huru ya kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani”. Tume iliyoundwa na kutangazwa jana.
Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025
Kwa kuzingatia muundo huo wa tume hiyo, ni wazi tume yenyewe kwa ujumla, imepoteza uhalali achilia mbali weledi katika kuitwa chombo cha uchunguzi – kabla ya kuanza kazi.
Kwanini? CCM ndiyo chama ambacho mdogo wake wa tumbo moja, Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ni Katibu Mkuu (Secretary General). Je, anaweza kuwa kuwa huru kutimiza wajibu wake?
Wananchi wanataka uchunguzi wa mauaji ya kutisha ya raia. Wananchi wanataka kufahamu watu wangapi wameuwawa, wangapi wamezikwa, wangapi maiti zao hazionekani na wangapi wamejeruhiwa.
Kwa kuwa waliounda hiyo tume wametueleza kwamba wameunda tume kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa matukio ya ‘uvunjifu wa amani’, ni wazi tume hiyo haituhusu wananchi.