Mzee Mtei, mimi nakuita baba kwa sababu nimesoma darasa moja na mtoto wako Meli.
Pili nakupongeza kwa kutoa maoni yako kuhusu hii tume, bali lazima nikiri wazi, baba umeanza kuzeeka!.
Hii ni tume, kazi ya tume sio kutupatia katiba bali ni kukusanya maoni, hii inamaanisha kazi ya tume hii ni kutusikiliza sisi Watanzania tunataka nini, halafu ndipo iya compile maoni hayo, sasa wewe wasiwasi wako wa nini?.
Hoja zako zote mbili baba, hazina mashiko.
1. Hili la uwiano, wa wajumbe 15 kutoka bara na 15 kutoka Zanzibar, sio la JK, hili ni takwa la kisheria ambalo ni lazima litimizwe!. Rais hapa hakuwa na choice ametimiza jinsi sheria ilivyosema.
Kijana wako Tundu Lissu hili alilipigia sana kelele mpaka akaonekana ni mpinga maendeleo. Kwa vile wewe ni miongoni mwa visima vya hekima, busara na uzoefu tulivyo navyo, ungetoa hoja binafsi kuwa kutokana na uwingi wa watu na ukumbwa wa eneo, muungano wetu uendeshwe kwa proportional representation na sio equal basis kama ulivyo sasa!. Naamini ungesikilizwa!.
Hizi haki za Zanzibar ndani ya muungano, zimekuwa zikikiukwa kwa miaka mingi mpaka tujajisahau kwa kudhania Tanzania bara ndio yenye haki kubwa ndani ya muungano kutokana na wingi wa watu na ukubwa wa eneo, kitu ambacho sii sawa. Tanzania na Zanzibar ni two partners wenye haki na hadhi sawa ndani ya muungano wetu kama zilivyo ndoa za kiserekali mkishaoana, siku mkiachana, mnagawana mali pasu kwa pasu na mkeo, hata kama ni wewe ndio ulikuwa umechuma hiyo mali na mkeo ni mama tuu wa nyumbani!.
Zingatia simaanishi hii ndio uwiano bora, ila hapa rais Kikwete ametimiza matakwa ya kisheria!.
2. Hili la pili la udini pia halijakaa vizuri, kwa vile idadi ni watu 14 toka kila upande tena kwa rais kupelekewa mapendekezo ya majina, hakuna shaka kuwa asilimia 99% ya Wanzanzibari ni Waislamu, hivyo ili kuweka uwiano wa dini, jee ungetaka hao wajumbe 14 toka Zanzibar ndio wawe Waislamu halafu wale 14 wa bara ndio wawe Wakristu?.Au hata kama hakuletewa hata jina moja la Mkristu kutoka mapendekezo ya Zanziabar, basi rais angejitafutia japo Mkristu mmoja amteua ili ionekane Zanzibar nayo ina Wakristo?!.
Kwa vile katiba tunayoitafuta ni katiba ya nchi na sio katiba ya uendeshaji wa ibada wala kupanga utaratibu wa swala, naomba tuipe imani, hata kama inawajumbe wengi kutoka dini fulani, hadidu za rejea hazionyesha kama aumuzi wa nini kiwepo kwenye katiba mpya na nini kisiwepo, utaamuliwa kwa wajumbe hao kupiga kura, hivyo Wakristo watashindwa!. Hoja hii ya uwiano wa bara na visiwani na Ukiristu na Uislamu, utakuwa na mashika wakati wa uundaji wa bunge maalum la katiba ambalo ndilo litaamua nini kiwepo na nini kisiwepo kwa kupiga kura, na wa mwisho kabisa ni sisi wananchi, kupiga kura ya maoni "referendum" kuikubali au kuikataa!.
Naamini yule mdogo wako mule kwenye tume, atayasimamia maslahi yako ipasavyo hata kama yuko yeye mmoja tuu!.
Namalizia kwa kuomba radhi tena kama kutaonekana ukosefu wowote wa adabu kwa wakuu wetu.
Asante.
Pasco.