Tume ya kuboresha mifumo ya haki jinai ni historia kwa Afrika

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Rev. John E. Kimario

Watu wa Mungu, watanzania wenzangu nawasalimu kwa upendo na kwa jina lipitalo majina yote. Kama tujuavyo HAKI HUINUA TAIFA, leo natuma waraka huu kwenu ukazidi kuifanya haki na upendo utamalaki kila kona ya nchi yetu hii nzuri.

Ndugu zangu, Mimi kama Mhadhiri katika Theolojia na falsafa nimefanya Tafiti nyingi katika nchi kadhaa ndani na nje ya Afrika. Kwa uzoefu wangu bila kupepesa macho napenda kumpongeza Rais Samia kwa ujasiri na nia njema aliyo ionyesha kuunda Tume hii muhimu.

Ndugu zangu, uamuzi wa kuunda Tume kwaajili ya kuimarisha mifumo ya utoaji haki ni UTASHI USIO WA KAWAIDA hasa kwa mataifa ya Afrika. Kila mtanzania anao wajibu wa kumuunga mkono na kumpa support Rais huyu mpenda Haki.

Rafiki zangu mlio kwenye siasa nawasihi msiibebe ajenda hii kisiasa kwani inalenga kuponya majereha na kuleta furaha katika nyuso za watanzania. Itoshe kusema Rais Samia ni kama nyota ya asubuhi inayoleta tumaini na kufungua kurasa mpya ya hatma ya Mama Tanzania.

Kwa hakika, Rais Samia anaishi maneno yake kwa vitendo, alianza kwa kufuta kesi zenye utata na sasa hajataka kukurupuka na kutumia mamlaka yake kufanya mabadiliko bali ameamua kutumia weledi kwa kuunda Tume itakayotoa dira kitaalam kabisa kufanya mabadiliko yenye tija katika utoaji haki nchini.
 
Lisu ameendelea kudai kwamba hayati Magufuli aliagiza msaliti hasitahili kuishi na baada ya muda mfupi Lisu akashambuliwa kwa risasi Dodoma, je kumbe Lisu alikuwa anajijua ni msaliti wa nchi?, maana Magufuli hakutaja jina la mtu alitaja msaliti.
Kwa nini Clouds FM hawakumuuliza dereva wake amemficha wapi?

Kwa nini Clouds hawakumuuliza sababu za Acacia kufutwa Tanzania na hawakushitaki MIGA?

Kwa nini Clouds hawakumuuliza kama alipigwa na Magufuli na sasa hivi ni miaka miwili Magufuli hayupo kwa nini uchunguzi haufanyiki sasa hivi?

Nb: watoto wa Mbowe na Lisu wote ni raia wa Marekani.
 
Nafikiri kama ikifanya kazi yake vizuri,kwa haki , weledi na uzalendo,Inaweza ikawa na mapendekezo ya kujifuta chama tawala na kukipiga kabisa marufuku Tanzania na popote duniani😂
 
Back
Top Bottom