sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,677
- 1,102
Tanzania nchi yetu tunaipenda sana,ndio maana tuliimba wimbo wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wangu wote.ni kweli tunaipenda kwa moyo wote japokuwa hatuna uhuru wa kujiamulia mambo yetu kwa matakwa yetu binafsi bila kupata mashinikizo toka kwa wanasiasa.Nasema hivi kutokana na kauli mbalimbali zinazojaribu kujitokeza toka kwenye vinywa vya watu waliopewa madaraka na kusahau kuwa cheo ni dhamana.
Wanasiasa hawa ndio msingi mkubwa wa kutufikisha katika hali duni tulizo nazo hivi sasa.Wanasiasa hawa ndio mabingwa wa kauli mbiu zisizotekelezeka kivitendo na kuishia zikipigwa vumbi kwenye makabrasha.Leo tunaimba wimbo wa katiba mpya,katiba ambayo haikuwa hoja ya CCM na wala haikupewa nafasi katika ilani ya chama hicho.Hali kama hii ndio inapelekea kuwatahadharisha wajumbe wakati ya maoni ya katiba wawe makini na mashinikizo yanayo tolewa na wanasiasa.
Tunazungumzia katiba yetu na muundo wa serikali tuitakayo,lakini napata mashaka na vikwazo ambavyo vinavyojaribu kupigiwa debe na viongozi kwamba tuvijadili si kwa nia ya kuvivunja bali kuviboresha.Hapa nazungumzia muungano ambao ulioasisiwa kwa matakwa ya watu wawili tu.Toka wakati wa kuanzishwa muungano huu kumekuwepo mipasuko mingi ambayo ikiachiwa inaweza kuitumbukiza nchi katika hatari kubwa.Sisi ndio wenye dhamana na nchi hii,tuachiwe tuamue wenyewe bila kuingiliwa kuamua ni muungano upi tuutakao kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili.Haki yetu kama wanachi isitumike kwa kupiga kura tu, bali itekelezeke hata katika kuamua aina ya serikali tunayoitaka, hapo ndipo ukomavu wa demokrasia utakapoonekana.
Yapo mambo yamesemwa ambayo ni mapendekezo ya CCM kwenye kikao cha NEC,mengine mazuri yanakubalika,lakini isiwe ndiyo hadidu za rejea kwa kuwashawishi wananchi waamue yale yanayotakiwa ambayo ndiyo msimamo wa chama katika kushinikiza kuingizwa katika katiba hii.Napata sana taabu hasa pale yalipozungumzwa asubuhi hii ya leo kama ndiyo tayari maazimio yaliyopitisha katika katiba.Unapozungumza tunataka jambo hili liwe hivi,hiyo si pendekezo bali ni command.Tunawaomba viongozi wa kivyama wazingatie taratibu kama walivyokubaliana na kuachwa suala hili kuwa mjadala wa umma mzima.
Tukiruhusu kila mtu atoe shinikizo lake hiyo haitakuwa katiba tunayoitaka,uhuru wa mawazo ya Watanzania uheshimiwe kama katiba ya hivi sasa inayotaka bila kuvunja sheria.Wananchi wajitokeze kwa wingi kupata nafasi hii adhimu katika historia ya nchi yetu kutoa mchango wa kimawazo juu ya nchi waitakayo.
Jukumu walilopewa Mh, Warioba na jopo la wajumbe wa tume ya katiba ni mzigo mzito unaohitaji hekima,busara na maarifa katika kuelekea kuipata Tanzania tuitakayo.Umakini wao,usomi wao uwe chachu na uongozwe na uzalendo walionao juu ya nchi yetu.Tunaomba waachwe wafanye kazi yao bila kuwaweke mipaka ya mjadala vinginevyo katiba tuitakayo itakosa mashiko.Tanzania yetu itajengwa na wale wote wenye moyo safi.
Mwisho wana JF wenzangu tuwe mstari wa mbele kutoa elimu kwa wananchi wenzetu na kuitumia bodi hii kuhakikisha mchakato huu wa katiba hautekwi kivyama bali iwe ni ridhaa ya Watanzania wote,wa dini zote,rangi zote na kabila zote.