RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania(CHRAGG), imesema kuwa kutorushwa kwa matangazo ya Bunge ya moja kwa moja kunaweza kutafsiriwa kama kuwanyima wananchi haki ya kupata habari kuhusu mwenendo na kazi muhimu inayofanywa na na chombo hicho kikuu cha uwakilishi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga jana usiku Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Umahiri Katika Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT), ambapo alikumbushia uhuru wa kupata na kueneza habari unalindwa na Ibara 18 ya Katiba ya mwaka 1977.
Nyanduga pia aligusia sheria ya magazeti ya mwaka 1976, inayolalamikiwa wadau wa vyombo vya habari ambayo katika Tume ya Jaji Nyalali iliyowasilishwa mwaka 1994, ilizungumzia Sheria Hiyo ya Magazeti ikiwa ni moja wapo ya sheria 40 kandamizi zilizotakiwa kubadilishwa kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Amesema kuwa kwa mujibu wa ripoti ya Jaji Nyalali sheria hiyo imempa mamlaka makubwa Waziri wa anayesimamia habari katika mambo ambayo yanavunja baadhi ya haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari, na kuongeza kuwa kwa mantiki hiyo sheria hiyo inakiuka Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.