Tume Tumeeeeee . . . . . Aaaaaagrrrrr | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume Tumeeeeee . . . . . Aaaaaagrrrrr

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CPU, Feb 18, 2011.

 1. CPU

  CPU JF Gold Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Jamani hiyo tume ni ya nini hasa?
  Hizi tume zinazoundwa baada ya majanga kutokea za kazi gani wakati wahusika wakuu ambao ni wizara ya ulinzi na Mkuu wa Jeshi la wananchi bado hawajaondoka ktk viti vyao??? Kwanini basi wizara yenyewe isichunguze hicho chanzo za mabomu???

  Huu ni mpango wa kujichotea hela tu kwa mgongo wa wahanga wa Goms. Ni ubadhilifu mkubwa wa mali za umma.

  Kwanin hiyo tume isiundwe kuchunguza fidia kwa wahanga??? Hii tume ina faida gani kwa mwananchi aliyepoteza ndugu zake, hana mahali pa kuishi, hajui aende wapi, hajui atakula nini leo na kesho???? Au hiyo tume ndio itajenga makazi mapya ya wahanga???

  Kwanini kasi waliyotumia kusambaza mabango ya kampeni nchi nzima wasitumie kurejesha makazi ya wahanga???

  Haya si ndio matokeo ya majeshi yetu ya ulinzi kuacha kazi zao za kulinda amani na usalama kwa wananchi wake na kujiingiza ktk siasa na kujifanya wanatoa vibali vya maandamano, mara habari za kiintelijensia halafu mwishoe kumpelekea Waziri Mkuu habari feki mpaka anaonekana amelidanganya Bunge???

  Walitakiwa (Wanajeshi) wajue wajibu wao wa kutunza silaha zisilipuke ktk makazi ya watu, badala ya kujiingiza kutoa matamshi ya kutisha wananchi kama tamko la Shimbo kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

  Hizi tume hazina tija kabisaaaaaaaaaaa
   
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ni kawaida kwa mujibu wa sheria kuunda baraza la uchunguzi pale yanapo tokea maafa yawe ya ajali ya gari,moto au hat kama ya Goms.
  Lengo la baraza ni kujua pamoja na mambo mengine,
  1.Nini chanzo cha ajali
  2.je kuna uzembe uliofanyika.
  3.je kuna mtu aliyekufa au kujeruhiwa.
  4.je Nani ALAUMIWE.
  5.Nini kifanyike ili hali kama hiyo isitokee tena.
  Hayo ni kwa uchache wa kazi za tume/baraza.
  Nimuhimu kufanya uchunguzi na matokeo ya uchnguzi huo kufanyiwa kazi.
  Hatakama hautafanyiwa kazi sasa ila wapo watakao ufanyia kazi na kuchukua hatua stahili.
   
Loading...