Naona unaongea upupu tupu, hakuna ambacho Zenji mmejifunza kuhusu matatizo ya uchaguzi.
Mna bahati kwamba mna wajomba zenu bara, mkiiba kura wanakuja kuwasaidieni ili msichinjane kama Kenya.
Kaka mbona unalia? Jibu maswala niliyokuuliza na sio kulia lia hapa.
Kwa taarifa yako Mapendekezo yaliyotolewa na Tume iliyomaliza muda wake ambayo kwa undani ni kutokana na malalamiko n kasoro zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita ni kama yafuatayo....
- Mapendekezo haya ni chini ya Tume ya Rais ya pamoja ya utekelezaji Muafaka wa CCM na CUF.
- Aidha timu ya wataalamu walioshiriki katika kutoa ushauri inaundwa na Bw. Ron Gould kutoka Canada na Profesa Chris Peter kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wataalumu wengine toka ndani na nje ya Tanzania
Nafasi ya naibu mkurugenzi wa uchaguzi na wasaidizi wakurugenzi wa uchaguzi imeondolewa na sasa imependekezwa kuwa na muundo wa divisheni sita.
Divisheni ya kwanza ni ofisi ndogo ya uchaguzi Pemba itakayosimamia shughuli za kiutawala, fedha na shughuli nyengine zote za uchaguzi, ikiwemo kumshauri Mkurugenzi wa Tume hiyo.
Divisheni ya pili ni ya uchaguzi ambayo itakuwa ikimshauri Mkurugenzi kuandaa utekelezaji wa taratibu za uandikishaji wapiga kura, uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi, upigaji kura, kuhesabu na kutangazwa kwa matokeo.
Divisheni ya tatu ni ya utawala na uendeshaji itakayosimamia shughuli za mafunzo kwa wafanyakazi, uajiri na haki za wafanyakazi kwa kuzingatia kanuni za utumishi.
Divisheni ya nne ni ya habari na uhusiano itakayokuwa na majukumu ya kujenga uhusiano kati ya vyombo vya habari na Tume na utoaji wa elimu kwa wananchi.
Divisheni ya tano ni ya fedha, ukaguzi na bajeti itakayokuwa na majukumu ya kuandaa bajeti ya fedha na malipo yanayofanyika kuhakikisha yanakidhi mahitaji yote ya upatikanaji na utumiaji wa fedha.
Divisheni ya sita ni ya sheria itakayofanyakazi ya kumshauri Mkurugenzi wa Uchaguzi masuala yote ya sheria za uchaguzi na kuwa Mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi mahakamani wakati inapohitajika kutoa au kujibu hoja kuhusu masuala yote ya uchaguzi yanayotokana na Katiba ya Zanzibar, Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zinazotungwa.
Mapendekezo mengine...
Kuwepo na ofisi katika kila wilaya ili kuendeleza zoezi la uandikishaji wapiga kura watakaokuwa wamefikisha umri unaotakiwa kisheria.
Kuangalia watu waliohama katika maeneo na kuingia katika maeneo mengine, ili kuhakikisha wanashiriki katika uchaguzi bila matatizo yoyote.
Sasa kama bado una dukuduku soma hapo juu vizuri, kama hukufahamu uliza swali na sio kulia lia hapa.