Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
Karume ateua Tume ya Uchaguzi Zanzibar
naam jee tume hii itakuwa ni jibu la wazanzibari? jee tume hii itaweza kutuvusha tusirejeee tulipotoka au kufikia walipofika ndugu zetu wakenya?
*Ni ya wajumbe mchanganyiko wa itikadi
Na Ali Suleiman, Zanzibar
RAIS Amani Abeid Karume, ametangaza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) mpya na kumteua Bw. Khatib Mwinchande Khatib, kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za Ikulu iliyotolewa jana, wajumbe wa Tume hiyo wakiwamo wawili kutoka CUF ambao ni Bw. Ayoub Bakari Hamad na Wakili wa Kujitegemea, Bw. Nassor Khamis Mohamed.
Wengine ni Bw. Said Bakari Jecha, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Jaji Omar Othman Makungu, Bw. Abrahman Rashid Mohamed na Bibi Mwanabakari Maalim Ahmed, ambaye ni mjumbe pekee mwanamke katika Tume hiyo.
Uteuzi huo umekuja baada ya Tume ya awali iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Masauni Yussuf Masauni kumaliza muda wake.
Katika Tume iliyopita, ni mjumbe mmoja pekee aliyerudi ambaye ni Mwenyekiti, Bw. Mwinchande.
Tume hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwamo kufanya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Pia tume hiyo wakati ikiwasilisha taarifa yake kwa Rais ilisema yapo marekebisho yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresha uchaguzi mkuu kuwa huru na wa haki zaidi.
naam jee tume hii itakuwa ni jibu la wazanzibari? jee tume hii itaweza kutuvusha tusirejeee tulipotoka au kufikia walipofika ndugu zetu wakenya?