Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Kikatiba, kisheria na kikanuni Muswada binafsi unaruhusiwa kuwasilishwa Bungeni. Huu ni Muswada ambao huwasilishwa na Mbunge tofauti na ile miswada inayowasilishwa na Serikali ili kuwa sheria.
Muswada huweza kuwa katika kutunga sheria mpya au kurekebisha zilizopo. Hata Katiba hurekebishwa na sheria inayoanzia kwenye Mswada. Mswada pia huweza kurekebisha sheria mbalimbali kwa wakati mmoja.
Bungeni kuna Kambi Rasmi ya Upinzani inayoundwa na kuongozwa na CHADEMA. Ina Wabunge wa kutosha na wenye haki za kuwakilisha Miswada binafsi kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa. Na wamechaguliwa tangu mwaka 2015.
Ni CHADEMA hao hao ndiyo wanaoshikilia hoja ya uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi hapa Tanzania. Hoja hii imeanikwa kama vipaumbele vya sasa vya Katibu Mkuu mpya wa chama hicho John J. Mnyika (Mb). Hoja hii inashikiwa bango mwaka huu; mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Kwanini?
Walikuwa wapi tangu mwaka 2015 kujenga hoja hii na hata kuwasilisha Muswada binafsi Bungeni kuhusu suala hilo? Kwanini nafasi hiyo ya Muswada binafsi haikutumika hadi sasa kuitaka Serikali kuwasilisha Muswada huu ya suala hilo kwa Hati ya Dharura?