- Thread starter
- #41
Ngoja tuone mwisho utakuwajeSiamini kama waliamua kuongopa lakini wamekosa uelewa wa industry. Ifahamike kuwa Mruma na wenzake ni academicians. Hawa ni wataalam wa theories lakini hawaishi kwenye Dunia halisia ya kiutendaji (industry practical world). Hata huko waliko, nina hakika watakuwa hawana amani, na watakuwa wanajilaumu kwa kukosa umakini.
Kuna uwezekano mkubwa maabara iliyotumika haina uwezo wa kufanya kazi iliyokusudiwa kwa usahihi. Na tatu, wahusika wameshindwa kutambua method ipi ya kimaabara iliyotakiwa kutumika kwa maana ya kujua nini kinatoka na kwa kiwango gani toka kwenye concentrate wakati wa recovery.