Tume huru ndiyo silaha ya mwisho, isipopatikana ndio mwisho wa upinzani Tanzania

MsemajiUkweli,

Yes mkuu, nimeuliza swali JF kwa ID ya hapa kushirikisha wengi tujadili. Lakini ninayo nafasi ya kuuliza viongozi wakuu wa Chadema USO kwa USO "kwa nini hamjamjibu Chakaza au MsemajiUkweli hoja yake kule JF?"

Hivyo ukipenda kuamini nasema nini karibu. Suala la Tumehuru huna haja ya kuniuliza muundo mie wakati serikali inao uwezo kama ina nia njema kuchukua mifano ya tume bora toka nchi zilizofanikiwa, mabunge ya Commonwealth nk.

Lakini 49% waweza kuwa wawakilishi wa vyama na 51% wataalamu wa sheria na wasio wanasiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tume huru itaundwa na kina nani? Kama wapinzani wenyewe ndio hawa tia maji tia maji wananunulika ata kwa buku hao watakaounda Tume huru watashindwaje kununulika?

Sent using Jamii Forums mobile app


Cc zero IQ
Bora wewe umesema ukweli kuwa mnawanunua wapinzani.Fikiria hii hofu ya Tume Huru ni ya nini kama mnakubalika?
CCM inaogopa hata Katiba mpya,ni aibu kwa chama kikongwe kama hiki?
Mimi sio mwanachama wa chama chochote ni mchangiaji huru

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni namna ulivyochangia,ni kama wanaCCM wanavyochangia kuwa hakuna haja ta Tume Huru ya Uchaguzi eti iliyopo ni huru kwa sababu IPO kisheria.
Je,unaunga mkono tudai Tume Huru kwa nguvu na akili zetu zote?
 
CCM haiwezi kuleta tume huru kwa sababu viongozi wake. Wana utamaduni wao na malengo yao siyo HAKI maana yake siyo kutenda haki. Watu waovu hawawezi kutoa haki, wakiwaachia wananchi kuamua hata kura millioni moja hawazipati.
Na HAKI itatendeka, shetani hawezi kuruhusu mtumishi wake atende haki

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha..mjue kusoma alama za nyakati, nakuhakikishia hata Mbowe apewe umwenyekiti wa tume ya uchaguzi JPM hatopata chini ya 95% ya kura za urais, endeleeni kutukana na kuandamana humu jf na kujiona nyie ndo "watanzania" wenye maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupata Tume huru ya Upinzani yapaswa kuwa ni hitaji la Wananchi wote wa Tanzania na si la viongozi wa vyama vya upinzani au wa madhehebu ya kidini. Je watanzania wako tayari? Kama wako tayari wanapaswa wafanye nini?

Mwaka 2018 yule dada wa California Mange Kimambi alifanya uhamasishaji mkubwa sana kupitia mitandao na kimsingi Magufuli binafsi na serikali yake waliogopa sana. Ushahidi kuwa waliogopa tuliuona kwa namna alivyoiweka Polisi na majeshi kuwa wanafanya mazoezi kwenye maeneo ya hadhara kuonyesha utayari wa kupambana na resistsnce yeyote. Pili ili kuudanganya umma alijipangia kuwa anazindua projects mbali mbali ilikujifanya ni mchapakazi.

Tume huru tunaitaka lakini tusiviachie vyama vya upinzani pekee na viongozi wa kidini. Tukiambiwa tuingie barabarani, tusianze uwoga. na kwa Tanzania huyu Magufuli ni muoga sana na wala siyo jiwe kama mnavyomwita. I assure you hata nusu saa tu tukiisimamisha Dar esSalaam, tunapata Tume Huru same day. Ila uwoga wetu ndiyo unamfanya yeye aonekane mungu mtu kwa akina Makonda na Agrey Mwanri na DC wa Longido.

Sudan Omar Bashir likuwa mwamba lakini binti wa miaka 22 ndiye aliyeongoza maandamano. Saa hizi Omar Bashir naye anapangiwa na nyampala zamu ya kubeba ndoo ya mavi rumande. ndiyo iwe Magufuli?? mwepesi kama karatasi
 
Hahaha..mjue kusoma alama za nyakati, nakuhakikishia hata Mbowe apewe umwenyekiti wa tume ya uchaguzi JPM hatopata chini ya 95% ya kura za urais, endeleeni kutukana na kuandamana humu jf na kujiona nyie ndo "watanzania" wenye maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo utoto sasa! Kama ni hivyo kwanini kuiogopa? Maneno maneno ya kwenye kanga hayana maana twende kwenye uasilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini tujiulize pia kwamba vipi je hiyo katiba mpya na Tume huru zikiwepo alafu bado ccm wakashinda nini tena tutadai ili upinzani ushinde?
 
Stuxnet,
Cha muhimu hata viongozi wanaotaka tuingie barabarani wahakikishe nawao wanakuwa pamoja nasisi hapo barabarani sio tunapigwa virungu wao wako sehemu wanakuywa wine.
 
Lakini tujiulize pia kwamba vipi je hiyo katiba mpya na Tume huru zikiwepo alafu bado ccm wakashinda nini tena tutadai ili upinzani ushinde?
CCM wakishinda kihalali hilo ndiyo hitaji letu,ila msilazimishe kupendwa na kukubalika wakati refa ni wenu,uwanja wenu na mashabiki wenu halafu mwajisifu kushinda kwa kishindo.Tunachodai ni usawa katika mchakato mzima wa kupata viongozi na siyo watawala wakutufanyia usanii hata kwa masuala muhimu ya kitaifa.
 
Tume huru inataka sacrifice, Jaji mkuu ateuwe wajumbe wasiotokana na vyama kuunda mfumo wa tume huru.
Wajumbe wakimaliza mchakato.Jaji Kiongozi apendekeze majina ya wajumbe wa tume huru.
Bunge la Jumuiya ya Madola ikiiiongozwa na serikali ya Uingereza ipitishe majina ya wajumbe.
Lakini Ingependeza miiko na kanuni za Uchaguzi usiopendelea upande wowote zikapitiwa upya.
 
Back
Top Bottom