Tumbua tumbua ya Rais Magufuli si salama kwa CCM

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
I am not bound to win, but I am bound to be true. I am not bound to succeed, but I am bound to live by the light that I have. I must stand with anybody that stands right, and stand with him while he is right, and part with him when he goes wrong.
By: Abraham Lincoln

Falsafa inayoishi ya aliyekuwa Rais wa Marekani Abraham Lincoln " sina mipaka ya kushinda, lakini nina mipaka ya kuwa mkweli, Sina mipaka ya kufanikiwa, lakini nina mipaka ya maisha ya nuru niliyo nayo, ni lazima nisimame na yeyote atakaye simamia haki na nitasimama naye akiwa sawa, isipokuwa atakapokuwa kinyume.

Yanayotokea awamu hii ni kinyume na matarajio ya Watanzania wanaoitwa wanyonge. Kwa kuwa unyonge wao ni faida kwa wajanja wachache.

Ndiyo maana uhalisia wa unyonge wao, wana nyongwa kwa kukamuliwa kodi zinazofanywa neema kwa wateule wachache, wapiga deal.

Niliwahi kusema kuwa wasomi wanamuangusha Rais, kwa kuwa wamesoma madhaifu ya Rais, imekuwa rahisi kuwa kwao kucheza na saikolojia yake.

Utashi wa Rais wetu ni sifa na mapambio, huo kwake ni ulemavu. Kwa kulijua hilo watendaji wake wameamua kucheza na akili yake kwa kumsifia kwa nyimbo na ngonjera, wakati huo huo wakitafuna keki ya taifa watakavyo.

Mbali na hayo, niliwahi kutahadhalisha kuwa huenda ufisadi katika fedha za umma ni mkubwa kuliko awamu zote za serikali zinazo ongozwa na CCM, watu walibisha na wengine kutukana.

Sasa yaliyojiri leo yanathibitisha uhalisia wa maandiko yangu mengi.

Toka kuingia kwa serikali hii madarakani, serikali imeikuwa mkanyagaji mkubwa wa katiba na mvunjaji mkubwa wa sheria za nchi.

Pamoja na kuapa kuilinda katiba, watendaji wote wa serikali wakiongozwa na Rais wamekuwa ndiyo wavunjaji wakubwa wa sheria, lakini pia wapotoshaji wakubwa wakidhani Watanzania wa leo ni wajinga!

Ikitokea mkadhani sisi wajinga mtakuwa mnakosea, japo Rais alikwisha watahadharisha kuwa sisi si wajinga, na kama wajinga basi ni wale wafukuza upepo wa CCM wanaofikiri kuwa kukosoa ni kukosa uzalendo.

Huwezi kuwalaumu moja kwa moja wasomi hawa waliogeuka kuwa majizi bila kuangalia udhaifu umeanzia wapi!

Maamuzi ya hovyo ambayo yamekuwa utamaduni kwa serikali hii ni maamuzi binafsi yanayokiuka sheria na mwongozo wa nchi, kwa maana ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Rais amekuwa akiibua miradi mikubwa inayogharimu fedha nyingi za umma bila idhini ya wananchi kwa maana ya bunge la Jamhuri ya Muungano.

Hali inayoondoa usafi wa matumizi ya umma, inayochukuliwa kama easy going.

Mathalani unakuwa na company, lakini kwa kuwa wewe ni mkurugenzi unaamua kuchota fedha za company bila kufuata utaratibu wa uendeshaji company hiyo, huo ni ubadhirifu unaotoa mianya kwa watendaji wako kuchota kwa staili yako uliyoianzisha, na mwisho wa siku company inaingia madeni makubwa yasiyo na tija then unamtafuta mwizi wakati wewe mwenyewe si msafi katika matumizi ya fedha za company.

Kwa mujibu wa sheria ya bajeti, manunuzi ya umma yatapitia na kuidhinishwa na bunge, ndipo serikali itafanya utekelezaji wa bajeti waliyo ileta yenye baraka za bunge letu, nao watafuata sheria ya manunuzi kwa kutangaza tender bid au kwa mfumo wa cortation, kwa kuzingatia sheria na viwango vya manunuzi.

Tumeona serikali ikiidhinisha billions of shilling kwa ujenzi wa uwanja wa Chato bila idhini ya bunge, tumeona manunuzi ya ndege zaidi ya 10 ambayo bunge pia haikuidhinisha.

Tumeona mikataba ya madini ya kimya kimya, wakati kuna kamati ya bunge ya nishati na madini na bunge likipata taarifa kupitia vyombo vya habari.

Kwa mantiki hii, kwa saga la Kangi ni muendelezo wa matendo ya kiongozi mkuu kwa anayoyafanya, ndio maana hoja ya Mh. Zitto Zuberi Kabwe inapata mashiko, kuwa kwa kuwa mchongo hakuanzia kwa Rais asiyefuata sheria ya bajeti kwa maslahi binafsi ndiyo maana deal la Lugola na wenzake limemkera Mkuu.

Kama alivyosema Rais Watanzania si wajinga nami nasema mtoto umleleavyo ndivyo akuavyo.

Tumeacha misingi ya sheria, tunaendesha nchi kwa mazoea, na kwa kuwa tuna dola iliyo kosa weredi, tumeruhusu kushughulikiwa ili kulinda maslahi binafsi ya wachache.

Yote haya yanasababishwa na mfumo mbovu unaolindwa na katiba isiyo na meno, inayotoa mwanya kwa wakosoaji kushughulikiwa na vyombo vya dola.

Kwa kulitambua hilo na kwa udhaifu wa katiba yetu hakuna aliye salama ndani ya CCM, kwa kuwa mfumo uliopo unamtengenezea hata malaika mianya ya kuwa fisadi.

Kwa kudhihirisha hilo tumbua tumbua ya Rais Magufuli haiwezi kuiacha CCM salama ikiwa tutafuata misingi ya utawala bora.

Ndiyo maana falsafa ya Abraham Lincoln inapokuwa na nguvu. Inatoa mwelekeo wa nchi yetu wapi yatupasa kwenda na kwa mfumo upi.

Ndani ya CCM hakuna msafi, wote wamechafuka, takribani kila wizara ina uchafu kwa staili hii ya chukua chako mapema CCM inapoteza legitimacy ya kuwaongoza Watanzania, kwa kuwa mfumo wa chama chao umeruhusu kuwanyonya Watanzania.

Ni wakati sasa wa kuamua wapi tunaipeleka nchi na nini mustakabali wa rasilimali zetu.

Hatuwezi kuendesha nchi kama gari lisilo na brake, ni lazima tujiulize nini hatima ya ufisadi unao fanyika kwa kukata mzizi na asili ya ufisadi wenyewe, vinginevyo tumbua tumbua ya Rais Magufuli haitakuwa na faida kwa nchi zaidi ya tafsiri ya kuzungukana kwenye deals.
 
Kama ''nitakubaliana'' na hoja yako hii uliyosema;
''Ndani ya CCM hakuna msafi, wote wamechafuka, takribani kila wizara ina uchafu kwa staili hii ya chukua chako mapema CCM inapoteza legitimacy ya kuwaongoza Watanzania, kwa kuwa mfumo wa chama chao umeruhusu kuwanyonya watanzania''.

Naomba ushauri wako, ni chama gani tukichague ambacho kina legitimacy ya kuongoza watanzania?
 
Kama ''nitakubaliana'' na hoja yako hii uliyosema;
''Ndani ya CCM hakuna msafi, wote wamechafuka, takribani kila wizara ina uchafu kwa staili hii ya chukua chako mapema CCM inapoteza legitimacy ya kuwaongoza Watanzania, kwa kuwa mfumo wa chama chao umeruhusu kuwanyonya watanzania''.

Naomba ushauri wako, ni chama gani tukichague ambacho kina legitimacy ya kuongoza watanzania?
Piga chini jiwe na ccm chagua chama/ Mtu umpendaye

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • tapatalk_1577999380187.jpeg
    tapatalk_1577999380187.jpeg
    36.4 KB · Views: 1
Nimchague yupi na chama gani?
Hoja siyo nani wa kumchagua wala chama gani cha kukichagua, jambo la muhimu ni kuwa na mfumo usioruhusu chama kinachokumbatia uhalifu kuwa katika madaraka wala mtu yeyote, bila kujali ni wa chama gani, asiyesimamia katiba na sheria, kupewa madaraka ya Urais.

Na hayo yote hayatawezekana kama hatutakuwa na katiba mpya. Bila kuwa na katiba mpya na mifumo inayozuia kiongozi au chama kufanya lolote wanalotaka hata kama ni kinyume na taratibu, hatutakuwa na uhakika na chama chochote au mtu yeyote kutotumia vibaya nafasi atakayopewa.

Tunaweza kuichukia CCM, tunaweza kumlaumu Magufuli, lakini tusipokuwa na mifumo imara ya udhibiti wa utawala, wanaweza kuja wengine, wakafanya mabaya kuliko hawa waliopo.

Sasa hivi, mfumo wetu wa utawala unategemea zaidi utashi wa mtu badala ya mifumo imara ya utawala. Na wala tusijidanganye kuwa hata huko nyuma tuliwahi kuwa na mifumo ya namna hiyo. Zaidi imekuwa ni kutegemea matakwa ya Rais, na siyo vinginevyo.

Tusipokuwa na mifumo ya udhibiti, kuna siku tutakuja kusema ni aheri ya Rais Magufuli, alinunua ndege bila ya kufuata taratibu za manunuzi, angalao ndege zilionekana maana anaweza kuja mtawala ambaye hatafuata taratibu za manunuzi, na aluchokinunua pia hamtakiona.

Tunatakiwa kuwa na katiba mpya yenye nguvu thabiti. Tusitake katiba kwaajili ya kuiondoa CCM, au kumwondoa Magufuli, au kuiingiza CHADEMA au ACT, bali katiba itakayolenga ustawi wa Taifa letu. Katiba itakayolazimisha kila mtu kutendewa haki anayostahili.
 
Bams,
Huwa sikubaliani na wewe katika masuala mengi lakini kwa mawazo yako haya ninakubaliana nawe!

Tukubali au tukatae, uwepo wa katiba mpya unategemea utashi wa watawala ndani ya serikali na bungeni kuwa wamoja. Tatizo la nchi yetu wanasiasa wanatumia dhana ya katiba mpya kufikia malengo yao ya kiutawala badala ya malengo ya taifa kwa ujumla.

Ninaamini uwepo wa nchi mbili ambazo zina historia tofauti kunasababisha pia ugumu wa kupatikana kwa katiba mpya.

Sioni kwa sasa uwepo wa katiba mpya kutokana na mgawanyiko wa wananchi uliojitokeza wakati za zoezi la kuandika katiba inayopendekezwa ambayo kwa sasa iko kwenye ''makabati''.

Hata hivyo kumbuka katiba sio mwarobaini pekee wa matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
 
Rais anayetumia fedha nyingi kwenye miradi isiyofuata bajeti wala kuwa na ruhusa ya bunge, anamfukuza kazi Waziri anayetymia fedha nyingi kwenye miradi isiyofuata bajeti wala kuwa na ruhusa ya bunge.

Hiki kama si kichaa ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya ccm kutofuata sheria na kuviua vyama pinzani sasa wanachama wake wanasema hakuna chama mbadala wakati wao ndio wameviua vyama pinzani!!!CHADEMA INAFAA KUWA CHAMA MBADALA LAKINI CCM INAKIUA KWA MTUTU WA BUNDUKI NA MAHAKAMA!!RIP:-ALPHONCE MAWAZO,BEN SAANANE,CHACHA WANGWE N.K!!!
 
Baada ya ccm kutofuata sheria na kuviua vyama pinzani sasa wanachama wake wanasema hakuna chama mbadala wakati wao ndio wameviua vyama pinzani!!!CHADEMA INAFAA KUWA CHAMA MBADALA LAKINI CCM INAKIUA KWA MTUTU WA BUNDUKI NA MAHAKAMA!!RIP:-ALPHONCE MAWAZO,BEN SAANANE,CHACHA WANGWE N.K!!!
Mkuu
Vyama hvyo vilipopewa nafas ndo vikatuletea lowasa kwenye steji atuburudishe
Na ndo vyama hvyo vitakavyotuletea Membe 2020 kwenye steji
Vp ishakuwa fiesta au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bams, Well
Said
Mkuu tuliona kwenye bunge la katiba
Watu waliishia kupiga posho tu, wakaganda kwny hoja za kipumbavu pumbavu tu yan coz hawakwenda na maslah ya taifa coz watu walienda na matakwa yao ya kisiasa, matakwa ya vyama vyao.
Mchakato ukakwama had kaja mtu mwingine kitin ambaye hatak kuona hyo ajenda mezan


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ''nitakubaliana'' na hoja yako hii uliyosema;
''Ndani ya CCM hakuna msafi, wote wamechafuka, takribani kila wizara ina uchafu kwa staili hii ya chukua chako mapema CCM inapoteza legitimacy ya kuwaongoza Watanzania, kwa kuwa mfumo wa chama chao umeruhusu kuwanyonya watanzania''.

Naomba ushauri wako, ni chama gani tukichague ambacho kina legitimacy ya kuongoza watanzania?
Mkuu kwanza nikusifu kwa andiko lililotulia na linalosimama ktk kweli, hasa hiyo Quote ya mstarin wa kwanza nimeipenda mno. tatizo la vijana wa Tz. ni kukosa akili za kuchambua mambo na kujua ukweli. hili ni donda ndugu hasa kwa walio ccm tena hadi wabunge wao ambao ni bendera fuata upepo!
 
Mfumo ni tatizo kubwa sana,lakini pia kwa kuwa katiba yetu ni katiba - pozo inatoa mwanya wa kulazimisha deal.

Mwalimu aliliona hili ndo maana akasema kwa katiba hii tukimpata rais kichaa tumekwisha.

Pia alionya na kuwatia moyo vijana jeuri wenye kuhoji na kukemea viongozi wabadhirifu wanao cheza na rasilimali za taifa
 
Back
Top Bottom