kuna dada fulani kila anapofanya tendo la ndoa na mumewe anapata maumivu ya tumbo once baada ya kumaliza kwa tendo ilo,maumivu hudumu kwa muda mrefu,,ameshaenda spitali but hajapata ufumbuzi,,naomba msaada wenu madocta....
Mpe pole sana mdada, maumivu ya tumbo anayoyapata yanaweza kuwa ya aina mbili, inawezekana ni kwa sababu ya misuli inayoshikilia kizazi kwa ndani (uterine ligaments) inavutwa sana wakati wa tendo la kujamiiana (over stretched) au inaweza kusabibishwa na infection kwenye kizazi na kibofu cha mkojo (cystitis).
Lakini pia baadhi ya wanawake wanakuwa na viungo vya uzazi vimelegea (laxy pelvic organs) ambapo husababisha kizazi kushuka kidogo sehemu ya ukeni (genital prolapsy) hawa nao hupata maumivu wakati wa kujamiiana. Kizazi hulegea pale ambapo mama anakuwa amezaa watoto wengi , au alikaa kwenye uchungu kwa muda mrefu, na wengine huzaliwa na tatizo hilo (congenital).
Uvimbe kwenye kizazi au kwenye ovaries huweza kusababisha maumivu ya tumbo baada ya kujamiiana.
Ni vizuri akamwona mtaalamu bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi (obstetrics and gynecologist) iliachunguzwe vizuri.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.