Tumbo linamnyima raha mchumba wangu jamani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumbo linamnyima raha mchumba wangu jamani.

Discussion in 'JF Doctor' started by Mliga, Oct 15, 2012.

 1. M

  Mliga Senior Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu kwa heshima yenu naomba mnisaidie kuirudisha furaha ya mchumba angu ilopotea tangu aanze kusumbuliwa na tumbo. Tulifuatilia hospital wakatuambia dawa ni kumtandika MIMBA Ndo atapona! Tatizo suala la mimba yamekaa vibaya sababu hatukupanga, na isitoshe binti wa watu bado anapekua madaftari so ntampa mzigo mno na pia bado hatujaoana kwahyo inaweza leta shida zisizo za lazma. Naomba msaada kama kuna tiba tofaut na hii, maana vilio haviishi had naogopa kupokea sim yake, ila alinigusia kuwa aliambiwa na wenzie eti ni "chango!" yaani hata sielewi! Nawasilisha wakuu.
   
 2. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu pole kwa kuuguza,...ila naomba kuuliza unamaanisha ulishauriwa umpe mimba ndiyo atapona tumbo mkuu?!!
   
 3. M

  Mliga Senior Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu ndio ivyo walivyo nishauri aisee, na wakasema akishapata hiyo mimba tu matatizo yote yataisha ila ndo ivyo hali hairuhusu!
   
 4. a

  amigooo Senior Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona kama huo ushauri unaosema wa Hospitalini hauna mashiko? Upo serious na mada yako?
   
 5. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yaani natoka ban nakutana na uzi kama huu.Sasa ushauri wangu ni huu kwanza uwe unapokea simu yake halafu fanya mpango mpeleke india haraka iwezekanavyo.
   
 6. Vegetarian

  Vegetarian JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 80
  Pole sana mkuu,japo hujaweka wazi,najuwa unazungumzia tumbo la hedhi.Tafuta tangawizi na ukwaju kwa uwiano wa 1:2 Mf. (kg 1tangawizi) kwa kg 2)ukwaju. Safisha ukwaju,menya tangawizi,changanya tia maji Lita 3,chemsha,mgonjwa anywe kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5. KUMBUKA dawa hii inanywewa ikiwa ktk hali ya uvuguvugu,dawa ikiisha kabla,andaa kwa uwiano tajwa,ili siku zote 5 zitimie.
   
 7. M

  Mliga Senior Member

  #7
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nko serious sana mkuu, hata mi nlishangazwa lakini kutokana na kutokuwa na utaalam wa kitabibu ikabidi niwe mpole. Kwakweli anateseka mno hasa anapokaribia kipindi cha hedhi.
   
 8. M

  Mliga Senior Member

  #8
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwakweli mkuu umepitia humo humo, yaani kikikaribia kipindi cha hedhi hali ndo inakuwa mbaya mno, tena ukizingatia yeye huwa anavusha hata mwezi! Nashkuru sana kwa ushauri wako ngoja niufanyie kazi naamini utamsaidia.
   
 9. G

  GlorytoGod Senior Member

  #9
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 8, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ila pia kwa ushauri wangu kama wewe ni mkristo naomba umshauri aende kwenye maombi, mimi nilikuwa na hilo tatizo ikifikia kipindi kama hicho siku 3 siendi kazini niliagiziwa dawa zote lakini iliyoniponya ni baada ya kufanyiwa maombi na kubeba hilo tatizo kama mzigo wakati ninapoomba. Kuna watu wana tabia ya kurushia wasichana mapepo yanaenda kukaa kwenye kizazi ili kila anapokaribia hedhi awe anaumwa ila nina imani kama mimi nilipona naye atapona maana nilikuwa naumwa asikuambie mtu anayejua adha niliyokuwa naipata ni mungu aliyeniponya.
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hakuna daktari atakae kwambia "mtandike mimba" mkeo. Hakuna

  Chagueni maneno ya kutumia mnapozungumzia watu mnaowaheshimu
   
 11. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dawa ni mazoezi kuna ambao nilikuwa nasoma nao mpaka wanazimia kwa ajili ya tumbo na kilichowasaidia ni mazoezi
   
 12. M

  Mliga Senior Member

  #12
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hilo neno sio neno zuri kwa mtu unayemuheshimu, na nimelitumia makusudi kuonyesha kuwa daktari hakumuheshimu mchumba wangu kwa ushauri ambao haukuzingatia mazingira aliyonayo kama yana mruhusu kubeba mimba. So sikuandika ili kumkosea heshima mtarajiwa wangu.
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Daktari yeye kazi yake ni kukutajia dawa. Dawa ni kuwa mjamzito. Ulitaka uambiweje?


  Daktari hajamvunjia heshima hata chembe huyo mchumba wako, ulomvunjia ni wewe
   
 14. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ni vema ukubali kwamba si vema kutumia lugha ya "kutandika mimba" au ya namna hiyo katika mazingira yoyote.
   
 15. M

  Mliga Senior Member

  #15
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa Mkuu ila cha umuhimu ni kupata msaada wa kulimaliza tatizo lake kwa njia tofauti na ujauzito, sababu hayuko tayar, na vilevile haliko katika mipangilio yetu kwa sasa.
   
 16. Chocs

  Chocs JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 8,202
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Kwa tumbo la uzaz(chango)weng tukienda hosptal tunaulizwa "je,upo tayar kupata mtoto?" whch means kubeba mimba na kujifungua ndiko humaliza tatizo..kwa ushaur na njia mbadala achemshe maj aweke kwenye chupa awe anajikanda,ale vyakula vyenye calsium kma dagaa,anywe maziwa fresh lakn ayaweke tanbond ya kutosha na anywe yakiwa yamoto kias.
  Dawa za hosptal zipo ila si nzuri hasa kwa mwanamke ambae hajapata mtoto bado.
   
 17. M

  Mliga Senior Member

  #17
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashkur kwa ushauri wako, tena tumbo lenyewe linauma kwenye kitovu au chini ya kitovu. Hayo maumivu anayolalamika, Aisee we acha tu
  ...!
   
 18. Rapha

  Rapha Tanzanite Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 631
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hospitali gani walokupa huu ushauri?!
   
 19. M

  Mliga Senior Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa uchache tu ni hospital ya Wilaya Korogwe(magunga), ya Wilaya ya Bariadi(somanda) na zahanati tofautitofauti alizoenda mambo yanapomzidia.
   
Loading...