Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Operesheni ya vigogo wa biashara ya dawa za kulevya au operesheni ya kusaka waathirika/mateja?
Kwa dhana ya kilichooneshwa jana kwa mbwembwe za kuhutubia mikono mifukoni, bila shaka kinachokusudiwa ni mateja, basi Kinondoni, Ubungo, Sinza etc mbona wako nje nje tu na wanaweza kujaza central police yote. Vinginevyo ni mind game tu.
Mzaha mkubwa kwenye suala zito kama hilo miongoni mwa majanga makubwa ambayo Serikali ya CCM imeshindwa kuyashughulikia kwa sababu wahusika na mtandao wenyewe ni miongoni mwa wale waitwao 'wenzetu'. Hao wasanii wala si miongoni mwa hao waitwao 'wenzetu'.
Vinginevyo operesheni hiyo ianzie na majina ambayo yalishasemwa na wakuu wa nchi kuwa yanajulikana. Hivyo mafaili yako mezani kwao pale jengo kuu. Huyu wa mkoa aombe apewe majina yanayohusu mkoa wake, aanzie hapo.
Kuanzia kinyume chake ni kuweka mkokoteni mbele ya punda.
Vinginevyo tuendelee kujadili anguko la elimu yetu linalojionesha kwenye matokeo mabovu ya wadogo zetu, huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa ufaulu mbovu.