Tumaini Makene huu sio wakati wa kulala, kuwa Active Mitandaoni

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Kwako ndugu Tumaini Makene

Huu sio wakati wa kulala. Nyie ndo Chama Tawala watarajiwa. Dalili zote zinaonesha watanzania wameamka na wako upande wenu.

Ushauri wangu kwako na kwa Uongozi wa CHADEAM, kuweni active sana kwenye mitandao ikiwemo JamiiForums, kuna mawazo mengi mnapewa humu na wadau mbalimbali. Yachukueni na yafanyieni kazi.

Wakati ni huu. Njia ni nyeupe sana kwenu mwaka huu!
 
Ni kweli kabisa, kitengo cha habari cha cdm kimekata pumzi. Kuna mambo kadhaa yanahitaji ufafanuzi wao wako kimya. Kwenye mitandao mbalimbali viongozi wa Cdm wako Active sana, lakini sehemu kubwa unakuta hawachangii mambo yenye manufaa kwa chama, sana sana utakuta wanachangia mambo ya kuchambana na kebehi.

Ni vyema kitengo cha habari kikawa kinatoa taarifa za chama wangalau mara 3 kwa wiki, na kukitokea upotoshaji watoe ufafanuzi iwapo inastahili.
 
Mkumbuke kukurupuka kutolea taarifa jambo lolote nayo sio sifa, lazima wajipe muda wakitoa taarifa iwe credible, sio kutoa taarifa haraka haraka ili tu kuwaridhisha baadhi ya watu.

Unaweza kutoa taarifa haraka majibu yako yakawa sio ya uhakika, kujipa muda kidogo kabla ya kutoa taarifa kwa jambo lolote ni suala la msingi sana.

Kwanza, linaongeza hadhi ya taasisi kwa kuwa na majibu mazito wakati wa kuitoa taarifa utakapofika.

Pili, unawapa waandaaji wa taarifa husika muda wa kutosha kuandaa majibu yatakayowaridhisha wasikilizaji.

Kusikika kila siku kutapunguza attention toka kwa wasikilizaji. Tumeona chama fulani kiongozi wake kila mara hutoa taarifa kuhusu masuala mbalimbali lakini taarifa hizo hazionekani kuwaongezea chochote wao na chama chao, ni kama vile wameshazoeleka kwasababu ya haraka zao.

Kwa wakati huu wa kuelekea kampeni, ni vyema Chadema wakawa active kwenye kutoa taarifa zao, lakini wawe makini wasijegeuka kama ndege, wawe makini na wajiridhishe vizuri kabla ya kutoa majibu.
 
Kabisa CDM waamke na kufanya uenezi kwa nguvu, wananchi wa Tanzania wanahitaji sana kutafuniwa siasa ili wazielewe wasije wakadanganywa na t-shirt na khanga za ccm.
Njia ni nyeupe mitandaoni au mpaka nje ya mitandaoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…