Habari wadau wa HnH,
Kufuatia mvua zilizonyesha kwa wiki hii mfulilizo, Sisi wakazi wa Mabwepande tumepata hadha ya kubomokewa na daraja la tumaini linalounganisha "Kwa Wahanga" na Block 14 Mabwepande viwanja vya Manispaa.
Tulimuita Diwani wetu aje kuona na kutufikishia ujumbe kwa wadau husika akatuambia kwamba ujenzi wa madaraja haupo tena chini ya mkurugenzi wa manispaa bali upo chini ya mkurugenzi wa TURURA hivyo wao hawana "SAY" yeyote.
Mpaka hivi tunavyoongea magari hayapiti,pikipiki hazipiti na hizi mvua zinazoendelea hata wanafunzi wa msingi na sekondary wanapata tabu sana kuvuka kwa jinsi miundombinu ya daraja ilivyoharibika.
Pale kuna mkandarasi anajenga daraja la kudumu lakini mpaka sasa lipo katika hatua ya chini sana na limeshachafuliwa na matope na zege ya kushika chini "landing" ilikuwa bado haijapigwa na tukimuuliza mkandarasi mboma umeacha nondo na marine wazi mda wote hamjamwaga zege akasema walishatoa "order" mda mrefu sana Wazo wapelekewa gari ya zege lakini mpaka muda huu zege haijaletwa.
Tunaomba mamlaka husika watusaidie hata kujenga daraja temporary kwa kutumia maringi madogo yale ya zege ili tuweze kupita pale na pikipiki pamoja na magari.
View attachment 1097933
View attachment 1097937