Tuma cv sasa upate kazi ya uhakika

Tuma cv sasa upate kazi ya uhakika

Vaislay

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Posts
4,532
Reaction score
1,840
Habari ndugu zangu, Natumai kila aliesoma kichwa akapatwa na mshawasha wa kutaka kujua kulikon,
Mimi sio mwajiri ila nataka kuwafahamisha kitu kimoja kwa wale wenzangu na mimi.
Najua tuko wengi tunaohaha na kutafuta kazi kwa njia mbalimbali,lakini sasa jaman tusipokua makini tutaliwa,Kuna matapeli wameingia kwa stail ya kuwaibia wale wanaoomba kazi,kuweni makini kuomba kazi za mitandaon hasa zile za vikampuni uchocho (bubu) kwa jina lingine kampuni zisizo eleweka.....Nimekutana sana na swala hili, kuna wanao kutumia email kwamba uende kwenye interview utakuta sehem hiyo huifaham,ukiomba maelekezo "unajibiwa njoo ukifika ( mf stend) hapo utampigia flani atakuelekeza" utapewa na namba, Hilo janga lilimkuta rafiki yangu akanusurika kuibiwa.email za wengine wanatumia luga ngumu ukiunganisha sentenc unajua kabisa hapa hakuna kitu.
Wengine wanakupigia, kwamba " Hii ni kampun flan inahusika na haya,tumeona CV yako,sasa unatakiwa uje kesho ofisini kwetu sa flan kama wewe ni mgeni ukifika hapo muulizie flan wa hapo ofisin" utafika pale utaulizia labda hilo jina ulilopewa mtu kweli utamkuta mwenye hilo jina but utakuta anakushangaa na wewe na tena ofc hiyo inakua haijatangaza kazi.
Kila mtu anajua kazi za sahzi kama si kujuana bac hela, Wengine wanapiga,anaanza kujieleza vizuri,badae anakuambia,"ofisi yetu ilikua inahitaj watu watano sasa kuna mmoja katolewa kapelekwa kitengo kingine sasa J3 njoo ukiwa umepigia kikazi kabisa na elfu 50 au 150,000 ya chai, tunakuingiza moja kwa moja kwenye system.
Kuna wajinga sasa wasiojua kuiba et anakutumia mesej, anajitambulisha vizuri, hii kazi mshahara ni m1.4 ,usiwe na wasiwasi kazi umepata,baadae anasema tuma 100,000 kwnye tgo pesa, na scanned cert zako kwenye email hii,nimeshaongea na Hr kazi umepata.....KIUKWELI KAMA UKIKURUPUKA NA FURAHA YA KUPATA KAZI UMELIWA,KUWA MAKINI,SHIDA ZAKO ZISIKUTIE MATATIZON,,IGOOGLE HIYO KAMPUNI UPATE UHAKIKA,MANA MAKAMPUNI MENGINE HATA WEB TU HAWANA NA HAO NDO WEZ WENYEWE.

mmh nahisi ungeweza kuleta point yako bila kutumia maneno hayo yote 10,000.imekuwa kama risala

mi nimepiiwa na jamaa wanaitwa tzjoblink wanadai niwatumie laki moja..utapeli huu

we mleta mada umeleta mada nzuri ila hitimisho lako limeifanya mada yako kuonekana haina mvuto.
Si kweli hata kidogo eti kampuni isiyo na web ni matapeli. Tanzania kuna kampuni zaidi ya elfu tano na si zote zina web. Kuwa na website haifanyi kampuni ya kitapeli kuwa si ya kitapeli na kutokuwa na web hakuifanyi kampuni kuwa ya kitapeli.
Kwa ushauri usijaribu mahali popote wakati wowote kumshauri mtu eti kgezo cha kuitambua kampuni ya kitapeli ni kutokuwa ya kitapeli.

asante sana mleta mada tunakushukuru
be blessed umetufumbua macho ingawaje mm nimeshaajiiiriwa ila nitakuwa makini kwa ndugu zangu kuwahabarisha
thanks

Similar Discussions

Back
Top Bottom