Rihana
JF-Expert Member
- Apr 26, 2013
- 498
- 250
Habari za kazi wakuu,
Natoa Taarifa, Juzi usiku kwenye saa Tano nilikuwa eneo la Tegeta Machakani kwenye grocery ndogo, maarufu kwa mama Tomino.
Tulikuwa kama watu watano hivi huku tukitaka kumalizia kinywaji kuondoka ghafla wakaja watu wawili na bodaboda wakiuliza sigara, ghafla tu mmoja akachomoa pistol akasema tuko chini ya ulinzi.
Mimi nilidhani ni askari kanzu maana ilikuwa saa tano kasoro nikataka kuhoji iweje tuwe chini ya ulinzi wakati muda wa kunywa haujafika. Ghafla tukaamrishwa kulala chini wote wakaanza kukusanya pochi simu na kila tulichokuwa nacho.
Mmoja wetu Mr. Dula alijaribu kuhoji iweje watuamuru tulale chini bahati mbaya jambazi mmoja akafyatua risasi ikampata kwenye paja ila tuliwahi polisi Wazo na tukapata form ya kutibiwa akatibiwa Rabinsia hospital kikatolewa kipande cha risasi mguuni na Xray ikaonyesha kuna kimoja kimebaki. Nadhani surgeon atakuwa amesha kitoa.
Jumla tuliibiwa kama laki 9 simu za smartphone mbili zenye thamani ya milioni moja na laki sita pia tumepoteza kadi ya benki ya CRDB. Kwa yoyote mwenye kuona kadi au kitambulisho naomba anijulishe hapa JamiiForums au akiache Kituo cha Polisi Wazo.
Tuliripoti tukio hilo wazo na polisi wakaja eneo la tukio wakalipata ganda la risasi wakasema wanaendelea na upelelezi.
N:B Kuna tabia ya watu wa kada ya katu kupenda kunywa bia kwenye vi grocery vidogo hasa wakati wa jioni. Ni muhimu kuchukua tahadhari maana wezi wanatembea na pikipiki. Sisi tulidhani ni toy pistol kumbe ni chuma kweli. Jambazi huyo ni kijana mdogo tu mwenye umri wa kati ya 28 na 33.
Tuwe macho wakuu wangu.
Asanteni ni mimi dada yenu Rihana