Nilikua Ruvu pia 1976 Operesheni Mapambano!
Hii imekaa vizuri mkuu.RUVU JKT
HIFADHI YA MAISHA YANGU: (NAKUMBUKA NATAFAKARI SANA, NASONONEKA)
1.1 Ni kwanza kondoka kwetu, napenda hilo mjuwe;
1.2 Niko Ruvu nathubutu, kujenga Taifa liwe,
1.3 Kishapo nirudi kwetu, mengineyo nipangiwe,
1.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
2.1 Ninang'arisha viatu, na magwanda niyafuwe,
2.2 Kisha nibebe mtutu, shabaha nijaribiwe,
2.3 Kamwe sitouwa mtu, ila nchi ivamiwe,
2.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
3.1 Ubongo siote kutu, twenda elimu tugawe,
3.2 Twafundisha watukutu, pia wazazi wenyewe,
3.3 Ghafla twaona chatu, wacha mbio tuzitowe,
3.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
4.1 Ruvu Chini shamba letu, ardhi tuitibuwe,
4.2 Tunapanda kila kitu, mpunga na njugumawe,
4.3 Shamba kamwe si msitu, bora mazao yakuwe,
4.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
5.1 Twabeba mapanga yetu, wasitutishe nguruwe,
5.2 Mashoka yaliyo butu, inabidi tuyanowe,
5.3 Tuwezefyeka misitu, mpingo tuuondowe,
5.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
6.1 Ufugaji kazi yetu, wavivu msitujuwe,
6.2 Tule nyama kefu yetu, na maziwa tukamuwe,
6.3 Ngozi nazo ni sapatu, pia jamvi zikaliwe,
6.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
7.1 Afande yu mwanagutu, anenayo muambiwe?
7.2 Adhani atenda utu, siutaki udadawe,
7.3 Tanga nina wangu Fatu, mwambeni asinijuwe,
7.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
8.1 Walojawa ukurutu, wataka waabudiwe?
8.2 Eti sisi 'recruit', adabu sawa tutiwe,
8.3 Liko wapi kosa letu, hadi haya tutendewe?
8.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
9.1 Imara fuadi zetu, nchi hii tu wenyewe,
9.2 Uzalendo sifa yetu, si sawa tuonelewe,
9.3 Wengi wetu Wabantu, haiswihi tuchezewe!
9.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
10.1 Twangoja majibu yetu, ili vyuo tupangiwe,
10.2 Tukanowe vichwa vyetu, mambo mengi tuyajuwe,
10.3 Tuijenge nchi yetu, uchumi wake ukuwe,
10.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
11.1 Sitobadilika katu, pendo langu kwako wewe,
11.2 Tanga wewe u mwenetu, sina wako mfanowe,
11.3 Sitokucheza upatu, daima mimi ni wewe,
11.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
Omari R. Nundu
D Coy, RUVU JKT
27 Disemba 1970
Ndio mwaka JK ilifutwa
Kila mmoja wetu ana uhuru wa kusema na jambo usilolijuwa ni usiku wa kiza hivyo tahadhari ni muhimu kwani ulimi hauna mfupa. Ni tabia murua ya binadamu kuchunguza kujuwa ukweli, kujiridhisha, kuamini halafu ndio kueneza. Ukifanya vinginevyo unapungukiwa na sifa za ukhalifa duniani. Matokeo unaendeleza chuki kuhusu Fulani kitu ambacho ni sifa ya viumbe wengine sio binadamu!
na wewe umeulizwa???Nilikua Ruvu pia 1976 Operesheni Mapambano!
Kiapo mzeee! Yale maneno wanayoapa huku wameshika vitabu vitakatifu yanawazuia kunena. Karibu na mwisho huwa nasikia wanasema ........NA KWA VYOVYOTE VILE SITATOA SIRI ZA BARAZA LA MAWAZIRI.....Mzee Nundu,
Mi nashauri tu kua ni vizuri ukaandika kitabu au vitabu kufumbua hayo yaliyoko moyoni mwako, ukaainisha hoja na matukio kinagaubaga ili sisi wananchi tukupate kwa ufasaha. Haya mashairi ni mazuri lakini hayatupi picha ya nini unataka kusema!
Hivi kwa nini unanitukana? Siruhusiwi kuandika humu mawazo na hisia zangu? Hata hivyo asante sana.na wewe umeulizwa???
au unatafuta umaarufu tu! shut up
Hivi sera sijui sheria ya whistleblowing iliishiaga wapi? Hivi viapo vina sambaratisha taifa.Kiapo mzeee! Yale maneno wanayoapa huku wameshika vitabu vitakatifu yanawazuia kunena. Karibu na mwisho huwa nasikia wanasema ........NA KWA VYOVYOTE VILE SITATOA SIRI ZA BARAZA LA MAWAZIRI.....
Kwangu mimi naona mzee Nundu alishughulikiwa tu, huyu mzee ni mzalendo.
RUVU JKT
HIFADHI YA MAISHA YANGU: (NAKUMBUKA NATAFAKARI SANA, NASONONEKA)
1.1 Ni kwanza kondoka kwetu, napenda hilo mjuwe;
1.2 Niko Ruvu nathubutu, kujenga Taifa liwe,
1.3 Kishapo nirudi kwetu, mengineyo nipangiwe,
1.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
2.1 Ninang'arisha viatu, na magwanda niyafuwe,
2.2 Kisha nibebe mtutu, shabaha nijaribiwe,
2.3 Kamwe sitouwa mtu, ila nchi ivamiwe,
2.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
3.1 Ubongo siote kutu, twenda elimu tugawe,
3.2 Twafundisha watukutu, pia wazazi wenyewe,
3.3 Ghafla twaona chatu, wacha mbio tuzitowe,
3.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
4.1 Ruvu Chini shamba letu, ardhi tuitibuwe,
4.2 Tunapanda kila kitu, mpunga na njugumawe,
4.3 Shamba kamwe si msitu, bora mazao yakuwe,
4.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
5.1 Twabeba mapanga yetu, wasitutishe nguruwe,
5.2 Mashoka yaliyo butu, inabidi tuyanowe,
5.3 Tuwezefyeka misitu, mpingo tuuondowe,
5.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
6.1 Ufugaji kazi yetu, wavivu msitujuwe,
6.2 Tule nyama kefu yetu, na maziwa tukamuwe,
6.3 Ngozi nazo ni sapatu, pia jamvi zikaliwe,
6.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
7.1 Afande yu mwanagutu, anenayo muambiwe?
7.2 Adhani atenda utu, siutaki udadawe,
7.3 Tanga nina wangu Fatu, mwambeni asinijuwe,
7.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
8.1 Walojawa ukurutu, wataka waabudiwe?
8.2 Eti sisi 'recruit', adabu sawa tutiwe,
8.3 Liko wapi kosa letu, hadi haya tutendewe?
8.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
9.1 Imara fuadi zetu, nchi hii tu wenyewe,
9.2 Uzalendo sifa yetu, si sawa tuonelewe,
9.3 Wengi wetu Wabantu, haiswihi tuchezewe!
9.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
10.1 Twangoja majibu yetu, ili vyuo tupangiwe,
10.2 Tukanowe vichwa vyetu, mambo mengi tuyajuwe,
10.3 Tuijenge nchi yetu, uchumi wake ukuwe,
10.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
11.1 Sitobadilika katu, pendo langu kwako wewe,
11.2 Tanga wewe u mwenetu, sina wako mfanowe,
11.3 Sitokucheza upatu, daima mimi ni wewe,
11.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
Omari R. Nundu
D Coy, RUVU JKT
27 Disemba 1970
Mzee Nundu,
Mi nashauri tu kua ni vizuri ukaandika kitabu au vitabu kufumbua hayo yaliyoko moyoni mwako, ukaainisha hoja na matukio kinagaubaga ili sisi wananchi tukupate kwa ufasaha. Haya mashairi ni mazuri lakini hayatupi picha ya nini unataka kusema!
dah....!! ase umenigusa ruvu ndo kambi yangu
AH 3570 SM SYLVESTER PIUS KAKANI
832 KJ RUVU JKT
OP MIAKA 50 JKT
Jun 2013-Sep 2013
KWA MUJIBU WA SHERIA
D COY
RUVU JKT
HIFADHI YA MAISHA YANGU: (NAKUMBUKA NATAFAKARI SANA, NASONONEKA)
1.1 Ni kwanza kondoka kwetu, napenda hilo mjuwe;
1.2 Niko Ruvu nathubutu, kujenga Taifa liwe,
1.3 Kishapo nirudi kwetu, mengineyo nipangiwe,
1.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
2.1 Ninang'arisha viatu, na magwanda niyafuwe,
2.2 Kisha nibebe mtutu, shabaha nijaribiwe,
2.3 Kamwe sitouwa mtu, ila nchi ivamiwe,
2.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
3.1 Ubongo siote kutu, twenda elimu tugawe,
3.2 Twafundisha watukutu, pia wazazi wenyewe,
3.3 Ghafla twaona chatu, wacha mbio tuzitowe,
3.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
4.1 Ruvu Chini shamba letu, ardhi tuitibuwe,
4.2 Tunapanda kila kitu, mpunga na njugumawe,
4.3 Shamba kamwe si msitu, bora mazao yakuwe,
4.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
5.1 Twabeba mapanga yetu, wasitutishe nguruwe,
5.2 Mashoka yaliyo butu, inabidi tuyanowe,
5.3 Tuwezefyeka misitu, mpingo tuuondowe,
5.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
6.1 Ufugaji kazi yetu, wavivu msitujuwe,
6.2 Tule nyama kefu yetu, na maziwa tukamuwe,
6.3 Ngozi nazo ni sapatu, pia jamvi zikaliwe,
6.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
7.1 Afande yu mwanagutu, anenayo muambiwe?
7.2 Adhani atenda utu, siutaki udadawe,
7.3 Tanga nina wangu Fatu, mwambeni asinijuwe,
7.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
8.1 Walojawa ukurutu, wataka waabudiwe?
8.2 Eti sisi 'recruit', adabu sawa tutiwe,
8.3 Liko wapi kosa letu, hadi haya tutendewe?
8.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
9.1 Imara fuadi zetu, nchi hii tu wenyewe,
9.2 Uzalendo sifa yetu, si sawa tuonelewe,
9.3 Wengi wetu Wabantu, haiswihi tuchezewe!
9.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
10.1 Twangoja majibu yetu, ili vyuo tupangiwe,
10.2 Tukanowe vichwa vyetu, mambo mengi tuyajuwe,
10.3 Tuijenge nchi yetu, uchumi wake ukuwe,
10.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
11.1 Sitobadilika katu, pendo langu kwako wewe,
11.2 Tanga wewe u mwenetu, sina wako mfanowe,
11.3 Sitokucheza upatu, daima mimi ni wewe,
11.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
Omari R. Nundu
D Coy, RUVU JKT
27 Disemba 1970
mzee wangu sijakutukana ??? kwanza nakuheshimu sanaHivi kwa nini unanitukana? Siruhusiwi kuandika humu mawazo na hisia zangu? Hata hivyo asante sana.
Sheikh Nundu,
Ahsante kwa beti hizi zilizojaa ujumbe...