Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,463
- 32,989
Kitali hebu ingia mohammedsaid.com
RUVU JKT
HIFADHI YA MAISHA YANGU: (NAKUMBUKA NATAFAKARI SANA, NASONONEKA)
1.1 Ni kwanza kondoka kwetu, napenda hilo mjuwe;
1.2 Niko Ruvu nathubutu, kujenga Taifa liwe,
1.3 Kishapo nirudi kwetu, mengineyo nipangiwe,
1.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
2.1 Ninang'arisha viatu, na magwanda niyafuwe,
2.2 Kisha nibebe mtutu, shabaha nijaribiwe,
2.3 Kamwe sitouwa mtu, ila nchi ivamiwe,
2.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
3.1 Ubongo siote kutu, twenda elimu tugawe,
3.2 Twafundisha watukutu, pia wazazi wenyewe,
3.3 Ghafla twaona chatu, wacha mbio tuzitowe,
3.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
4.1 Ruvu Chini shamba letu, ardhi tuitibuwe,
4.2 Tunapanda kila kitu, mpunga na njugumawe,
4.3 Shamba kamwe si msitu, bora mazao yakuwe,
4.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
5.1 Twabeba mapanga yetu, wasitutishe nguruwe,
5.2 Mashoka yaliyo butu, inabidi tuyanowe,
5.3 Tuwezefyeka misitu, mpingo tuuondowe,
5.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
6.1 Ufugaji kazi yetu, wavivu msitujuwe,
6.2 Tule nyama kefu yetu, na maziwa tukamuwe,
6.3 Ngozi nazo ni sapatu, pia jamvi zikaliwe,
6.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
7.1 Afande yu mwanagutu, anenayo muambiwe?
7.2 Adhani atenda utu, siutaki udadawe,
7.3 Tanga nina wangu Fatu, mwambeni asinijuwe,
7.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
8.1 Walojawa ukurutu, wataka waabudiwe?
8.2 Eti sisi 'recruit', adabu sawa tutiwe,
8.3 Liko wapi kosa letu, hadi haya tutendewe?
8.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
9.1 Imara fuadi zetu, nchi hii tu wenyewe,
9.2 Uzalendo sifa yetu, si sawa tuonelewe,
9.3 Wengi wetu Wabantu, haiswihi tuchezewe!
9.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
10.1 Twangoja majibu yetu, ili vyuo tupangiwe,
10.2 Tukanowe vichwa vyetu, mambo mengi tuyajuwe,
10.3 Tuijenge nchi yetu, uchumi wake ukuwe,
10.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
11.1 Sitobadilika katu, pendo langu kwako wewe,
11.2 Tanga wewe u mwenetu, sina wako mfanowe,
11.3 Sitokucheza upatu, daima mimi ni wewe,
11.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!
Omari R. Nundu
D Coy, RUVU JKT
27 Disemba 1970
dah....!! ase umenigusa ruvu ndo kambi yangu
AH 3570 SM SYLVESTER PIUS KAKANI
832 KJ RUVU JKT
OP MIAKA 50 JKT
Jun 2013-Sep 2013
KWA MUJIBU WA SHERIA
D COY