Tulitizame la Arusha katika angle zote-amani ya nchi ni muhimu kuliko CCM& CHADEMA please moderator

mkisah2

Member
Feb 5, 2011
53
16
Let us think inside the box, outside the box and trash the box and think without a box as well.

Inside the box

CCM wamepanga njama ya kulipua bomu kwenye mkutano wa CHADEMA ili wananchi waogope kuhudhulia mikutano ya chadema. Tuhuma hizi zinakuzwa na maneno ya Mwigulu Nchemba ambaye katika mikutano yake alionya kwamba watakaohudhulia mikutano ya chadema watakufa pamoja.Pia vifo vilivyofanya na polisi kwenye mikutano ya CHADEMA huko morogoro na iringa pamoja na utekwaji na uteswaji wa Ulimboka na wengineo vinafanya watu wengi ikiwamo viongozi wa CHADEMA waamini kuwa CCM ilitumia polisi kufanya hujuma hizi
LAKINI, kwanini yalipuliwe siku ambayo ni mwisho wa kampeni?Lengo lingekuwa ni kuwatisha wananchi wasihudhulie mikutano ya chadema basi bila shaka bomu lingelipuliwa mwanzoni kabisa mwa kampeni.

Outside the box

Kuna wengine wanaamini CHADEMA wamejilipua wenyewe ili kutafuta umaarufu na huruma ya wapiga kura pamoja na kuipaka matope serikali ya CCM pamoja na jeshi lake. Fikra hii inachukuliwa kwa uzitio kwani hata katibu mwenezi wa CCM Nape Mnauye katika tarifa yake kwa vyombo vya habari anatuaminisha hivyo.
LAKINI, kiongozi gani yupo tayari kumwaga damu kwani tunaambiwa bomu lililipuka jirani na jukwaa kuu na miongoni mwa waliokufa ni kiongozi wa CHADEMA. Isitoshe kulikuwa na mpango wa kutengeneza mlipuko mkubwa zaidi ambao ungeleta madhala zaidi kwani Tenki la mafuta la gari la matangazo lilikutwa limepigwa risasi kwa mategemeo lingelipuka.

Trash the box and think without the box

Mimi nafikiri kuna mtu/ kikundi cha tatu ambacho tunatakiwa tukiweke kwenye tafakari zetu wakati tunamtafuta mchawi katika hili. Kikundi hiki kinaweza kuwa ndani ya nchi ama hata nje ya nchi. Tujiulize je ndani ya nchi kuna kikundi kinapenda kuona CHADEMA na CCM kwenye malumbano? Je kuna kikundi ama mashirika ndani ya nchi hakipendi kuona watanzania tunaishi kwa amani?
Je kuna Vikundi vya nje ama nchi za nje ambazo hazipendi kuona watanzania tunaishi kwa amani? Je kuna nchi ama vikundi tuna uhasama navyo?
Ndai ya nchi sina uhakika kama kuna kikundi ama chama cha siasa kisichopenda kuona CCM na CHADEMA wakilumbana ama kinachopenda tuingie kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, labda TISS watakuwa wanajua.
Kuhusu vikundi nchi za nje ambavyo vina uadui na Tanzania, nina uhakika na M23. Kikundi hiki cha wanamgambo wanaopigana Congo ambao inaaminika wanafadhiliwa na serikali za Rwanda na Uganda havijafurahishwa na hatua ya serikali ya Tanzania kupeleka majesi yake kwenda kulinda amani Congo. Sijui vikundi vingine nadhani TISS wana idadi ya ya vikundi tulio na uadui navyo.
Kuhusu nchi pia nina uhakika kwamba tuna uadui na Malawi kutokana na mgogoro wa mipaka kule ziwa nyasa. Pia nina uhakika tuna uhasama na Rwanda na Uganda kwakuwa tumeingilia Maslahi yao kwa kupeleka majeshi Congo. Sina uhakika na nchi nyingine ila nadhani TISS watakuwa wanajuia nchi ambazo tuna uhasama nao kwasababu ndio kazi yao , ingawa Kenya lazima tutakuwa na uhasama nao kwenye masuala ya kibiashara.
Kwanini natilia mashaka vikundi vya nje ya nchi ama nchi majirani zetu?
Kwasababu aina ya bomu lililolipuka katika kanisa la Joseph mfanyakazi Olasiti ni ile ile iliyolipuka katika mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA. Ni bomu la kiwandani na limetengenezwa China.
Mabomu haya ni kwaajili ya majeshi sio polisi.
Ikumbukwe kipindi kile bomu lilipolipuka kanisani , kulikuwa na Tension kubwa sana kati waislam na wakristo. Motive ya mlipuaji ilikuwa ku spark vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wakristo na waislam. Hii ilishindikana baada ya wakristo kuendelea kuonyesha uvumilivu pia ilikuja gundulika kwamba mtu aliyerusha bomu ni mkristo mwenzao. Nadhani dhamira ya kikundi ama nchi iliyotaka tuingie katika Mapambano ya wenyewe kwa wenyewe ili fail.
Wakati huu ambapo kulikuwa na Tension kubwa kati ya mahasimu wa siasa CCM na CHADEMA hapa Arusha tunaona hali hii inajirudia. Motive ni ile ile ya kutaka tuingie kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, wakati huu katu ya wafuasi wa CHADEMA na CCM.
Viongozi wetu wanatakiwa wawe makini sana wanapotoamatamko yao kwani tukianza kuuana hakuna atakayepona. Kwamfano kakukuwa na haja ya Mh Lukuvi ama Nape kutoa matamko ya namna ile ama jeshi la polisi kuzuia wafuasi wa CHADEMA kufanya maombolezo ya wafuasi wao waliouawa katika mlipuko
Halikadhalika hakukuwa na sababu ya viongozi wa CHADEMA kuwatuhumu polisi moja kwa moja kabla ya kuwa na uhakika wa kinachoendelea kwani wakati wa matukio kama ya uchaguzi polisi huwa wanaletwa toka kila kona ya Tanzania kwahiyo sio rahisi polisi walio katika scene kujuana, kitu kinachoweza kutoa mwanya kwa wahalifu ku camouflage kama police na kutekeleza adhma yao(kumbuka tunaambiwa polisi walimtorosha mrusha bomu je tuna uhakika ni polisi wetu, ama ni agents wa maadui zetu?).
NB; Rejea maneno ya rais wa Rwanda baada ya hizi kash kash aliposema Kikwete Kikwete anajidai kupatanisha nchi za wenzake wakati kwake kumshinda. Pia bomu la kanisani lililipuka pindi tu askari wetu walipokuwa deployed kwenda rwanda
;Rejea maneno ya M23 kwenye mitandao yao
;ikumbukwe kenyan hawafurahishwi na our mega development projects kama za ujenzi na upanuaji wa bandari zetu, na reli utajiri wa gas, ujenzi wa bomba na impact zake katika uchumi hapo baadae etc
Sina Chama
Naomba kuwasilisha
 
Subiri na ushahidi wa CHADEMA, kwa sasa tuko msibani. Unaweza kujiona hujui kufikiria
 
Viongozi wetu wanatakiwa wawe makini sana wanapotoamatamko yao kwani tukianza kuuana hakuna atakayepona. Kwamfano kakukuwa na haja ya Mh Lukuvi ama Nape kutoa matamko ya namna ile ama jeshi la polisi kuzuia wafuasi wa CHADEMA kufanya maombolezo ya wafuasi wao waliouawa katika mlipuko.

Wewe unafundisha watanzania kuwa wanafiki wakati watu wanaangamia.. Unataka kupandikiza nidhamu ya woga miongoni mwa watanzania.

Halikadhalika hakukuwa na sababu ya viongozi wa CHADEMA kuwatuhumu polisi moja kwa moja kabla ya kuwa na uhakika wa kinachoendelea kwani wakati wa matukio kama ya uchaguzi polisi huwa wanaletwa toka kila kona ya Tanzania kwahiyo sio rahisi polisi walio katika scene kujuana, kitu kinachoweza kutoa mwanya kwa wahalifu ku camouflage kama police na kutekeleza adhma yao(kumbuka tunaambiwa polisi walimtorosha mrusha bomu je tuna uhakika ni polisi wetu, ama ni agents wa maadui zetu?).

Nenda katoe ushauri huu Lumumba na kuchukua buku 7.

NB; Rejea maneno ya rais wa Rwanda baada ya hizi kash kash aliposema Kikwete Kikwete anajidai kupatanisha nchi za wenzake wakati kwake kumshinda. Pia bomu la kanisani lililipuka pindi tu askari wetu walipokuwa deployed kwenda rwanda

Hivi kwa nini mtu adanganye wakati ukweli unajulikana?... Mbona vielelezo vyote vya polisi kumuua MWANGOSI VIPO humu jamvini lakini wauaji wanazidi kupanda vyeo?

;Rejea maneno ya M23 kwenye mitandao yao
;ikumbukwe kenyan hawafurahishwi na our mega development projects kama za ujenzi na upanuaji wa bandari zetu, na reli utajiri wa gas, ujenzi wa bomba na impact zake katika uchumi hapo baadae etc

Sina Chama... Naomba kuwasilisha

Arusha mabomu hayarushwi na AL shababu wala Aqaida, bali MACCM.


 
Halikadhalika na wewe huna sababu ya kutoa tamko la kuwatilia mashaka Rwanda, Kenya n.k. kabla hujapata uhakika. Eti Kenyan hawafurahishwi........
Bomu tumeambiwa limetoka China, je na lile la kanisani lilitoka China?
 
Let us think inside the box, outside the box and trash the box and think without a box as well.

  • Inside the box
  • Outside the box
  • Trash the box and think without the box
Sina Chama
Naomba kuwasilisha
Umewasilisha nini? Kwamba hatuna serikali? hatuna viongozi? hatuna vyombo vya dola? Au unawasilisha kwamba wewe ni popo, si ndege si mnyama...what are you then? Kuona huoni, kusikia husikii na hata kunusa hunusi! Je hao polisi wananoua watu wanatumiwa na M23, Kenya, Rwanda? What's wrong with us people?

My advice to you mkisah2; at your level of reasoning please stop thinking outside the box, think inside the box! Your vision will become clear only when you can look into your own heart. One who looks outside, dreams; one who looks inside, awakens.
 
unapoteza muda ndugu kuzungumza na hayo madubwasha ya chadema,yamekaa kama mizezeta,bahati mbaya au nzuri waongozaji wa jf huwa hawatoi maoni yaliyo na uzito wa hoja wanaowasuta chadema,wanaweka zile cheap post zinazowapinga chadema,wanafanya usanii kama baba zao. achana nayo hayo
Umewasilisha nini? Kwamba
hatuna serikali? hatuna viongozi? hatuna vyombo vya dola? Au
unawasilisha kwamba wewe ni popo, si ndege si mnyama...what are you
then? Kuona huoni, kusikia husikii na hata kunusa hunusi! Je hao polisi
wananoua watu wanatumiwa na M23, Kenya, Rwanda? What's wrong with us
people?

My advice to you
mkisah2;
at your level of reasoning please stop thinking outside the box, think
inside the box! Your vision will become clear only when you can look
into your own heart. One who looks outside, dreams; one who
looks inside, awakens.
 
Aisee, Athari ya Vurugu za Arusha ni kwa Watanganyika wote, tusijidanganye eti victim litakuwa kundi flan, mleta Uzi kajitahid sana kuleta mjadala wenye Afya ya Nchi ila wavurugaji hawatokosekana hasa wale Vidampa wanaoamin Chama kwanza Nchi baadae, Tuvipe ushirikiano vyombo vya Dola nchi ikivurugika hakuna cha Vyama wala dini wote tuta Suffer iwe Maskin au Tajiri. Ee Allah tuweke Mbali na Wenye jicho la Husda na Jamhuri yetu ya Watanganyika! Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanganyika!
 
Inashangaza namna mwanadamu anavyoweza kujifanya mjinga kwa makusudi kabisa.

Eti kundi la tatu ambalo halitutakii watanzania tuishi kwa amani as if dunia nzima pamechafuka isipokuwa hapa tu.Useless post.
 
Mleta mada hayo uliyonena yanaitaji tafakuri ya kina tatizo humu jf kitu akishazungumza kiongozi wa kisiasa ni marufuku kumkosoa tena zaidi cdm,ni upoyoyo akili zako kukubali kushikiwa na mtu mwengine,

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom