Tulirukia gari kutahamaki tupo kambi ya jeshi

Jf ifungwe kwa mwwka mmoja. Huu uzi unatasha kuhitimishia mwaka 2021.
Hii michezo watoto waliokulia jiji la Ilala hawaijui
 
Sisi tulidandia gari la Mheshimiwa Paul Kimiti kipindi hicho tunasoma chekechea pale Chuo cha Ushirika Moshi, siku hizi wanafundishia Masters yale majengo aisee tulijutaaa, jamaa yupo kimyaa dereva yeye anapangua gia tu, kuruka mtu huwezi unajiona haoo tunarudishwa kwa Mwl. Sibo (RIP) ila utoto raha sana
 
Mambo vp wadau?

Niende kwenye kisa moja kwa moja.

Ile tabia ya kuangalia movie za Rambo na komando kipensi enzi za utotoni zilipelekea wengine kuzi apply kwenye real life🤣🤣 ndiyo yaani unaangalia movie alafu ukitoka hapo kwanza unajiona wewe ndiyo Rambo alafu mtu akikuzingua unajisemea moyoni tu kuwa bahati yako, ngedere wewe sina mjegejo ningekulipua ya kichwa shwaini🤣🤣🤣 yaaani mizuka flan hivi ya kibabe sana.

Sasa bhana katika michezo tuliyokuwa tunaipenda ni ya kudandia magari yaani kuna sehemu ilikuwa mbovu sana, hapo hata uwe na international license lazima uridi gia na lazima upite kwa kupanyenyekea na sisi ndiyo hapo hapo tunarukia kwenye bodi kwa nyuma alafu tunaendelea nae then tukifika mbele tuna jump ile kisoldier japo gari inakuwa bado ke mwendo yaani kiufupi ni kama tulikuwa tuna jaribu kum conviece malaka mtoa roho afanye yake ila MUNGU anasema achana na hao malaika zangu, basi wenyewe tunajiona kama ni ma soldier waliofuzu zile cozi konki za ngazi za juu za ukomandoo tena kule kwa mzee baba federi Castro🤣🤣🤣.

Mchezo huu wa kudandia magari tuliumudu sana na hatukuwahi kukamatwa wala kushtukiwa. Sasa bhana kuna siku kama kawa nikiwa kama mkuu wa kikosi cha makomandoo ikapita gari ila kwa haraka haraka hatukuwa tumewahi kuiona na kwa vile haikuwa na ishara yoyote ya kuwa ipo kitengo gani tuaona mbona easy tu mzee nikatoa ishara kuwa kuna chombo kina kuja tukae tayari kurukia ile imefika kwenye target yetu tuka dandia. Kwa kuwa ilikuwa imefunikwa kwa maturubai basi tukafanikiwa kikosi cha makomandoo wabonezi kuingia nyuma ya gari watoto kama sita hivi.
Ila sasa huyu dereva naona alikuwa sijui amechelewa anapoenda ebwa akawa anabandika tu gia yaani haina kupangua kila tukichungulia nje ni kama ndege inataka kuruka chombo kimekolea kinoma noma, nikatoa ishara kama kiongozi kuwa ebu wote turelax tusiwe na pressure mchezo tutaucheza tena vizuri tu. Bhana bhana dereva yule utafukiri anajua kama tuliingia kwenye ile gari tukaona ss leo ngoja tuone mwisho wake kama ndiyo safari ya Bukoba au Congo itafahika mbele kwa mbele🤣🤣

Ukomandoo taratibu ukaanza kutuondoka mule ndani ikawa kama gari iliyobeba wafiwa watu macho yametuiva, hatujui wapi tunaenda na dereva kwa sifa yeye anapanga gia tu fyuuuuuuuu.... dadeki.

Nikiwa kama mtu aliyeshikwa ugoni nilitulia nikiwa nawaza vile home watakavyo anza kututafuta yaaani pale tena nikiri ukomandoo ukawa undezi sasa mafua yanatoka yenyewe na ila ukimywa ulizidi kutawala kila mtu akawa anawaza lake dadeki.

Kama nusu saa hivi gari ikasimama mara ya kwanza tukaangaliana hata hamu ya kuangalia nje haikuwepo ile tunataka kuchungulia nje dereva giaaaaa..... mara chwiiiiiii break za kufa mtu. Pale nikawapa ishara tulieni komando mbobezi nicheki mazingira , nikajiinua inua pale mpaka kwenye ka mpenyo flan hivi kudeku nje shaaaabashiiii shubamiti tupo kambini full ma true soldiers sasa pale nilirudi nikawa kama bubu hivi, washkaji wakiwa na hamu ya kujua tupo wapi nilirudi huku mwili ukiwa unasikia joto na baridi kwa pamoja yaani mwili na roho ni kama vilikuwa havina ushirikiano hivi.... jasho si jasho baridi si baridi... nikawaonyeshea wenzangu nao wacheck tu haina haja ya kuambiana kwanza nikaona nikama tuna vipaza sauti so kuongea ni kama tunatangaza uvamizi hivi ile wenzangu kucheck nje hivi nilisikia mmoja kati yetu akitoa ushuzi flan hivi ule wa pole pole ila wa sauti ya kwanza..... pyuuuuuuu.....pyuuuuuuuu. Nikajisemea eheee hii ni kali ya mwaka leo ndiyo leo.

Basi nikapata ujasiri nikakumbuka kwenye mapigano yale makali kama ya wavitinam anayeshindwa huwa ananyoosha mikono juu nikachoropoka bila kushauriana na mtu kushuka kwenye gari huku nimenyoosha mikono juu kama mateka flan hivi aseee wooote tukaaanza kuuoka kwa style ile ile wale ma soldier walishangaaa ila plus na yule dereva akashangaaa vibwengo hawa wa wapi tena? Ila kama dk mbili hivi masoldier walituchukua maelezo tukakiri mchezo wetu mchafu na walicheka sana. Uzuri walituelewa na kwa vile nilikuwa wa kwanza kushuka nikapewa jina na captain, dereva akapewa jukumu la kuturudisha pale tulipodandia tukamuelekeza nikakaa kabisa mbele kwa dereva nikamuongoza hadi pale pale tulipodandia ikawa pona pona yetu.......

Muwe na wakati mwema.
Utoto una raha na karaha zake jamani khaa!! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Duh nimecheka sana...hadi kuongea unaona kama mna vipaza sauti
 
Dah nimecheka sana mkuuu. Umenikumbusha mbali ww utakua umezaliwa enzi za miaka ya 80 na 90 mwanzoni achana na wa kizazi cha cartoon.
 
Unajua kitendo cha sisi kutoka kwenye lile gari tu na vile vi mwili vyetu vya utoto na mikono tumenyoosha kimateka macho yametuiva mafua yanatoka tu yenyewe yale mepesiiii ni kama tunalia ila kisailensa flan hivi tunashindana kuvuta mafua tu fyuuu fyuuuu yaani wale masoldier walishangaa sana na wakajua tayari tumeshajiadhibu manake wote macho mekunduuu na visura kama vimevimba na hatukuficha kitu tulieleza kila kitu, wakatukanya na kutusamehe na ikumbukwe tulikuwa kama sita hivi, hivyo tukisema tunaomba mutusamehe tunasema wote basi tunatia huruma kinoma vishingo pembeni nn 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 acha kabisa
Lazima kuna masoja wenzako humu JF hahah
 
Yani wabongo bana!,ukiandika story fupi watakwambia iongezee nyama.

Ukiandika story ndefu utasikia ndefu sana sijaisoma yote.

We subiri siku nikiandika uzi wa jinsi ya kumtoa mtu busha atakaye sema uzi mfupi naanza kumtolea mfano huyo huyo busha ngaaaa.... alafu tutafutane dm 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Dah nimecheka sana mkuuu. Umenikumbusha mbali ww utakua umezaliwa enzi za miaka ya 80 na 90 mwanzoni achana na wa kizazi cha cartoon.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣 sisi ma game tunayajulia ukubwani huku ila huko bush ni timbwili timbwili tu kizazi kama ulichosema tuna matukio kibwena asee
 
Back
Top Bottom