Tuliozaliwa zamani kuna haya. Je, ulishawahi kukutana nayo?

1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa kwa mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana kuvaa nguo ya ndani aina moja nchi nzima (VIP), usiombe ikakatika ukakuta imebana kifua.
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bruce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kulisugua chini
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe maridadi.
18. Ubitozi Ulikuwa ni Kusimamisha Kora Ya Shati.
19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".
20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakuambia "Utaipata Siku Ya Kufunga Shule".

Je wewe unakumbuka nini??

Nimeipenda hii...kumbuka bitoz lilitokana na wale wanamuziki maarufu wa Uingereza 'the Beatles.."

Nyingeza:

21. Kwenda shuleni boarding na sanduku la mbao
22. kuvaa mashati ya nylon na kuweka noti nyekundu ya sh. 100 maarufu kama 'masai' kwenye mfuko wa shati kuwakoga wenzako
23. kwa wale wa vijijini kuvaa viatu siku ya Jumapili tu...
24. Magari ya Omo kufika maeneo mbalimbali mjini kuonyesha sinema nyingi zikiwa za 'cow boys' za akina Bud Spencer, Lee Van Cleef, Clint Eastwood, John Wayne na wengineo
25. Kutembea na notebook kwenye mfuko wa nyuma wa kaptura ikiwa na maneno magumu ya kiingereza

26. vijana wa jinsia ya Ke kuwaandikia barua vijana wa Me zikiwa zimezungushwa na michoro ya maua na kuweka 'poda' (powder)
 
kuvaa suruali pekos au bugaluu. viatu vya ghorofa vya Bora shoes yani raison. suruali ya kubana ukitaka kuvua sharti ukae chini. mashati ya kubana sana slim fit halisi
 
Siku jirani akipika wali maharage unavizia wakati wanakula unajisogeza mlangoni kwake na kuanza kujikoholesha ili wakusikie uitwe
 
hizi mambo nimezshuhudia mwisho 2008, nipo kidato uninyolee mkasi? atafika afisa elimu
 
Hii sijawahi isikia labda ilikuwa ya kimila zaidi
hapana si ya kimila sema tulikuwa na iman na yale maji ya baraka kwamba ukiyamwaga barabarani lazima uokote pesa ni kama wanavyo amini wengine kwamba ukiwa unaumwa tumbo basi ukinywa yale maji tumbo lina tulia kwa wale wakristo wanaelewa hili (ila utoto kazi ati unamwaga maji ya baraka barabaran mfano siku ya jumanne unasubiria hadi jumanne ijayo ndipo uokote pesa )
 
1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa kwa mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana kuvaa nguo ya ndani aina moja nchi nzima (VIP), usiombe ikakatika ukakuta imebana kifua.
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bruce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kulisugua chini
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe maridadi.
18. Ubitozi Ulikuwa ni Kusimamisha Kora Ya Shati.
19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".
20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakuambia "Utaipata Siku Ya Kufunga Shule".

Je wewe unakumbuka nini??

Huingii kwa Jirani kuangalia movie hadi ukaoge, halafu vibanda umiza kipindi hicho vilikuwa ktk ofisi za ccm!
 
1.kulikuwa na kitu kinaitwa Malani/ utani, mfano mtu anamwambia mwenzie twende sura imejukunja Kama ngozi ya p****
2. Kuwachungulia waschana na waalim kwa kudondosha kioo chini.
3. Tobo gumi
4. Angaisha bwege
5. Kula tum bakishie baba
6. Kuruka beki
7.mashindano ya umitashumta
8. Kande na mseto baada ya kengele ya saa nne
9. Shilingi ishilini ilikuwa pesa kubwa, hapo utapata mseto,kande, makunazi na fulu
10. Mafuta ya rays
11. Soda ilikuwa vimto, fahari na mirinda orange shilingi 70
12.shilingi ishirini ilikuwa ya noti ya zambarau, na pia kulikuwa na shilingi ishirini na tano
13.soksi za pundamilia
14. Kuvaa moka siku ya sikukuu
15. Maonyesho ya kibisa/mazingaombwe
16. Mbiu ya mgambo
17. Hadithi za mazimwi
18. Chopeko na mnofu/ karudi baba mmoja toka Safari ya mbali/ sizitaki mbichi hizi
19. Ukipiga picha unanyooshea kidole kwenye redio ama tv, au unapiga kwenye Maua.
20. Sikinde/ mbaraka mwinsheh/ ottu Jazz, pamela nkutta, Oliver ngoma pepe kale ndio ngoma zilikuwa zikihiti
 
Mchezo kupinga kuputana chakula kama vile mihogo ya kuukaanga au barafu wenyewe tulikuwa tunaita ice cream ya ukwaju.
 
KARUDI BABA MMOJA, TOKA SAFARI YA MBALI,
KAVIMBA YOTE MAPAJA NA KUTETEMEKA MWILI,
WATOTO WAKE WAKAJA ILI KUMTAKA HALI,
WAKATAKA NA KAULI IWAFAE MAISHA.

AKATAMKA MGONJWA, NINAUMWA KWELI KWELI,
HATA KAMA NIKICHANJWA HAITOKI HOMA KALI,
MWILI NAONA.........., KIFO KINANIKABILI
.........

.......
.........
........

BABA ALIYEKUFANI, AKAJIBU LILE SWALI,
BABA YENU MASIKINI, NINAKUFA SINA MALI,
NENO MOJA LISHIKENI, KAMA MNATAKA MALI,
FANYENI KAZI SHAMBANI, MWISHO MTAPATA MALI.


SAMAHANI SIZIKUMBUKI ZOTE BETI ZA SHAIRI HILI. KAMA KUA MWENYE KUMBUKUMBU ATUWEKEE HAPA TUFURAHI

(NILIKUWA NAJISIKIA RAHA HATA YA KWENDA SHULE NA BETI ZOTE TULIKUWA TUNAIMBA KICHWAI KULIKO HATA WIMBO WA TAIFA. LAKINI WATOTO WETU SIKU HIZI WANAKOSA MENGI NDIO MAANA MTOTO ANAMALIZA LA SABA HAJUI KUSOMA NA KUANDIKA)
 
Back
Top Bottom