Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Wengi wamefilisika kwa kuendekeza starehe hasa kuwa malaya.
Pesa haiwezi kudumu mikononi mwa mtu mlevi na malaya.
Sisi Wakinga huu mtihani tunaumudu kwa asilimia kadhaa.
Yaah sahihii mkuu, Mkinga kwanza huwezi kumdhani, ukitaka kujua wa Kinga wana Mali nenda Iringa wapo akina Macity na akina mzee Mzalendooo, ni balaa
 
Nikiwa nimemaliza chuo sina hili wala lile, niko kitaa nikijipanga, nikachangiwa na ndugu zangu mtaji wa milion 4 point something huko, niende nikafanye biashara ya mchele toka Moro vijijini kuleta mijini na kusambaza kwa bei ya jumla.

Biashara mwanzo ilienda vizuri, mwisho wateja wangu wa siku zote wakawa wakopaji wangu wakubwa, malipo yakawa ya kuzungushana, nikawa mkali kidogo ila kwa bahati mbaya pesa ikawa ndogo kwenye mzunguko wangu, sinunui tena zile kilo nilizoanza nazo kwa wakati, mambo yakawa tofauti kidogo, nikaenda weee.

Mwisho wa siku nikachanganyiwa mchele kipuuzi kabisa na mtu ambae nilikua namuamini, nikajikuta nipo na mchele wa vitumbua na jamaa yule kakimbia, hapo ndio ukawa mwisho wangu, nilifilisika kama kuku, ndugu zangu hawakunielewa tena, nilipata stress kama tani 7 hivi.

Wakati tena nikapataga milion 3 kwa enzi zile haikua haba aisee, nikawa naishi vizuri tu, hizo elf 10 kwangu zilikua buku, sina cha kujibania kwa kweli, kuja kustuka nimenunua friji na tv tu vya geto tena ka friji kale kadogoo kabisaa, hela yotee imeisha katika njia zisizoeleweka, nilichanganyikiwa tena, sina nidhamu ya fedha.

Mwisho nikarudi zangu kusoma tena chuo ndio nikaja kutoboa kwa njia zingine kabisa kwa kutumia kazi niliyosomea.

Je, wewe unakumbuka vipi? Nini kilikupata?
Bila kuajiriwa, maisha yatakushinda
 
Back
Top Bottom