Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu, binafsi nimewahi kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.

Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.

Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya Sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, sikusita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.

Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.

Unaweza kushare mawili matatu kama umewahi kukumbwa na maswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.

Pia soma Fanya yafuatayo ukigundua kuna majambazi nje ya Nyumba yako
 
Daaah nlikutana na Kicheche hatar fayaaa mzee baba hadi kero
Nikachukua asali yake Weweee ni noooomaaaa Pumbavu kabsaa yule
Nlitimua mbio Nashukuru nyumba ilikua Karibu nikazama bila hodi vuupuu....
Watu kule ndan Uuuwiii Uuuuwwiiiii Uuuuwwiiiii Uuuuwwiiiii Uuuuwwiiiii Uuuuwwiiiii Uuuuwwiiiii Uuuuwwiiiii Uuuuwwiiiii Uuuuwwiiiii woooyoo woooyoo woo-hoo yaan full purukushani
Kicheche kusikia full kelele kikakimbia
Yaan nikikumbuka Siku ile nacheka sanaa
Vicheche ni noooomaaaa sanaaa
Jaman wanaume tuwe makini Hawa viumbe ni shida ukiwaendekeza utapata aibu kwa jamii
Tangu Siku ile nilikoma sitaki shobo na kiumbe chochote nawahi home mapema
Gambe nimeacha kabsa
Ilikua singida mzee baba


Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Miaka ya 2000 mwanzoni, likizo time mshua katufata boarding school tunarudi home. Tulichelewa kuvuka boarder ya Mutukula tunaitafuta Bukoba. Baaasi tukakutana na bonge la road block, wazee walee na SMG zao. Wakapunga mkono style ya Traffic police wa awamu ya tano. Sijui mshua alitoa wapi confidence, ali reverse shangingi faster na kwa speed almost 40km/h au zaidi for about 10 minutes, akageuza huyooo tukarudi boarder tukala.. ndo ikawa pona yetu..

2. Wazee baba walikua wanammendea mshua kitambo, wakijua pesa pale ipo. Sehemu ya kazi ya mshua ilikua ni porini, katika ranchi za taifa. Basi siku moja mshua kapokea mishahara ya wafanya kazi, kaenda nayo porini. Majambazi yakatonywa, yakajiandaa, jioni saa kumi na mbili yakatimba home na bunduki kubwa kubwa, sisi watoto hatujui A wala B. Mshua alikua katoka kaenda kupiga maji na washakji zake. Majambazi yakatukuta sisi na step mom, yakamwambia step mom awapekele mpaka safe ilipokua, akawapeleka, sema wakashindwa kuifungua. Wakatafuta funguo wakakwama. Mama nae hajui funguo ilipo. Wakampa kipigo cha mbwa koko lakini hakuwapa walichokitaka, kiukweli hakujua funguo ilipokuwa. Safe wakaifyatulia risasi lakini haikufunguka.. walivyoona muda unakwenda, wakabeba redio, TV na jewerly wakasepa. Dingi anarudi kalewa zake, anasema funguo zilikua kwenye suruali aliyokuwa kaivaa jana yake, suruali iko juu kwenye hook.

3. Mwaka 2016 saa nane usiku natoka zangu kula bata na wana wa TIA, nina kama mwezi nimenunua mark X, nafika TAZARA taa zinawaka red, hamna magari kabisa na malori ni yakuhesabu, ile nasubiria zimulike green, akatokea mtu out of nowhere anataka nishushe kioo, ana bonge la panga.. nikajaa wenge, pombe zikaniishia. Jamaa mwingine akatokea upande wa kushoto akaanza kugonga kioo kwa kitako cha bastola... mweeee, nikakanyaga mafuta gari inaondoka kwa speed matata. Bahati nzuri nilikua sijaweka P(parking). Kuna semi trailer lilikua linavuka kwenda airport nililikosa kosa kuligonga. Nikanyoosha mijamaa nikaiacha haiamini kama nimeiponyoka. Nilipofika Buguruni sikujali kama kuna watu na magari wanavuka 24hrs. Huyooo mpaka getto Tabata.. !
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom