Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Nduki kama Usain Bolt
Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu,,, binafsi nimewai kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.

Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.

Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi, saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, siku sita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.

Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.

unaweza kushare mawili matatu kama umewai kukumbwa na mswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kitu cha kufurahia maana kuna wengine ni vilema,wamefirisika na wengine kuuliwa.

Kuvamiwa iwe na majambazi au hata vibaka tu wakikuwahi Mungu pekee ndio msaada wa mwisho.

Binafsi nimewahi vamiwa usiku na majambazi nikiwa naishi Mwanza buzuruga.

Mwaka 2016 usiku wa kuamkia tarehe 21 mishale ya saa 04:30 alfajiri.

Siku hiyo nilikua na vipesa kama milioni 12 mchana hadi saa 00:00 usiku nikiwa nimebakiwa na milioni 8 baada ya kufanya manunuzi ya vitu nilivyokua nimepanga kununua,

Saa 01:00 usiku nilikua Cassino moja ipo mkabala na stand ya posta nikaamua niende nyumbani,nikiwa na tax nikafikiria Kwa nini niende na pesa zote zile nyumbani,bahati nzuri kazini kwangu palikua maeneo ya mjini kati mtaa wa uhuru nikamwambia tax nipite kazini mara moja.

Nilipofika kazini usiku ule nilitoa laki 2 na elfu 20 kwenye zile pesa zilizobaki nikaziacha kazini.

Saa 2:10 nikawa nimefika nyumbani,pale nyumbani nyumba nilikua naishi kulikua na mlinzi wa kampuni pia kulikua na uzio wa maana tu.

Muda mfupi alikuja mdogo wangu ambae alikua anafanya kazi kwenye kampuni flani ambayo walikua wanafunga kazi kati ya saa 1:00 na saa 2:00 usiku,nikamfungulia na nikafunga mimi mwenyewe milango tukalala.

Nikiwa nimetega alarm saa 04:30 alfajiri niamke kwenda zoezi,ilipotimia mida ya saa 10 kama kawaida nikaamka,nikafungua mlango wa chumbani nikamwacha mke na mtoto nikafika sebuleni.

Ile nataka fungua mlango wa kutoka nje ukaanza kuvuma upepo mkali sana na nikiwa pale ghafla ikaanza mvua kubwa kunyesha.

Kuona vile nikaamua kurudi chumbani lakini milango yote ikiwa imefungwa vyema kasoro mlango wa kuingia chumbani kwangu.

Mvua na upepo unaendelea nikaamua kujilaza,mara nikasikia sauti ya dirisha upande wa jiko ukiwa kama umebamizwa kwa sauti kubwa.

Nikamuuliza mwanamke kuna dirisha mlisahau kufunga? Akanijibu yawezekana nyumba kubwa na madirisha ni mengi!.

Lakini nikamwambia itakua upepo tu. Dakika 2 baadae ile sauti ya dirisha ikajirudia sasa hapo akili nimeshaiaminisha ni upepo sikujali! Mwamba nikavuta shuka juu ya mto mguu wa kuku upo.

Dakika 5 baadae mwanamke ananiambia baba flani TUMEVAMIWA! Nikamjibu

Tukawekwa mtu kati tochi kama 4 zimetumulika na amri ni usijaribu kufanya chochote!hapo ni saa 04:24 hivi asubuhi.

Nikaamrishwa kushuka chini huku nimewekea bunduki kubwa iliokatwa kitako usoni,mwanamke kawekewa panga kichwani..mwingne anasema tukileta choko choko atampasua mtoto!

Nikashushwa chini nikalazwa chini uso chini mgongo juu!nikiwa na hofu kuu.

Cha kwanza walikusanya simu zote zilizokuwepo,cha pili wakaomba pesa nami nikawauliza mmekuja kwa ramani au mnabahatisha kama kuna pesa wakasema,tuna uhakika umekuja hapa na pesa zaidi ya m5.

Nikawaambia nilikuwa nazo lakini dakika ya mwisho nimezipitisha kazini na hapa pesa iliopo ni laki 2 tu nikawaonesha wakabeba.

Wakasema hamisha pesa iliopo Mpesa! Ikabidi niwape namba yangu ya siri halali wakaangalia salio wakahamisha 1.6m

Walivyomaliza wakaniamrisha hamisha pesa toka bank kuja kwenye simu,nikawambia Sina huduma hiyo na hata ingekuwepo kwenye mvua haiwezekani kufanya mwamala.

Wakabeba ATM card zote zilizokuwepo.

Wakati huo bonge la mvua linashuka Japo upepo umekata saa 05:00 alfajiri.

Wasenge wakabadili viatu walivyokuja navyo wakavaa safety boots nilikua na pairs nyingi.

Wakati huo nikagundua nje kuna mtiti wa hao jamaa na ndani walikuwemo kama 5 hivi

Mmoja akataka kumbaka mke wangu wakati anataka kuvua nguo,mkuu wake wa msafara akaingia akamwambia nishakuzuia tabia hiyo na hapo ndio ukawa pona ya wife kuliwa mbele yangu.

Mwisho waliinua kitanda wakaniweka uvunguni

Baadae wengine wakaenda kusearch vyumba vingine kulikuwa na beki 3 wakamleta chumbani hapo wameniweka uvunguni na wamenigadi na chuma kama 2

Chumba cha mwisho yupo mdogo wangu kulingna na kulala usiku mwingi alikuwa amesinzia wakamkurupusha akapiga kelele tumevamiwa akala bapa ya mgongoni akaambiwa akae kimya! Naye akaletwa chumbani kwangu

Wakawekwa chooni wakafungiwa huko na beki 3 huko nje wanapiga risasi hovyo, zinaaunguruma balaa.

Wakaomba funguo za mlango wa nje nikawaelekeza,wapuuzi wakasema ukipiga kelele muda huu huna bahati,subiri dakika 10 ndio uombe msaada.

Dakika 3 baadae baada ya kuondoka nikamwambia wife awafungulie waliopo chooni waje wasaidiane kuinua kitanda ili nitoke uvunguni wakafanya hivyo.

Muda wote huo hata hofu ilishaisha.

Nikatoka kumcheki kukuta mlinzi kapigwa kudu mikono na miguu pia mdomo kapigwa plasta!

Nikamfungulia mguu kumbe alikatwa panga.

Nikasubiri saa 06:00 ndio nikaenda polisi.

Katika tukio lile sikupigwa hata kofi zaidi ya mlinzi kujeruhiwa.

Baada ya Upelelezi kama wiki 2 kwa msaada wa pesa ya mpesa na card maana walijaribu kwenda bank kutoa pesa mnyororo wote ulidakwa.

La haulaa wale ni vijana mchana ukiwaona ni wasaniii walikua waimbaji na wana studio mtaa wa mecco mwanza huwezi wafikiria kama ni wezi.

Walipigwa mpaka nikawaombea msamaha Japo 2 kati yao waliuwa kwenye kipigo kile.

Kwa uzoefu ule kuvamiwa wezi wakikuwahi unatakiwa kua mpole zaidi ya hapo utaumia tu!

Huu ndio mkasa wangu kwa kesi za wezi.

Mwenzangu tusimulie je ushawahi kutana na kazi a kama hii je ilikuaje?

====
Kanuni ya kwanza ukiwamiwa na majambazi na ukaona wamekuwahi basi unatakiwa kua mpole na kuwapa ushirikiano wote wanaouhitaji.

Majambazi hua na siraha ila huitumia tu pale wakiona usalama wao uko hatarini, zaidi zile ziraha hua ni kwa ajili ya kukutishia ili uogope, sasa ukileta mgomo hapo ndio hulazimika kutumia siraha.

Siku zote usibishane na jambazi, mpe ushirikiano wote unaohitajika, fuata maelekezo wanayokupatia.

Pia siku zote usidharau mlio/kelele yoyote isiyo ya kawaida wakati wa usiku unaousikia jirani au nyumbani kwako, hakikisha unaamka kuangalia ni kitu gani. Juzu mwezi wa 11 mwaka jana, nikiwa macho, taa inawaka chumbani kwangu na tena dirisha moja nimefungua pazia hivyo ukiwa nje unaniona, nikiwa nachat jamii forum sa 7 usiku nikasikia mlio wa kama dirisha la jikoni kwangu linavunjwa, nikapuuza nikasema itakua labda jirani yangu karudi, nikapuuzia, kumbe vibaka wanavunja dirisha waeeze kufungua mlango wa jikoni wazame ndani.

Baada ya kushindwa wakavunja grill ya jirani yangu, wakavunja mlango, wakaingia wanachukua laptop, flat ya samsung nchi 55 nshikaji alikua kainunua hata wiki haijaisha, wakachukua hela, wakaondoka, kumbe walikuja na gari hapo nje geti kubwa.

Bahati mbaya kwao ni kua niliamka kwenda kukojoa nizime taa nilale ila kabla sijapanda kulala nikaenda jikoni kuangalia, nakuta dirisha limevunjwa, mlango umelegea kama vile ulikua unachezewa, kufungua nakuta grill hangu imeng'olewa, kuangalia kwa jirani mlango uko wazi, grill imevunjwa, hapo ndio nikastuka, jirani amelala fofofo, nikamamuasha hakuamka, nikaachana nar kwanza, kisha kwangu nilikua na mshikaji kalala roon nyingine nikamuamsha, kutoka nje gari ikakimbia wakaacha mazaga yote waliokua wamekusanya nyumba za jirani zote. Hiyo ndio ikawa pona ya vitu vya mshikaji na majirani.

Vibaka wengi wa siku hizi ni washkaji tu, hawa vijana waliopenda kazi ila wanapenda kunywa na kula vizuri, kumiliki mademu wazuri nk. Mimi nikikamata kibaka/mwizi hawa masharobaro sitamuua wala kumpigia kelele, namuingiza room nampiga mashine ya kueleweka huku namchukua video kisha namuacha.
 
Mkuu hiyo mitaa ya buzuruga, memo, had I national vijana wezi sana. Mimi mwaka Jana mitaa niliyokuwa naishi national nyuma ya comfort hotel walinipulizia dawa wakaiba flat screen,jiko, nguo na via zangu kwenye nlishtuka SAA 3 asubuhi. Hata job nilishindwa kwenda sumu Kali sana ile.
 
Daaah aisee
Mkuu hiyo mitaa ya buzuruga, memo, had I national vijana wezi sana. Mimi mwaka Jana mitaa niliyokuwa naishi national nyuma ya comfort hotel walinipulizia dawa wakaiba flat screen,jiko, nguo na via zangu kwenye nlishtuka SAA 3 asubuhi. Hata job nilishindwa kwenda sumu Kali sana ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanuni ya kwanza ukivamiwa na majambazi na ukaona wamekuwahi basi unatakiwa kua mpole na kuwapa ushirikiano wote wanaouhitaji.

Majambazi hua na siraha ila huitumia tu pale wakiona usalama wao uko hatarini, zaidi zile siraha hua ni kwa ajili ya kukutishia ili uogope, sasa ukileta mgomo hapo ndio hulazimika kutumia siraha.

Siku zote usibishane na jambazi, mpe ushirikiano wote unaohitajika, fuata maelekezo wanayokupatia.

Pia siku zote usidharau mlio/kelele yoyote isiyo ya kawaida wakati wa usiku unaousikia jirani au nyumbani kwako, hakikisha unaamka kuangalia ni kitu gani. Juzi mwezi wa 11 mwaka jana, nikiwa macho, taa inawaka chumbani kwangu na tena dirisha moja nimefungua pazia hivyo ukiwa nje unaniona, nikiwa nachat jamii forum sa 7 usiku nikasikia mlio wa kama dirisha la jikoni kwangu linavunjwa, nikapuuza nikasema itakua labda jirani yangu karudi, nikapuuzia, kumbe vibaka wanavunja dirisha waweze kufungua mlango wa jikoni wazame ndani.

Baada ya kushindwa wakavunja grill ya jirani yangu, wakavunja mlango, wakaingia wanachukua laptop, flat ya samsung nchi 55 mshikaji alikua kainunua hata wiki haijaisha, wakachukua hela, wakaondoka, kumbe walikuja na gari hapo nje geti kubwa.

Bahati mbaya kwao ni kua niliamka kwenda kukojoa nizime taa nilale ila kabla sijapanda kulala nikaenda jikoni kuangalia, nakuta dirisha limevunjwa, mlango umelegea kama vile ulikua unachezewa, kufungua nakuta grill yangu imeng'olewa, kuangalia kwa jirani mlango uko wazi, grill imevunjwa, hapo ndio nikastuka, jirani amelala fofofo, nikamuasha hakuamka, nikaachana nae kwanza, kisha kwangu nilikua na mshikaji kalala roon nyingine nikamuamsha, kutoka nje gari ikakimbia wakaacha mazaga yote waliokua wamekusanya nyumba za jirani zote. Hiyo ndio ikawa pona ya vitu vya mshikaji na majirani.

Vibaka wengi wa siku hizi ni washkaji tu, hawa vijana wasiopenda kazi ila wanapenda kunywa na kula vizuri, kumiliki mademu wazuri nk. Mimi nikikamata kibaka/mwizi hawa masharobaro sitamuua wala kumpigia kelele, namuingiza room nampiga mashine ya kueleweka huku namchukua video kisha namuacha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom