Tuliowahi kukopesha watu pesa na tukazimwa tukutane hapa

hahhahahhahhaha mkuu nakuona hapo kwenye avatar ndio unalia hadi leo... pole sana kwa matatizo yako
 
Me niliwahi kopa penzi na sikumlipa sio ufahari ni ujinga ila aliyataka mwenyewe nilivokuta mchafu
 
Nipe mbinu mkuu,
Kesho kuna mtu kaniahidi pesa yangu ni mwaka sasa ananizungusha tu.... Ili kesho nikienda nipate mbinu mpya maana uwaga nikienda na hasira sound zinakuwa nyingi napita hivi, sasa sitaki kumuacha sasa... Ulifanyaje?
 
Nipe mbinu mkuu,
Kesho kuna mtu kaniahidi pesa yangu ni mwaka sasa ananizungusha tu.... Ili kesho nikienda nipate mbinu mpya maana uwaga nikienda na hasira sound zinakuwa nyingi napita hivi, sasa sitaki kumuacha sasa... Ulifanyaje?
Nishasema nilichofanya chief, cheki post #59 juu kidogo utaona.
 

Hii safi sana,
 
Jamaa kaja. Kuna dili twende tukapge faida tukipata na uhakika tungawana 50/50.
Dili kwisha anajidai anaharaka. Sikumpgia simu wala nini.

Baada ya wiki 5 mbele, alikuwa anadalalia uuzaji wa gari. Mnunuzi muhaya anataka kulipa kwa benk na yeye account namba yake kasahau, mie nkamwambia si ufanye kesho? Mnunuzi muhaya akasema yani wote wawili hamna account, nkamjibu andika yangu.
Wakati anasema jina nani na kiasi nkajifanya nafungua wallet huku nasoma kwa uhakika, nakutiksa kichwa.
Kesho yake nkachukua 100% ya hela yangu na gharama ya kutunza hela kuanzia usiku sa 5 mpaka asubuhi sa 5.
 
Kuna jamaa nimemkopesha laki 3 toka 2015, hadi leo hajanipa na tukionana anajifanya kama nothing happened. Yaani marafiki ni shida ukiwanyima wanalalamika dunia nzima kuwa wewe ni mbaya. Ukimkopesha umetoa sadaka
 
Mimi nilimkopesha jamaa yangu
Akawa halipi Nasi nilimuendea kwa kasi kwake
Kila mara kila siku ikiwa ni kero Sana kwake
Siku moja akaniambia nikulipe kwa njia nyingine
Sikujua njia gnyingine nilikubali kusikia hiyo njia
Tulitoka nje ya Nyumbani kwake ili aaaniambie
Duuh jamaa aniambia nimle mkewe tumalizane Deni
Niliamua kusamehe tu hela Hana na njia aliyotumia sikuikubali
Nimesamehe
 
mkewe analipa???
 
Hii ni hadithi ama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…