Tuliowahi kukaa mahabusu/jela tukutane hapa!

Tuliowahi kukaa mahabusu/jela tukutane hapa!

Nikola24

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2024
Posts
598
Reaction score
1,236
Mimi binafsi nimewahi kuwekwa mahabusu mara 6 kwa vipindi tofauti.Sababu ni ugomvi ugomvi.

Nimeanzisha huu Uzi tu share stori za mikasa na uzoefu uliopata ukiwa lock up.

Mimi naanza:
Nikiwa mahabusu woga mkubwa ni wafungwa wenzangu.Unakuta watu kibao humo, wapo walioua,kubaka,wezi, na hata majambazi. Wahalifu Wote mnakaa chumba kimoja.Hii structure inatisha sana.

Kuna wengine wakiwa mahabusu hawana stress kabisa,utakuta kachangamka kama yuko kitaani.Kwangu hata kula nilikuwa najilazimisha ,nakuwa nawaza sana aisee.

Ukiwa mnyonge unaweza kuonewa hata kubakika na cell mate wenzako.

Kikubwa nashukuru nilitolewa ndani ya siku chache nikarudi home dah.

Nanyi wekeni uzoefu wenu tujifunze....
 
Mahabusu ya Polisi au Magereza?

Mahabusu zote mchana hazina shida, shida inaanza usiku pale MBU wakianza kazi zao na joto kali
Hahah nimewasahau mbu! Kuna mbu balaa tena nahisi wana sumu maana wakikung'ata inauma balaa.

Uliwahi kwenda huko mahabusu?
 
Nilikaa jela wiki mbili ila niliishi kama mfalme baada ya siku ya kwanza kampani yangu ilivyofika kunitembelea..

Mazagazaga kibao mpaka mengine polis walizuia yasiingie, baada ya hapo mpaka manyampala wakawa machawa wangu.
 
Nakumbuka kuna jamaa alielezea jinsi alivyotoroka jela,Kumbe wale Askari wanamfuatilia,kasubiri usiku WA manane ndo Aingie kwa mama yake Ile anaruka ukuta Tu wanae 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 alinichekesha Sana!
Sahihi Mkuu!
 
Mimi binafsi nimewahi kuwekwa mahabusu mara 6 kwa vipindi tofauti.Sababu ni ugomvi ugomvi.

Nimeanzisha huu Uzi tu share stori za mikasa na uzoefu uliopata ukiwa lock up.

Mimi naanza:
Nikiwa mahabusu woga mkubwa ni wafungwa wenzangu.Unakuta watu kibao humo, wapo walioua,kubaka,wezi, na hata majambazi. Wahalifu Wote mnakaa chumba kimoja.Hii structure inatisha sana.

Kuna wengine wakiwa mahabusu hawana stress kabisa,utakuta kachangamka kama yuko kitaani.Kwangu hata kula nilikuwa najilazimisha ,nakuwa nawaza sana aisee.

Ukiwa mnyonge unaweza kuonewa hata kubakika na cell mate wenzako.

Kikubwa nashukuru nilitolewa ndani ya siku chache nikarudi home dah.

Nanyi wekeni uzoefu wenu tujifunze....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom