kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 733
Jamani wale wote ambao tumewahi kuchunga wakati tukiwa wadogo kabla hatuja anza shule na hata baada ya kuanza shule yaani ukirudi shule unachunga na zile siku za wikiendi basi wewe ni kwenda porini/malishoni kuchunga mifugo kama vile ng'ombe, mbuzi na kondoo tukutane hapa kuelezea uzoefu wetu pamoja vituko, mikasa na masahibu ya huko porini/malishoni ulipokuwa unachunga.
Mimi nilikuwa nikipenda sana kutokana na zile raha za kupata kila aina za matunda huko maporini pia kulikuwa na kuwinda wanyama wadogowadogo kama vile digidigi, pimbi, sungura pamoja na kanga na kware yaani ilikuwa wewe mchungaji unaporudi unapokelewa kwa heshima Kubwa ukirudi hasa ukiwa na mnyama uliyewinda huko machungoni, yaani ilikuwa kijana anayechunga anajaliwa na kuheshimiwa nyumbani mda wote kabla ya kutoka na baada ya kurudi machungoni anapewa chakula kizuri cha kushiba bila kusahau maziwa ya kutosha hata kama chakula ni kidogo basi atakula mchungaji kwanza wengine mtasubiri baadae wasiowachungaji walitamani kuwa wachungaji kutokana na mchungaji anavyojaliwa pale nyumbani kwetu.
Kingine nilichokuwa nakipenda ni kutembea na jeshi la mbwa wakali waliofundishwa kuwinda huku kila mbwa akiwa kapewa jina lakie kama vile chui, simba, nyati, mbogo, mwitu, jeshi, polisi, n.k
Hawa mbwa kwanza wakati wa kwenda machungoni ilikuwa ni mwiko kuwapa chakula(asiwe mvivu kuwinda) yaani mbwa akiwa na njaa akifika porini dakika kumi nyingi digidigi kadakwa hapo utasikia mbwa akitoa mlio wa sauti kuashiria mimi niende kuna jambo limetokea kwani wakikamata mnyama yeyote hawamli hadi mimi niende nikamchukue kama ni kumalizia kumchinja nifanye mimi na hapo mbwa watafurahi sana kwani kichwa ,miguu,matumbo ya ndani ndio mlo wao yaani nilikuwa nawapikia supu moja matata mno, baada ya kuja huku dsm nimeshangaa kuona supu lile ndio linaitwa kongoro.
Aisee ninayo mengi, hebu share na wewe yako.