Tuliowahi kufumaniwa bafuni/chooni tukutane hapa

Bulaya001

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
5,868
6,480
Natumai ni wazima kama nilivyo.

Moja kwa moja pasipo kupepesa macho najitosa kwenye mada yangu.

Wakuru hakuna kitu kinatia haibu/fedheha kama kufumaniwa ukiwa unashusha mzigo au upo bafuni unaoga tena ukute aliekufumania ni mtu mnaeheshimiana naye mno hasa hasa baba/mama mkwe, baba/mama mzazi wadogo zako wa kukufuata/wakubwa zako. Au uwe mgeni sehemu alafu ufumaniwe na mwenyeji kwakweli huwa inatia ukakasi sana. Unaweza ukatamani dakika zirudi nyuma ili tendo lisitokee ila inakuwa ishatokea hivyo.

Naomba tupeane uzoefu kuwa baada ya haya mafumanizi/matukio tata hasa lile la toilet (ambalo ndiyo baya zaidi) huwa unaangaliana vipi na aliye kufumania.

Mimi kwa upande wangu nimewahi kutamani kuhama home baada ya bi mkubwa kunifuma live toilet na mzigo ukiwa chini yangu, kwa kuwa nilikuwa -18 haikuwa kesi sana ila hivi leo nikikumbuka huwa natamani nimsahaurishe mama kwa kile kilicho tokea.

Tuna siku nyingi hatucheki, embu weka story yako ili tucheke kwa pamoja.

#karibuni
 
Back
Top Bottom