Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,465
Waraka huu ni kwa wana Tambaza wote-wale tuliosoma hapo zamani, na hawa wanaoendelea kutia aibu. Shule ya Sekondari Tambaza iliheshika sana kwa kuwa na VIPANGA wa ukweli. Imetoa watu maarufu sana ambao wameshika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Tambaza ilikuwa ya watu ambao akili zao zilikata kama wembe! Hawakukubali kuchokozwa. Kwa sababu ya sayansi, walifikia hatua ya kutengeneza hata mabomu. Muziki wao unajulikana sana kwa shule zote za Dar es Salaam za wakati huo.
Baada ya mwaka 1992 shule hii ikawa ya kidato cha nne na tano tu. Wakaanza kuvaa suruali. Walimu wakapelekwa wengine kabisa. Wanafunzi wakaanza kula chips. Wakapuuza kwenda kupiga dua kwenye kaburi la Mzee Tambaza! Hapo ukawa mwisho wa umaarufu wake, na sasa tumeona matokeo yake. Aibu tupu.
Nawaomba jamaa zangu kina Michael, Chuwa, Mjuba, Bob Rich, Mashaka Mgeta, Bob Chura, kundi zima la R4P MOB (Rujumu for Power), Kyaro na wagumu wengine wote tujitokeze kuhoji uhalali wa matokeo haya! Ni aibu.