Tuliopitia maisha magumu tukutane hapa!!

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
16,447
Reaction score
38,155
Nimeona nyuzi nyingi zikianzishwa za watu kuonesha kukata tamaa juu ya maisha wanayopitia, wengine wamefikia hatua ya kutamani hata kujiua!!

Kupitia Uzi huu tunaweza kutoa experience ya yale tuliyoptia na mpaka tulipofika ili hawa wenzetu wasifikiri ni wao!!

Kwa upande wangu nimezaliwa katika familia yenye uwezo Wa kawaida miongo karibia mitatu iliyopita, baba akiwa mwajiriwa serikalini na mama akiwa mama Wa nyumbani tu! Mama alifariki nikiwa std 2, na baba alifariki nikiwa std 4! Kuanzia hapo maisha yalivurugika kwa kiasi kikubwa maana mzee hakuacha mradi wowote ambao ungetusaidia zaidi ya nyumba ya kuishi!!

Nimeanza kuishi mwenyewe nyumbani toka std 4 mwishoni, nimepitia magumu ambayo hata hayasimuliki.. Kukosa na kushindwa kula ilikuwa kawaida na kutwa ilikuwa kuvizia nyumba za ndugu ikifika saa mbili usiku (hii ni experience ambayo sitaki hata kuikumbuka), hawa ndugu ilifika kipindi walinichoka na majungu ya chini chini nikawa nayasikia ila ningefanya nini? Ndugu waliosaidiwa mpaka kupata kazi na mzee wangu katu sikuwaona katika lolote!

Kikubwa juhudi katika shule sikuitupa, std 7 nilifaulu shule ya serikali, huko nako hata ada ambayo nilikuwa 70000 kwa mwaka nilikuwa tatizo achilia mbali mahitaji mengine kama nguo, sabuni, vitafunwa hata madaftari na pen! Hali ilikuwa tete sana, Ila mungu ni mwema nilifanya vizuri Olevel na nilienda A level na hatimaye chuo kikuu!!

Baada ya Kumaliza chuo huku nikiwa na matarajio makubwa juu ya maisha, ndipo nilipokuja kugundua maisha siyo vile tunavyotaka yawe! Kupata kazi kilikuwa kimbembe kingine! Nilizungusha sana CVs bila mafanikio yeyote, zaidi ya mwaka nilikaa kwa ndugu bila kazi yeyote mpaka nilipoamua kuomba kazi ambayo haikuwa professional yangu! Nashukuru hiyo kazi ndiyo iliyonipa mtaji na mpaka sasa Nina lines of businesses na Nina ambitions za kufika mbali katika biashara zangu!!
Hivyo basi ugumu wowote tunaopitia una mwisho ikiwa utakuwa na nidhamu ya unachofanya, kuwa na subira pia kuheshimu wengine!!

NB: Maisha niliyopitia yamenifanya nisiwe Mtu wa kujali sana, mpaka sasa sijaoa wala sina mahusiano yeyote strong... Nikiwa mwenyewe huwa naona maisha ni bora zaidi kuliko nikiwa katika mahusiano!
Kingine ambacho huwa kinanitia hasira ni pale ninapoona watu waliokuwa kwenye position ya kuweza kunisaidia kwa lolote na hawakufanya hivyo wanapoanza kujileta leta.. Huwa naharibiwa siku kabisa!
 
Poleni mliopitia maisha magumu.

Wengine hiyo hali hatuijui kabisa na si kosa letu kwamba hatuijui.
 
Pole sana mkuu, ni mda muafaka sasa na wewe kuwa msaada kwa vijana wenzako wanaopitia katika maisha magumu uliyopitia ww natumai kwa kufanya hivyo utapata dhawabu kubwa kwa Mungu
 
Maisha magumu ndio nini wakuu?
Unajitoa ufahamu sio? hakuna formula hayo maelezo aliyoyatoa mtoa mada ni mfano tosha ya maisha magumu aliyowahi kuyapitia na kila mtu amepitia yake.
 
duuh kweli ukidhan umepitia au unapitia maisha magumu kuna wengine they have gone through worse
 
Nimeona nyuzi nyingi zikianzishwa za watu kuonesha kukata tamaa juu ya maisha wanayopitia, wengine wamefikia hatua ya kutamani hata kujiua!!

Kupitia Uzi huu tunaweza kutoa experience ya yale tuliyoptia na mpaka tulipofika ili hawa wenzetu wasifikiri ni wao!!

Kwa upande wangu nimezaliwa katika familia yenye uwezo Wa kawaida miongo karibia mitatu iliyopita, baba akiwa mwajiriwa serikalini na mama akiwa mama Wa nyumbani tu! Mama alifariki nikiwa std 2, na baba alifariki nikiwa std 4! Kuanzia hapo maisha yalivurugika kwa kiasi kikubwa maana mzee hakuacha mradi wowote ambao ungetusaidia zaidi ya nyumba ya kuishi!!

Nimeanza kuishi mwenyewe nyumbani toka std 4 mwishoni, nimepitia magumu ambayo hata hayasimuliki.. Kukosa na kushindwa kula ilikuwa kawaida na kutwa ilikuwa kuvizia nyumba za ndugu ikifika saa mbili usiku (hii ni experience ambayo sitaki hata kuikumbuka), hawa ndugu ilifika kipindi walinichoka na majungu ya chini chini nikawa nayasikia ila ningefanya nini? Ndugu waliosaidiwa mpaka kupata kazi na mzee wangu katu sikuwaona katika lolote!

Kikubwa juhudi katika shule sikuitupa, std 7 nilifaulu shule ya serikali, huko nako hata ada ambayo nilikuwa 70000 kwa mwaka nilikuwa tatizo achilia mbali mahitaji mengine kama nguo, sabuni, vitafunwa hata madaftari na pen! Hali ilikuwa tete sana, Ila mungu ni mwema nilifanya vizuri Olevel na nilienda A level na hatimaye chuo kikuu!!

Baada ya Kumaliza chuo huku nikiwa na matarajio makubwa juu ya maisha, ndipo nilipokuja kugundua maisha siyo vile tunavyotaka yawe! Kupata kazi kilikuwa kimbembe kingine! Nilizungusha sana CVs bila mafanikio yeyote, zaidi ya mwaka nilikaa kwa ndugu bila kazi yeyote mpaka nilipoamua kuomba kazi ambayo haikuwa professional yangu! Nashukuru hiyo kazi ndiyo iliyonipa mtaji na mpaka sasa Nina lines of businesses na Nina ambitions za kufika mbali katika biashara zangu!!
Hivyo basi ugumu wowote tunaopitia una mwisho ikiwa utakuwa na nidhamu ya unachofanya, kuwa na subira pia kuheshimu wengine!!

NB: Maisha niliyopitia yamenifanya nisiwe Mtu wa kujali sana, mpaka sasa sijaoa wala sina mahusiano yeyote strong... Nikiwa mwenyewe huwa naona maisha ni bora zaidi kuliko nikiwa katika mahusiano!
Kingine ambacho huwa kinanitia hasira ni pale ninapoona watu waliokuwa kwenye position ya kuweza kunisaidia kwa lolote na hawakufanya hivyo wanapoanza kujileta leta.. Huwa naharibiwa siku kabisa!
Dah mkuu kwanza pole ya hayo uliyoyapitia lakini hongera pia kwa kurudi kwenye mstari maana maisha haya yakikukuta unaweza toka kabisa kwenye mstari.

Binadamu tuna hulka ya kujisahau sana kwa kweli, hao waliokuwa na nafasi ya kukusaidia na hawakukusaidia sometimes kiburi cha maisha kiliwafanya wajisahau sana.

Nilichojifunza kwenye haya maisha ni kuwa simple tu na kumsaidia kila mtu mwenye shida kama una nafasi hio hata kama alikuzingua sana huko nyuma.

Kuwa binadamu ni kazi sana aisee, usiombe kupitia maisha magumu halafu ukanyanyasika halafu mwisho wa siku ukabahatika wale wale waliokuzingua wakaanza tena ujipitisha pitisha, inauma sana aiseee, na hapa ndipo ubinadamu ulipo na kazi.

Ubinadamu ni kazi aisee.
 
Nilipitia ugumu kiasi fulani ingawa sio wa kutisha sana. Hii ni baada ya baba yangu kupunguzwa kazi kipindi kile cha mambo ya ubinafsaji wa mashirika ya uma. Kipindi kile ndio nilihitimu darasa la saba halafu matokep hayakuniruhusu kwenda shule za serikali.Baba yangu akajipinda kunipeleka shule binafsi ingawa ada haikuwa kubwa sana ila uchumi uliyumba sana ikafika kipindi hata nauli ya kwenda shuleni inakuwa shida.
Wakati mwengine rafiki zangu walikuwa wananipiga tafu nauli kwa sababu ilinihitaji shilingi 100 tu kwenda na kurudi shule kwa wakati ule. Lakini nayo ilikuwa ngumu kupatikana nikaenda kiubishi mpaka nikamaliza kidato cha nne . Matokeo yalipowadia niliishia kufeli vibaya sana nikahisi nimeshapoteza dira ya maisha yangu ya baadae. Nikajiingiza kwenye tabia nyingi sana hatarishi hasa udokozi na kufanya kazi ngumu kama kubeba matofari nk. Nikawa navuta bangi na ulevi wa pombe haramu ya gongo ndio ilikuwa starehe yangu( Ndio maana nilipo msikia Chidi Benzi alipo sema alijiingiza kwenye madawa baada ya kuelemewa na msongo wa mawazo wala sikushangaa sana).
Lakini Allah alikuwa bado ananihitaji , Katika kazi zangu za wizi udokozi siku hiyo nikabahatisha nikapiga mzigo wa nondo na washirika wenzangu tukagawana nikapata laki tano.
Nilivyopata ile pesa nikasema kwa nini niishi maisha hatarishi hivi wakati fursa zipo ikanibidi niende kusoma kozi ya mambo ya Clearing and forwarding and shipping management.
Kuna watu niliwafuata kipindi kile kuwaomba msaada ili niweze kusomea taaluma yoyote niweze kujikomboa lakini wote walinitolea nje na niliona kabisa uwezo huo walikuwa nao kwa kipindi kile.
Ila sasa hivi ninashukuru Allah nina maisha yangu na familia pia nikikumbuka nilipotoka huwa nahisi simanzi sana .
Niliamua kuacha vitu vyote vya haramu ,pombe ,bangi nk.
 
Nakumbuka tokea mzee amefriki miaka ya 2004 nikabaki na mama na ndugu wengne nilipata shida sana maana nilikuwa Ndo npo kidato cha kwanza na jukumu la kunisomesha lilibaki kwa kaka na dada wa damu ila walikuwa ni wabahili sana ingawa walikuwa na nafasi nzuri serikalini na binafsi kulipa ada ya 70000 ilkuwa ni ngumu ila hali hiyo ilinifanya nisome kwa bidii nikamaliza o level na deni la ada hvyo hvyo nikaenda advansi nako ikawa shida kwenye ada na mtumizi mengne ya bodi school ilikuwa shida saa nne wanafunzi wote wanaenda kupata chai na vtafunwa mi najifanya mgumu napenda kusoma nabaki class natia msuli tu nikatoboa chuo nikapata mkopo wa bodi nikaendeleza ugumu niliopitia advansi sikuwa na demu wala sikuangaika kununia laptop nguo nzuri zaidi ya mitumba yangu hii yote ni katka kujibana ili kupata mtaji wa kujiendeleza maana nilishaona sina wa kumkimbilia zaidi ya kujipigania mwenyewe mpaka sasa si haba nimesimama ila hali ya maisha niliyopitia imenifanya nimeshindwa kushindwa kuwa na mahusiano mazuri na ndugu na marafiki kwani naona si watu wanaoweza kunisaidia niwapo kwenye changamoto hata mahusiano yanayoeleweka kuyajenga kwa sasa imekuwa tabu kwani maumivu ya zamani bado yapo kwenye akili yangu ila naamuomba mungu anipe roho ya kusamehe n Kusahau naamini ikifika wakati nitasamehe na kusahau
 
Eeh Mungu Kama ni kwa Mapenzi yako, basi naomba kikombe hiki kiniepuke
 
Nimeona nyuzi nyingi zikianzishwa za watu kuonesha kukata tamaa juu ya maisha wanayopitia, wengine wamefikia hatua ya kutamani hata kujiua!!

Kupitia Uzi huu tunaweza kutoa experience ya yale tuliyoptia na mpaka tulipofika ili hawa wenzetu wasifikiri ni wao!!

Kwa upande wangu nimezaliwa katika familia yenye uwezo Wa kawaida miongo karibia mitatu iliyopita, baba akiwa mwajiriwa serikalini na mama akiwa mama Wa nyumbani tu! Mama alifariki nikiwa std 2, na baba alifariki nikiwa std 4! Kuanzia hapo maisha yalivurugika kwa kiasi kikubwa maana mzee hakuacha mradi wowote ambao ungetusaidia zaidi ya nyumba ya kuishi!!

Nimeanza kuishi mwenyewe nyumbani toka std 4 mwishoni, nimepitia magumu ambayo hata hayasimuliki.. Kukosa na kushindwa kula ilikuwa kawaida na kutwa ilikuwa kuvizia nyumba za ndugu ikifika saa mbili usiku (hii ni experience ambayo sitaki hata kuikumbuka), hawa ndugu ilifika kipindi walinichoka na majungu ya chini chini nikawa nayasikia ila ningefanya nini? Ndugu waliosaidiwa mpaka kupata kazi na mzee wangu katu sikuwaona katika lolote!

Kikubwa juhudi katika shule sikuitupa, std 7 nilifaulu shule ya serikali, huko nako hata ada ambayo nilikuwa 70000 kwa mwaka nilikuwa tatizo achilia mbali mahitaji mengine kama nguo, sabuni, vitafunwa hata madaftari na pen! Hali ilikuwa tete sana, Ila mungu ni mwema nilifanya vizuri Olevel na nilienda A level na hatimaye chuo kikuu!!

Baada ya Kumaliza chuo huku nikiwa na matarajio makubwa juu ya maisha, ndipo nilipokuja kugundua maisha siyo vile tunavyotaka yawe! Kupata kazi kilikuwa kimbembe kingine! Nilizungusha sana CVs bila mafanikio yeyote, zaidi ya mwaka nilikaa kwa ndugu bila kazi yeyote mpaka nilipoamua kuomba kazi ambayo haikuwa professional yangu! Nashukuru hiyo kazi ndiyo iliyonipa mtaji na mpaka sasa Nina lines of businesses na Nina ambitions za kufika mbali katika biashara zangu!!
Hivyo basi ugumu wowote tunaopitia una mwisho ikiwa utakuwa na nidhamu ya unachofanya, kuwa na subira pia kuheshimu wengine!!

NB: Maisha niliyopitia yamenifanya nisiwe Mtu wa kujali sana, mpaka sasa sijaoa wala sina mahusiano yeyote strong... Nikiwa mwenyewe huwa naona maisha ni bora zaidi kuliko nikiwa katika mahusiano!
Kingine ambacho huwa kinanitia hasira ni pale ninapoona watu waliokuwa kwenye position ya kuweza kunisaidia kwa lolote na hawakufanya hivyo wanapoanza kujileta leta.. Huwa naharibiwa siku kabisa!
Umeshare experience nzuri sana kwani itasaidia sana watu ambaowanakaribia kata tamaa. Kuanzamaisha darasala nne na kufanikiwa kufika ChuoKikuu! Hongerah sana. Ila wazazi japo hawakuacha miradilakini kuacha nyumba tu ni Baraka sana kwani inaonekana walifariki wakiwa siwazee. Hongerah sana kwa juhudi zako. Wengine watajifunzakuwa maisha magumi actually hujenga!
 
Back
Top Bottom