Tuliolipia pesa CDA kusubiri viwanja , ndo tumeibiwa au, presha juu

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
2,264
4,702
Habarini wanajamvini, mimi ni mmojawapo kati ya watu Zaidi ya 100,000 ambao wamelipia viwanja cda na walikuwa wanasubiri kupewa viwanja hivo, sasa wasiwasi wangu ni kwamba je ndo tayari tumeshapoteza haki zetu, mimi tu pekeyangu nililipa mil2.5 na cda waliniahidi wangenipatia kiwanja mwakani wakati pesa tulilipia mwezi wa tatu mwaka jana, huu ni uwizi ambao unaweza kutokea.

Pia naona kuvunjwa kwa cda kutasababisha watu wengi Zaidi kupoteza haki zao, ni kweli cda ilikuwa na matatizo yake lakini naona kama hii transition italeta maafa makubwa. Naomba raisi tu kama tutadhulumiwa pesa na viwanja tusipewe basi aturudishie pesa zetu mana tulilipia crdb tena katika akaunti yao hao cda na risiti za cda tunazo , hatuwezi kukubali,
 
Kwa vile wamesema shuguli za CDA zimehamishiwa kwenye Manispaa..
Nafikiri huko ndiko kwa kufatilia Mkuu..
Lukuvi amejitahidi kwa kiasi kikubwa kupaweka Ardhi vizuri na siku hizi mtu kudhulumiwa chake ni ngumu kidogo.
Linalogharimu ni ufatiliaji.
 
Daah!. Kama Rambirambi zililiwa, je nyie sasa? Pole sana Mkuu.

Hebu nenda Dodoma Manispaa.
 
Lukuvi anajitahidi sana kwenye wizara yake sema watendaji wake wa chini ni mateja wa rushwa, angewapeleka sober house ya rushwa wizara ya ardhi ingekua poa sana. Yani unaweza mkuta best au ndugu yako kabisa unamuomba akupimie viwanja kwenye shamba lako ambalo limekaribiwa na makazi anakwambia bila kumgawia viwanja hapo hapimi.
 
Hakuna kuibiwa!
Serikali yako ya Chama cha Mapinduzi ipo nanyi kwa raha na Shida mpaka Kifo kiwatenganishe

Shughuli za CDA hazijafutwa bali zinahamishiwa Manispaa ya Dodoma Mjini, Serikali ilifikiria yote kabla ya Nyinyi kufikiria

Hata waliopewa Hati ya Miaka 33 na CDA Mh. Rais wa Jamhuri na Mwenykt wa Chama ametaka hati hizo kugeuzwa na kuwa za Miaka 99!
 
Habarini wanajamvini, mimi ni mmojawapo kati ya watu Zaidi ya 100,000 ambao wamelipia viwanja cda na walikuwa wanasubiri kupewa viwanja hivo, sasa wasiwasi wangu ni kwamba je ndo tayari tumeshapoteza haki zetu, mimi tu pekeyangu nililipa mil2.5 na cda waliniahidi wangenipatia kiwanja mwakani wakati pesa tulilipia mwezi wa tatu mwaka jana, huu ni uwizi ambao unaweza kutokea.

Pia naona kuvunjwa kwa cda kutasababisha watu wengi Zaidi kupoteza haki zao, ni kweli cda ilikuwa na matatizo yake lakini naona kama hii transition italeta maafa makubwa. Naomba raisi tu kama tutadhulumiwa pesa na viwanja tusipewe basi aturudishie pesa zetu mana tulilipia crdb tena katika akaunti yao hao cda na risiti za cda tunazo , hatuwezi kukubali,

Ulitoa pesa kwa ahadi ya kiwanja hewa. Nasikitika kusema utaisoma namba. Toka mwaka jana bado hujastukia hilo dili! Subiri Manispaa ianze kazi pengine watakusaidia.
 
Hakuna kuibiwa!
Serikali yako ya Chama cha Mapinduzi ipo nanyi kwa raha na Shida mpaka Kifo kiwatenganishe

Je wakinyofoa bastola kiunoni ukishuka kwenye gari karibu na St Peters utatetea kauli yako?
 
Mkuu kama umelipia si unazo document kama risiti? Hizo ndio zitakuokoa kwa vile shuguli zinahamishiwa manispaa. Ila usiende mikono mitupu na kusingizia ooohhhh nilikuwa nadai CDA hauna document, hii awamu ya tano
 
Nadhani usemi wa "ngoja ngoja yaumiza matumbo "utakuhusu siku zote yanapotokea mabadiliko kuna watakaolia na kusaga meno na watakaofurahia
 
Habarini wanajamvini, mimi ni mmojawapo kati ya watu Zaidi ya 100,000 ambao wamelipia viwanja cda na walikuwa wanasubiri kupewa viwanja hivo, sasa wasiwasi wangu ni kwamba je ndo tayari tumeshapoteza haki zetu, mimi tu pekeyangu nililipa mil2.5 na cda waliniahidi wangenipatia kiwanja mwakani wakati pesa tulilipia mwezi wa tatu mwaka jana, huu ni uwizi ambao unaweza kutokea.

Pia naona kuvunjwa kwa cda kutasababisha watu wengi Zaidi kupoteza haki zao, ni kweli cda ilikuwa na matatizo yake lakini naona kama hii transition italeta maafa makubwa. Naomba raisi tu kama tutadhulumiwa pesa na viwanja tusipewe basi aturudishie pesa zetu mana tulilipia crdb tena katika akaunti yao hao cda na risiti za cda tunazo , hatuwezi kukubali,

Haki haiwezi Jupiter ila usiseme hatukubali contract yenu na cda
 
Back
Top Bottom