Uchaguzi 2020 Tuliokwama Kwenye Foleni Sababu ya Miundombinu Mibovu tuna Jambo Letu tarehe 28 Oktoba 2020

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
Dah,

Muda huu Saa Nane na Nusu usiku ndo naingia home. Nimetoka Stesheni saa kumi na moja jioni, gari ilikua nusu tank but kufika Victoria imeisha mafuta Sababu ya Foleni. Nimeingia hasara kununua tena mafuta Sababu tu ya kifoleni-mshenzi cha Palm Beach.

Nimeshinda na Njaa muda wote huo, sijala Chochote toka nlivokula saa saba mchana ndo nakuja kula muda huu. Hapa nimejitia risk ya vidonda vya tumbo. Home nimewaweka macho kunisubiri ili tu wasije wakapitiwa na usingizi na mlango haujafungwa.

Why nailaumu serikali? Sababu yenyewe ndio inajinasibu kuwa kwa miaka mitano hii imejenga Miundombinu ya kutosha hivyo tuichague Tena.

Hivi ni Miundombinu gani hiyo mvua ya siku moja mji mzima haupitiki kwa amani kila mahala foleni na/au mafuriko? Why Jangwani mpaka leo karne ya 21 kimvua cha siku moja tu panafungwa?

Kwa kweli katika hili nasema hapana, lazima tuonyeshane hapo 28-10 iwe isiwe.
 
Yani hii seeikali dhalimu lazima tuinyeeshe tr 28.Kazi yao kuminya wananchi ktk kila angle kuchaji parking hadi ktk mitaa ya majumbani zawatu sijui parking fees alaf miundo mbinu ni sifuri. Fisiemu is a failed party why cant tanzanians dig that out?

Haya yote mwisho ni tr 28 October tumechokaa
 
Sisi huku walipokuja kwenye kampeni wakatuambia wamejenga barabara za juu Dar huko na mnapita juu mpaka majumbani kwenu,wamenunua ndege saba,sasa inakuaje mnasema barabara za jiji hazipitiki.Na kwanini msipande ndege kufika kwenu?
Hizo fly overs mimi nilijuwa labda ni magari yamefungwa mbawa hivyo yatakuwa yana paa tuu,dah walah tarehe 28 sikubari lazima nifanye jambo langu
 
Shetani akamwambia Yesu , Ukinisujudia nitakupa fahari yooote hii maana Mimi ndiye mjenzi wake! Yesu akamwambia Nenda zako shetani imeandikwa utamsujudia Bwana Mungu wako yeye Peke yake.

Yesu alikataa Fahari za Dunia alipolazimishwa kumwabudu Shetani. Kuwalazimisha watu wamsujudia mungu mtu kwa sababu ya daraja ni kosa. Na naiona Tanzania itakayochwapwa viboko na Mungu Muumba wa vyote ambaye ameshasema kuwa yeye ni Mungu wa haki .

28/10/2020 watanzania tusikubali kumsujudia mtu mwovu kwa sababu ya Fahari za Dunia anazotuonyesha. Anawaonyesha watu majumba ,madaraja, pesa , Vyeo , madaraka na kutisha kuwanyima maji na hospitali yaani atawapiga kwa dhiki kwa kukataa fahari zake.

Tusimame katika haki.
 
Yani hii seeikali dhalimu lazima tuinyeeshe tr 28.Kazi yao kuminya wananchi ktk kila angle kuchaji parking hadi ktk mitaa ya majumbani zawatu sijui parking fees alaf miundo mbinu ni sifuri.Fisiemu is a failed party why cant tanzanians dig that out?
Haya yote mwisho ni tr 28 October tumechokaa
Tangu nikufahamu leo umeongea point. 👍
 
CCM sijui watajibu nini hapa. Maana haya ni maji ya shingo ndani miaka 50 na zaidi kero ni zile zile miaka yote. Pale Jangwani hata kipindi cha kiangazi panaonesha siyo sehemu aminika kabisa bado wakapitisha na Mwendokasi.

Hii kitu itawapotezea sana kura kama wataendeleza viburi kwa kujibu eti kwan Mvua imeletwa na CCM
 
Back
Top Bottom