tuliokulia Arusha hali ya uwanja wa sheikh amri abeid inaumiza sana

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Enzi hizo bana kabla ya kujengwa gombani pemba na ally hassan mwinyi tabora(viilikuwa moto enzi hizo)unaambiwa uwanja mzuri ulikuwa ccm kirumba ukifatiwa na sheikh amri abeid arusha maana wa dar es salaam ulikuwa ni kituko cha afrika,ismailia walisemaga ni uwanja wa kuchezea farasi kule kwao
Nikiwa mtoto na ball boy nimeshuhudia michezo ya AICC ilikuwa mikubwa sana kama sportspesa cup...nikashuhudia michezo ya mashirika ya posta afrika mashariki nikawaona watu hatari kama sam onyango jogooo
nikashudia team ya wanawake ya sweden ikicheza na arusha combain wanaume wakala kama 7 -0 nikashuhudia mohamed mwameja (akiwa sentahafu wa ndovu) akizaa na jirani yangu nilikuwa namuita aunt juddy mtoto wa mmiliki wa kitundu bar bar siku hizi shivaz
Nikawa rafiki(wa kushikwa mkono kuingizwa uwanjani mambo ya enzi hizo watoto ukishikwa mkono unaingia bure) wa HAMIS GAGA GAGARINO wakati huo ndovu / pilsner wanaishi mashele guest ,duh na MOHAMED BOB CHOPA, God bless those days,wachezaji wakipita mtaani (kumbuka hawakuwaga na magari )tulikuwa watoto tunaunga tela kuwashangilia .
Kikubwa zaidi hata michezo ya castle cup ilikuwa pia inaletwa arusha usisahau kulikuwa na kitu kinaitwa MOUNT MERU MARATHON nazungumzia marathon ya ukweli siyo magumashi ya rock city marathon au kili marathon huku niliwashuhudia kina BARIE,JUMA IKANGAA... kipindi hicho Tanzania iko juu ya kenya kwenye riadha
Uwanja hadi sehemu ya kukimbilia ulikuwa standard una vikokotoo vidooogo sijui vichangarawe vimesagwa vyeusi leo naona picha hizi toka Arusha,uwanja pembeni vumbi kama lijiwanja la VILLAGE ingawa sijaenda for years roho imeniuma sana nimewakumbuka hawa wazee waliokuwa wanatunza uwanja...ALLY MTUMWA,MZEE GEOFREY,BOKKASA KAJEMBE...
SHAME ON YOU CCM ARUSHA
 
Attachments

  • ars 2.png
    ars 2.png
    126.9 KB · Views: 5
  • ars 1.png
    ars 1.png
    107.4 KB · Views: 5
Sijui zamani ulikuwaje ila juzi kati niliutembelea umechoka sana huo uwanja.

Sijui watunzaji hawapo?
 
Hivi Viwanja havina hadhi ya kimataifa, vinahitajika viwanja vipya kujengwa ambavyo vitagharimu mabillioni

Kutegemea serikali ambayo hata vyoo vya shule za misingi inajengewa kwa misaada ya usaid au ukaid itakuwa ni kupoteza muda tu
 
Umenikumbusha kitambo sana enzi za utotoni, mambo ya fungulia mbwa na kuruka ukuta, sometimes tulikua tunapanda juu ya nyumba za annex kuchungulia mpira au show za akina Mbilia Bel na Bozi Boziana.

Mzee goefrey (RIP) alikuwa mkorofi sana na mapengo yake, Bokasa alikua mlinzi mbabe wa gate la chini. Huu uwanja hauna tena hadhi ya kuwa pale ulipo, umesongwa sana na biashara nyingine na hakuna hata parking kwa nje.
 
Kumbukumbu zangu mwisho ni kuwaona AFC enzi hizo wakiwa moto wanacheza na Pamba ya Mwanza uwanja unajaa full, Tukuyu Starz ya Mbeya uwanja unajaa full, Simba na Yanga wakija ndio balaa, siku hizi naona vumbi tu hapo uwanjani hakuna msisimko wa mpira tena.

TFF sijui wanaogopa nini kuvifungia hivyo viwanja vyenye pitch mbovu wakati wasimamizi wapo, timu zikicheza hapo wanachukua percentage za mapato ya viingilio mwishowe wanaenda kunywea bia tu.
 
Jamaa wamepora viwanja karibu vyote vya michezo kuvitunza hawawezi!
 
Hii nchi hatutapata maendeleo ya kweli kama tutaendelea kuiweka ccm mbele na Tanzania nyuma.
 
Nilikua sikosi mashindano ya Rolling Stone.

Timu za vijana toka E.A zote zilikuwepo.
 
Enzi hizo bana kabla ya kujengwa gombani pemba na ally hassan mwinyi tabora(viilikuwa moto enzi hizo)unaambiwa uwanja mzuri ulikuwa ccm kirumba ukifatiwa na sheikh amri abeid arusha maana wa dar es salaam ulikuwa ni kituko cha afrika,ismailia walisemaga ni uwanja wa kuchezea farasi kule kwao
Nikiwa mtoto na ball boy nimeshuhudia michezo ya AICC ilikuwa mikubwa sana kama sportspesa cup...nikashuhudia michezo ya mashirika ya posta afrika mashariki nikawaona watu hatari kama sam onyango jogooo
nikashudia team ya wanawake ya sweden ikicheza na arusha combain wanaume wakala kama 7 -0 nikashuhudia mohamed mwameja (akiwa sentahafu wa ndovu) akizaa na jirani yangu nilikuwa namuita aunt juddy mtoto wa mmiliki wa kitundu bar bar siku hizi shivaz
Nikawa rafiki(wa kushikwa mkono kuingizwa uwanjani mambo ya enzi hizo watoto ukishikwa mkono unaingia bure) wa HAMIS GAGA GAGARINO wakati huo ndovu / pilsner wanaishi mashele guest ,duh na MOHAMED BOB CHOPA, God bless those days,wachezaji wakipita mtaani (kumbuka hawakuwaga na magari )tulikuwa watoto tunaunga tela kuwashangilia .
Kikubwa zaidi hata michezo ya castle cup ilikuwa pia inaletwa arusha usisahau kulikuwa na kitu kinaitwa MOUNT MERU MARATHON nazungumzia marathon ya ukweli siyo magumashi ya rock city marathon au kili marathon huku niliwashuhudia kina BARIE,JUMA IKANGAA... kipindi hicho Tanzania iko juu ya kenya kwenye riadha
Uwanja hadi sehemu ya kukimbilia ulikuwa standard una vikokotoo vidooogo sijui vichangarawe vimesagwa vyeusi leo naona picha hizi toka Arusha,uwanja pembeni vumbi kama lijiwanja la VILLAGE ingawa sijaenda for years roho imeniuma sana nimewakumbuka hawa wazee waliokuwa wanatunza uwanja...ALLY MTUMWA,MZEE GEOFREY,BOKKASA KAJEMBE...
SHAME ON YOU CCM ARUSHA
Tom Kipese, Lazaro "Tingisha"...James Kisaka...ni baadhi ya wachezaji niliowaona ars nikiwa bwana mdogo.
Ligi daraja la tatu pale sheikh amri abeid,baadhi ya timu zilikuwa;
Waya mkali, Morani (Polisi), Faru,Home boys(Wakali wengi walikuwa humu..Shio na Cheupe)etc.
Getini namkumbuka mzee Bokasa na mzee mwengine mzee mzee hivi naskia alishafariki.
Kulikuwa na jukwaa la wavuta weed, la utani na vip..
Simba ilikuwa ikiutumia sana sheikh amri abeid nadhani na mapenzi yangu ya simba yalianzia humo..kipindi cha akina;
Mwameja, Alphonse Modest,Masatu,Masha,Chumila,Dua na Mustapha hoza...Arushaa
 
Back
Top Bottom