Tulioenda Dodoma ndiyo tulioshuhudia nguvu ya Edward Lowassa! Ana mikakati mizito!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Nimefuatilia jinsi wana CCM (wachache wao) na wananchi wengine baadhi wakilichukulia juujuu swala la Edward Lowassa kuhamishia majeshi UKAWA. Niseme tu kuwa hawamfahamu kabisa Edward Lowassa.

Kwanza kwa utangulizi tu, nchi hii ina watu watatu ambao mikakati yao ni zaidi ya majasusi wa CIA! Watu hao ni Edward Lowassa, Freeman Mbowe na mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Watu hawa wakiamua kuchimba chini hadi waimalize Tanzania kwa kutumia kucha zao wanaweza! Kimsingi ni wana mikakati wazito sana!

Sasa fikiria kwa undani sana watu hawa W ameamua kuungana na kuiweka mikakati yao pamoja! Ni nini kitatokea?

Hawa ni watu wasiotetereka kamwe! Wakisema sasa ni "A" wanamaanisha "A" kweli na siyo "a"!

Tulioenda Dodoma wakati wa vikao vya mchujo wa CCM tuliishuhudia nguvu ya Edward Lowassa! Alitakiwa zaidi ya ujuavyo! Watu walipoliona gari la Kikwete likipita walilikimbilia huku wakimuimba Lowassa! Kamati kuu ilivunjika mbele ya Lowassa! Idara ya usalama ilimeguka mbele ya Lowassa! Warioba alisema mbele ya Lowassa! Kingunge alishikilia msimamo mbele ya Lowassa! Unadhani ni kwa nini?

Magufuli analindwa kama rais! Haya yote ni matokeo ya nguvu ya Lowassa! Nguvu ya Lowassa ni kubwa sana, nguvu na ushawishi wa Mbowe mnaujua! Hawa sasa wameungana siyo bure siyo kitoto! Ikibidi kila kitu kitawekwa wazi ili kufanikisha kwa namna yoyote ile mikakati iliyokusudiwa.

Sasa wanamkakati watatu wameungana! Wana CCM ni lazima muelewe kuwa kimbunga kitasababisha maafa makubwa ni lazima kujipanga zaidi ya kujipanga!
 
Ccm walikua hawamjui Freeman Mbowe.. Walivyoona anajinyeyekeza kwa Cuf walimuona mjinga kumbe alikua tageti zake.. Na ile ilikua plan A kwa kunyakua kura za Zanzibar, Hapa anamalizia Gemu kwa plan B.. Nayo majibu yake ni kesho El akitua ukamandani.. Karibu Tanzania mpya
 
Mkuu unajua hata wanadamu tunabadilika eeeeh...
Kiukweli waondoke tu nimetunza kadi yangu 25/10 mapema nawahi nikamuondoe huyu Mkoroni mweusi

Taratib kitaeleweka tu mimi sina uchungu na alichofanyiwa lowasa ila dharau waliyomuonyesha makamu wa rais haielezeki.
Yaani kumuweka kwenye kapu moja na yule mkigoma!!
 
Back
Top Bottom