Hahahaha ikawaje sasaMimi babu langu alikuwa na nyumba zake mtoni mtongani sasa likizo huwa namtmbeleaga
Kuna siku nilipomtembelea nilikuta anaugomvi na mpangaji wake nilipofika tu akanambia nakupa mtihani ukiweza utakaa hapa likizo yote ukishindwa kweeenuuu, nikamwambia poa aknipa peni na karatasi akanambia anataka nataka umuandikie barua joseph ahame hivyo andika kama ninavyoongea usipunguze hata herufi moja akaanza na fyonyoo akambia andika ,akaja nyoooo' akaendelea JOSE JOSE SIKUTAKI KWANGU KAMA UMESIKIA HIKI KITUO CHA KULEA MASIKINI SIO KWANGU ,MTOTO HUNA HAYA KUTWA KUMUANGALIA MKE WANGU fyonyo la pili,,,,akaendelea HUKUNISAIDIA MCHANGA WALA KOKOTO (tusi) hukuleta mchanga wala nondo (tusi) kazi kuning'iniza...(tusi) akanigeukia na mimi ole wako lipungue neno nami nikala tusi laini akaongeaaaaa jioni nikawakuta baa wanakunywa pamoja eti mimi ndo mbaya nimetunga maneno nalazimisha urithi nilikuwa 4m4...dah yule mzee wa bandari alikuwa burudani saaana na alikuwa anapenda mnoooooo mis him much
Na bibi yangu akija mgeni anaanza kumsimulia,,Bibi yangu mzaa mama (RIP)alikuwa anapenda wageni jamani yaani hata mtu anapita njiani hapo kwake ni njia akimsalimia tu ataanza story nae hadi mtu anasimama masaa anamsimulia habari hata hazimuhusu. Alikuwa napenda kuteta watu "gossiping"
Dingi alinifukuza home nilipata ujauzito usio na maelezo mother akanipeleka kwa bibi. Yaani nilitetwa mimi halafu nasikia kabisa watu wakimuuliza tu Bibi mbona huonekani wee anaanza "nitaonekana vipi nimeletewa mzigo mzito kweli umo ndani, mzigo hauna mahari wala posa."
Ila alikuwa sio mchoyo wa chakula na hodari wa kulisha ila hazingatii ratiba breakfast babu anapewa saa sita lunch jioni kwa sababu ya kupenda kuongea na kila mtu kazi zake zinasimama. Ana ng'ombe wake anakamua maziwa anauza. Siku mteja akikosa maziwa tu akute maziwa yameisha ataanza kuniteta
"Kuna mzigo upo ndani unakunywa maziwa kama maji ya kunywa kwa kweli nashindwa kuelewa karibu nitakosa hata pesa ya madawa sasa maziwa ya biashara yote anamaliza "
Basi nikisikia naishia kulia tu.
Kituko sasa nimejifungua mwanangu bibi yangu anamwambia mama yangu ee uje upesi mtoto analia mdomo wake una sauti kali sijui kabila gani huyu mtoto halafu halali usiku kwani huyu mwanao kazaa na nani asije kuwa kazaa na majambazi maana ndio hayana adabu yanakesha usiku kuiba" anaongea hivyo kwa kutumia simu yangu hatanii anamaanisha. Halafu tupo wote hapo hapo.
Akimaliza hapo anakuletea uji wa maana na supu yaani nilikuwa nalia lakini misosi unafurahi na roho yako
Bibi yetu alikuwa hapendi kabisa ukae na Babu (RIP) kuongea chochote akikukuta tu lazima atawavuruga anasema mwacheni aongee na TV yake huyo si anaongea na wanawake zake wazungu. Kisa babu alizaa na mzungu watoto wawili miaka hiyo huko Uingereza wakati keshamuoa bibi alienda kusoma.
Babu alitangulia kufa baada ya siku tano bibi akafa wote walikufa wamelala. Walale salama huko waliko.
Jamani sanduku la bibi lilikutwa na pesa nyingi sana. Alikuwa ana pesa haishiwi. Pesa yake ya maziwa inakaa kwenye sanduku pesa ya matumizi watoto zake walikuwa wanampelekea kila mwezi. Na ile pesa babu hagusi. Ya kwenye sanduku hakuna aliyekuwa anajua kuwa kuna mipesa ndani Bibi yangu namkumbuka sana kwa kuteta na masimango mchaga yule mwisho.
Hahahahahah hiyo kaliyaani wazee wangu basi tuu,halafu babu yangu anapenda kuuliza SAA(muda)hata uwe umeenda Pluto hamjaonana miaka 20,ukiingiza tuu mguu ndani cha kwanza kukuuliza ni "hivi sasa ni SAA ngapi hapo"yani hana kummisi MTU wala nn hajui umerudi ukechooooka au vipi yy ni SAA tuu usipomjibu utamsikia " najua nawakera ila hamnipendi tuu"..na ukimjibu labda SAA 6:30 mchana baada ya dk 2 anauliza tena....eeeh unatamani umkate vibao akalazwe muhimbili
Mgemuuliza anaenda kuvifanyia ninibas bibi angu akija mjini kaz yake kuokota vitu vilivyotupwa ka makopo ya lotion viboks na nin anaweka chumba anacholala,na mkitupa ni ugomvi mkubwa na anarudi tena kuokota,cku ya kuondoka anachukua roba chafu anaviweka na ole wako ubadilishe roba sasa,siku moja tukachukua roba usiku tukalitupa asubuh sasa anapelekwa stand akauliza mzgo wake na akasema siondok ad nipewe mzigo wangu ikabidi tukamtafutie roba lenye vitu vyake
Hahahahahah hiyo kali
Mim bibi hana simu,akiomba apigiwe mtu flan halaf mkawa busy,anaanza nije tu ninunue simu yangu tu akitaka kununuliwa hataki tena
Dinazarde nimecheka had machozi jaman !dah eti ukiomba ng'ombe anasema miguu imevunjika !jamani nimecheka !i can imagine kwa bibi yako !Mungu ampe maisha marefu jaman muendelee kuenjoy !
mie sijaishi karibu na bibi zangu walikua hawajui kiswahili na mie sijui kisukuma bas nikawa napishana nao tu round about !rip bibi zangu
Weee tena hao usipime watata kama nini,tena ukute wale waliowahi kuwa mabepari mbona utahama nchiiHivi na mabibi wa kizungu wapo kama hawa wa kwetu?
Wewe kwenu upareni eee?Hivi na mabibi wa kizungu wapo kama hawa wa kwetu?
Hiko ni kipindi cha njaa ndio wazazi walikuwa wanafanya hivyo,wamama wanaweka mawe kwenye chungu mnayachochea moto kuanzia asubuh hadi jion wakati huo mzee anapambana huko mpate chakulaAlikua na maana gani kuchemsha jiwe kwenye chungu?
Rip dearest bibi yangu. Alikuwa na vituko sana alinipenda kuliko wajikuu wote wa ukoo mzima, walikuwa na uchoyo Fulani ila kwangu hakuna kitu ambacho sikula kwake.
Apumzike kwa amani, alifariki akiwa 96-age.nampenda hata Leo.