Tulio Arusha tupeane mawazo kuhusu hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulio Arusha tupeane mawazo kuhusu hili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MVUMBUZI, Jun 22, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni kutokana na mgao wa umeme kuwasababishia watu wengi hasara na hatimaye kuongeza umaskini nimeomba ushauri kama tunaweza kuanzisha Umoja wa Kisheria wenye lengo la kumlinda mtumiaji wa huduma mbalimbali hususani za jamii.

  Huduma hizi ni Umeme, maji, simu, n.k.

  Lengo la umoja huu ni kuwa na nguvu ya kisheria ya kumshataki mtoa huduma pale ambapo kukosekana kwa huduma yake kunasababisha hasara kwa mtumiaji au mlaji. Yaani kitu kinachofanana na " Consumer's Protection Network au kampuni. Kuanzishwa kwa mtandao huu kutokane na wanachama watakaoamua kukaa pamoja na kuanzisha jambo hili kwa manufaa ya watumiaji wote wa huduma husika.

  Lengo kuu:

  Ni kuwataka wale watakao shindwa kutoa huduma kwa expectation za consumers e.g. TANESCO wawalipe fidia ya hasara iliyopatikana na siyo kutoa majibu ya kibabe.

  Ninaomba ushauri wa Kisheria kutoka humu jamvini kama hili linawezekana ili tuanze mchakato haraka la sivyo ndugu zangu hatuna mtu wa kujitetea inabidi tuji- mobilise wenyewe ili kuondokana na hasara za kusababishiwa na irresponsible leaders.

  Angalizo:
  Hii Network haitajihusisha kwa namna yoyote na Siasa

  Naomba wenye pointi za kujenga tuchangiane mawazo wakuu na kama mtu ana hisi atatoa Mizaha basi asichangie aende kwenye jukwaa la JOKES siyo hapa.
  Karibuni na asanteni
   
 2. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  wakuu huu ukimya unaashiria kwamba wazo ni fake au mnaona haiwezekani?
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mimi naona Tuandamane bei ya Mishumaa Ishuke
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  Tanesco ni kichwa cha paka, hawasiii wala hawaoni tuombe tu CHADEMA ikamate nchi ndo tujue pa kuanzia.
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Issue ya kumfunga paka kengele lazima ijadiliwe
   
Loading...