Tulikuwa tukiandika kuhusu udikteta ndani ya Tanzania

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
Tulikuwa tukiandika kuhusu udikteta ndani ya Tanzania. Tumekemea uadui wa wazi, matamko ya vitisho kutoka kwa viongozi wakubwa, kauli za kutishia maisha ya watanzania kutoka kwa watu wenye mamlaka ya kuamuru majeshi. Baadhi ya kaka zetu na ndugu zetu walitushangaa sana; lakini sisi hatukuwashangaa kwa kutushangaa. Tuliwapa majibu mazuri tu! Kwamba hata Adolf Hitler na Benito Mussolini walikuwa na wafuasi wao wengi. Idd Amin Dada alikuwa na wafuasi. Joseph Stalin alikuwa na wafuasi. Emperor Hirohito wa Japan alikuwa na wafuasi. Kwa hivyo hatuwashangai wafuasi wa watawala ovyo wanaoishi kwa nguvu za damu za wengine, watawala wanaoishi kwa chuki, ghiliba, wivu, ukatili na kufurahia mateso ya wengine. Hatuwashangai.

Tukubaliane au tusikubaliane, Watanzania tumetumbukia shimoni. Tunaonja jehanamu tungali hai!

Ujumbe wangu kwa Rais Magufuli; Endelea kuishi kwa kututishia. Hatutaacha kukosoa kamwe, na hatuhami nchi hii.

Mwisho wa siku, miili yetu sote, pamoja na wako itaoza na kushambuliwa na funza wa ardhini, litabaki mifupa na hatimaye kutoweka kabisa juu ya uso wa dunia. Lakini Tanzania itabaki. Ni ukweli ambao wajinga hawawezi kuuishi hata ukiwaeleza kila siku.

Kwahiyo Mh. Rais; Jifunge vizuri mkanda wako, jipange kuamuru washika bunduki watuwinde kama digidigi, hatutaacha kukosoa. Na hatutainamisha shingo chini, tutasimama wima tukikutazama usoni kukueleza unapoteleza huku tukipuuza filimbi na vigeregere vya wajinga wanaoshabikia kauli zako za vitisho.

Karibu.
 
Taja basi na jina lako kama anavyofanya Pascal Mayalla.
Kama huogopi kufa.

Teeeh teeeh haaa haaaa haaaa haaa
 
Back
Top Bottom