Tulikuwa naye James Mbatia Juzi juzi tu hapa, Yupo wapi sasa?

Livejr

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
2,070
2,794
Wassalam wanajamvi…!

Kama kichwa cha mada kinavyosema huyu Mhandisi kwa sasa mbona hasikiki..?

Yupo wapi huyu mbunge wa VUNJO kiboko ya Mzee MREMA uchaguzi wa 2015…?

Yupo wapi huyu mteule wa rais wa awamu ya nne ambaye aliingia bungeni na hoja binafsi kuhusu ELIMU..?

Yupo wapi huyu Mh. Ambaye alikuwa msemaji wa UKAWA wakati sio katibu mwenezi, Kurugenzi wa habari au Katibu wa chama chochote miongoni mwa vile vinavyounda UKAWA…?

Yupo wapi huyu msemaji wa UKAWA kipindi cha kampeni ambaye kwa hakika alifanikisha vema dili la LOWASA kupeperusha bendera ya UKAWA kupitia CHADEMA. Ni huyu huyu Mh. Baadae aligeuka kuwa msemaji wa CHADEMA huku akiimudu vema nafasi ya ndg yetu Tumaini Makene.

Simsikii tena huyu Mh. Mbunge Mhandisi James Francis Mbatia akiwa anaimarisha chama chake au hata Bungeni kipindi cha Bunge la January.

Yu wapi huyu kiongozi wetu mwenye kujenga akiwa nyuma ya maiki kunako mjengoni..?
 
Huyu kamanda amebaki kama mkiwa ndani ya NCCR-Mageuzi..

Anaimba na kuitikia peke yake....
 
Umeenda home kwake au ofisini kwake umemkosa au unakimbilia JF kuanzisha Thread tu badala ya kufanya uchunguzi kwanza?
 
tulimwona mwanasiasa mwelevu kipindi kile kwa sbb wanasiasa wengi hawakuwa na elimu na uwezo kama wa sasa hivi amebakiza kupiga kelele tu
 
Wewe jamaa nina wasiwasi kama akili ni nywele unazo kama ni zaidi ya hapo huna akili na unaona kama Tanzania unaijua kumbe unapajua kijijni kwenu
 
ndio napajua kijijini kwetu, kwani sehemu gani nimesema naijua Tanzania yote..?
 
Wassalam wanajamvi…!

Kama kichwa cha mada kinavyosema huyu Mhandisi kwa sasa mbona hasikiki..?

Yupo wapi huyu mbunge wa VUNJO kiboko ya Mzee MREMA uchaguzi wa 2015…?

Yupo wapi huyu mteule wa rais wa awamu ya nne ambaye aliingia bungeni na hoja binafsi kuhusu ELIMU..?

Yupo wapi huyu Mh. Ambaye alikuwa msemaji wa UKAWA wakati sio katibu mwenezi, Kurugenzi wa habari au Katibu wa chama chochote miongoni mwa vile vinavyounda UKAWA…?

Yupo wapi huyu msemaji wa UKAWA kipindi cha kampeni ambaye kwa hakika alifanikisha vema dili la LOWASA kupeperusha bendera ya UKAWA kupitia CHADEMA. Ni huyu huyu Mh. Baadae aligeuka kuwa msemaji wa CHADEMA huku akiimudu vema nafasi ya ndg yetu Tumaini Makene.

Simsikii tena huyu Mh. Mbunge Mhandisi James Francis Mbatia akiwa anaimarisha chama chake au hata Bungeni kipindi cha Bunge la January.

Yu wapi huyu kiongozi wetu mwenye kujenga akiwa nyuma ya maiki kunako mjengoni..?
Anajenga jimbo lake acha umbea
 
Back
Top Bottom