Ogah Inawezekana kweli ndilo tatizo letu; ni ada yetu watanzania kutofanya mambo siriasi!! Teh!! teh!! teh!!!Mwl Kichuguu,
BTW.......unakumbuka tuliwahi kuwa na mijadala ya namna hii......na kuna sehemu tulifika kwenye ule mjadala tukaona tunachokosa ni Katiba inayokidhi yale tuyatakayo kama nchi..............tukaanza mchakato wa kukusanya maoni na mapendekezo yetu.....yaliyotokana na ule mjadala katiba ikiwemo......mpaka ikawekwa electronic copy ya katiba........tena nakumbuka wewe ulijitolea kuhariri maoni......hivi ile kazi iliishia wapi......au ndio matatizo yenyewe tuliyonayo?
Dah umenikumbusha mbali sana mkuu wangu.. Nakumbuka vizuri kile kazi tulikorogana sisi wenyewe baada ya kushindwa kupata mjenzi wa blog au tovuti, kuna mtu Marekani nimemsahau jina lake aliingia mitini basi tukabakia kushabikia mgogoro wa Jambo na Jamii.. Unajua tena wasahili wakiona ngumi huacha hata kazi zao kuja tazama masumbwi..Taasisi ndiye alikuwa mhariri wa kazi ile naye sijui kaishia wapi..Ebu fikirieni ilivyokuwa rahisi leo halafu just five or six yrs ago tulikuwa tunapata shida..Mwl Kichuguu,
BTW.......unakumbuka tuliwahi kuwa na mijadala ya namna hii......na kuna sehemu tulifika kwenye ule mjadala tukaona tunachokosa ni Katiba inayokidhi yale tuyatakayo kama nchi..............tukaanza mchakato wa kukusanya maoni na mapendekezo yetu.....yaliyotokana na ule mjadala katiba ikiwemo......mpaka ikawekwa electronic copy ya katiba........tena nakumbuka wewe ulijitolea kuhariri maoni......hivi ile kazi iliishia wapi......au ndio matatizo yenyewe tuliyonayo?
Chifu Kichuguu, kwa mujibu wa sheria za ardhi namba 4 na 5 za mwaka 1999, ardhi yote ya Tanzania ipo chini ya mamlaka ya rais. Hivyo suala la mikataba ya ardhi ya aina hiyo lipo ndani ya uwezo wa rais. Kwanini? Kwa sababu sheria hizo zinampa uwezo rais kuchukua ardhi yoyote kwa manufaa ya umma na taifa; rais Ana mamlaka ya kuvunja mikataba hiyo kwa manufaa ya taifa. Lakini kwa rais huyu sioni Kama hili jambo linaweza kutekelezwa. Angalia yanayoendelea Bonde la Kiru, Babati na kule Grumeti; maslahi ya wawekezaji tena wa nje ndiyo yanapewa kipaumbele dhidi ya maslahi ya taifa. Ndiyo maana naamini kama tukiweza kuchanga na kucheza karata zetu vizuri, mwanya wa kuandika katiba mpya unaweza kutumika katika kuweka misingi imara ya kuliwezesha taifa kutekeleza 'mixed economy'.Nzi,
Mfumo unaojulicana kama "mixed economy" yaani mchanganyiko wa ujamaa na ubepari ndio mfumo uliozikomboa nchi nyingi sana duniani hasa huko Asia. Serikali inasimamia maswala ya elimu, huduma za afya, na kumilik biashara nyeti kwa taifa kama mali asili, nishati, na njia kuu za usafirishaji kama treni, usafiri wa anga huku ikiwahimiza raia wake (siyo raia wa nje) kuwekekaza katika biashara hizo. Wakati huo huo ikiwaachia watu binafsi wajifanyie biashara zao nyinginezo.
Ma-giants wote wa uchumi huko Asia: Singapore, Taiwan, China, Korea, na Japan walifanya hivyo. Sehemu nyingi za skandinavia zinaendesha uchumi wa namna hiyo hadi leo, na Hata Australia nayo inafuata uchumi wa aina hiyo hiyo.
Je Tanzania tuchukue hatua gani ili kurudi kwenye uchumi huo iwapo viongozi wetu walishasaini mikataba ya miaka 99 na makampuni ya nje?
Lakini mkuu wangu mikataba yenyewe imewekwa na rais iweje yeye tena ndiye aivnje kwa sheria hiyo?..Si lazima kuwepo na ushahidi tosha kwamba alokabidhiwa ardhi hiyo amekiuka?.. Haya tumeingia mikataba ya madini kwa ruzuku halafu hadi madini yaishe kwa kuwaamini Barricks ndio wafanye mahesabu yao na kuyawakilisha.Chifu Kichuguu, kwa mujibu wa sheria za ardhi namba 4 na 5 za mwaka 1999, ardhi yote ya Tanzania ipo chini ya mamlaka ya rais. Hivyo suala la mikataba ya ardhi ya aina hiyo lipo ndani ya uwezo wa rais. Kwanini? Kwa sababu sheria hizo zinampa uwezo rais kuchukua ardhi yoyote kwa manufaa ya umma na taifa; rais Ana mamlaka ya kuvunja mikataba hiyo kwa manufaa ya taifa. Lakini kwa rais huyu sioni Kama hili jambo linaweza kutekelezwa. Angalia yanayoendelea Bonde la Kiru, Babati na kule Grumeti; maslahi ya wawekezaji tena wa nje ndiyo yanapewa kipaumbele dhidi ya maslahi ya taifa. Ndiyo maana naamini kama tukiweza kuchanga na kucheza karata zetu vizuri, mwanya wa kuandika katiba mpya unaweza kutumika katika kuweka misingi imara ya kuliwezesha taifa kutekeleza 'mixed economy'.
Lakini mkuu wangu mikataba yenyewe imewekwa na rais iweje yeye tena ndiye aivunje kwa sheria hiyo?..Si lazima kuwepo na ushahidi tosha kwamba alokabidhiwa ardhi hiyo amekiuka?.. Haya tumeingia mikataba ya madini kwa ruzuku halafu hadi madini yaishe kwa kuwaamini Barricks ndio wafanye mahesabu yao na kuyawakilisha.
sababu ya nchi zote kudai ubia na asilimia ktk share sio tu kumiliki hiyo mali bali pia kufahamu mahesabu na thamani ya mauzo na matumizi maana mko share. Leo hii maadam hatuko share na Barricks hesabu zozote wanazotuletea inabidi tuzikubali.
Toka 2003 hadi leo miaka 10 hawajalipa corporate tax kwa sababu wanadai hawajarudisha fedha yao..Na walivyo wajanja wakijenga shule, wakitoa misaada yote hizi zote zinaingia ktk gharama zao maana wanatakiwa kuwa answerable kwa investors na sio serikali ya Tanzania..Sasa mkuu wangu mkataba wenyewe hadi madini yaishe, utapindua vipi wakati majority shares wenyewe ni Bush, Kashogi na Moroney!.. Sii ndio tutakuwa Iran au Afghanstan nyingine....
...Kichuguu,Hata mimi ni muumini mkubwa sana wa all politics is local; lakini nimewahi kuishi katika vijiji ambavyo vina local politics nikakuta kuwa bado viongozi hawajibiki tena. Yaani wananchi wanakuwa wanamhusudu yule kiongozi waliyemchagua anapokuwa anajineemesha kwa raslimali zao. Kumpinga inakuwa kama vile ni kumuonea wivu! Ule ujasisri wa kumwajibisha mtu hatuna kabisa.
...Nadhani, inabidi tukubali kuwa, kwa maendeleo tuliyonayo leo -ambayo, how ironic faida zake hazijaweza sambaa kwa wengi- ya kuweza kupata habari, kusoma, na kutumia teknolojia za kisasa kabisa, tumeweza kuona, kuchambua, na kufahamu matatizo yetu na hata kubainisha hatua sahihi za kuchukua. Hata hivyo, hatutafanikiwa kama taifa kwa kuwa wengi ni wajinga na ndio kwanza wanajifunza. Europe walitumia miaka mingi kufikia industrial revolution, na hata hapo bado walikuwa na kazi kubwa ya kufanya.Swali langu la leo zaidi ni kuhusu tabia zetu kama watanzania kubadilika vile ingawa tulikuwa chini ya katiba hiyo hiyo. Ingawa sote tunayoosha kidole kwa uongozi na utawala kwa jumla, nadhani tukubalinae kuwa tabia zetu binafsi nazo ndizo zinazosababisha tuwe na uongozi mbuvu, siyo kweli kuwa uongozi mbovu ndio unaotuletea tabia mbaya. Hali ya uchumi ni sababu moja kama ambavyo wengi tunaamini ila kama DAR si LAMU alivyoainisha tena, na nimekubaliana naye ni kuwa tuna tabia ya unafiki sana wa kufanya mambo kiuongouongo na kibabaishaji ndiyo imezalisha hayo mengine mengi. Hata kama tutakuwa na katiba nzuri lakini tukajiendesha kwa mtindo huu huu wa kutokuwa na ethics, na unafiki basi katiba itabaki ni kijitabu tu. Ni kama ambavyo hivi sasa tuna sheria dhidi ya rushwa na tuna vyombo vya kupiga rushwa lakini hakuna linaloendelea. Inabidi kwanza tuangalie namna ya kutibu tabia zetu sisi wenyewe kabla ya kuangalia sheria zikoje; jambo ambalo kama Mkandara alivyoweka bayana ni kuwa tabia hizi zimejengwa kutokana na elimu duni na umaskini.
Ni mawazo mazuri sana lakini sio kwa Maskini na Mjinga.. Umuhimu wa kuweka Umaskini na UJINGA kua vipaumbele ndio njia pekee ya kumkomboa Mtanzania. Pasipo elimu tutaendelea kuvaa mitumba, madawa feki, na households ktk fikra za kimtoni (kama Ulaya) badala ya kukabili mahitaji yetu ktk standard ya juu kulingana na mazingira..Tunaagiza juice ya machungwa, tende na hata nazi kutoka Dubai ni kwa sababu ya UJINGA na huwezi kumweleza kitu Mdanganyika aliyezoea juice ya embe kutoka Dubai.Kwa maoni yangu binafsi. Matatizo ya Tanzania ni matatizo ya kijamii. Swali,kama rais au serikali ingeingia mikataba mizuri na wawekezaji katika sekta ya madini, je kungekuwa na ufanisi wowote?
Kama serikal ingekuwa na sera nzuri ya nishati na kufanya nchi kutokuwa na matatizo ya umeme, je watanzania wangekuwa na tabia nzuri za ufanyaji kazi?
Majibu katika maswali hayo juu ni hapana. Matatizo ya umeme, matatizo ya mikataba mibovu, matatizo ya kutokuwa na uwajibikaji makazini ni matokeo ya matatizo ya kijamii na sio kiini cha matatizo hayo.
Matatizo yanayotokea Tanzani sasa hivi ni mavuno ya tulichopanga miaka mingi iliyopita. Na kuondoa matatizo hayo turudi kwenye basics.
Kitu cha kwanza, sera za serikali ziandaliwe kwa kutumia resources zinazopatikana katika jamii (live within your own means). Mtu anayetegemea misaada ya wahisani kusomesha watoto wake shule au kujenga barabara, hawezi kuwajibika.
Pili, all politics is local. Umefika wakati watanzania wapewe madaraka ya kuchagua na kuongoza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Mkuu Kichuguu na wanajamvi, ni kweli kuwa kuna mwingiliano mkubwa sana wa hayo aliyoorodhesha kichuguu.(a) Hatujali kabisa ethics za kazi; nadhani hili linaeleweka sana.
(b) Hatujitumi kazini katika majukumu ambayo hayana rushwa; hatuogopi utendaji mbovu.
(c) Tunapowewa madaraka, tunaamini kuwa tuko entitled kuwa na madaraka hayo, na tunaweza kujipatia chochote kutokana na madaraka hayo.
(d) Tunathamini sana mali kuliko heshima; tuko tayari kulamba kiatu cha mwekezaji ili atupatie kitu kidogo.
(f) Tunapenda sana njia za mkato kwa kila kitu. Tukiwa na matatizo tunapenda kumtafuta mtu mwingine atutatulie
(g) Hatutaki kuwajibika wala kuwawajibisha tuliowapa majukumu. Kila wakati tunaamini kuwa tuko right, yanapotokea makosa katika mazingira yetu basi tunakuwa wa kwanza kutafuta mtu au kitu cha kulaumu; tukikosa kitu cha kulaumu basi tunamlaumu Mungu.
Mambo haya yameungana kiasi kuwa ni huwezi kuondoa moja ukaacha mengine. Kwa bahati mbaya mambo hayo ndiyo yanasoababisha tunashindwa kuendelea.
Nina maswali mawili ya kujiuliza:
(a) Ni wapi tulipokosea hadi tukajenga element mbovu hizo katika maisha yetu?
Nina imani hali ngumu ya uchumi iliyosababisha mapato halali ya wananchi kupungua vilisaidia kusababisha watu waanza kuachana na ethics za kazi kwa kutafuta rushwa, na kuanza kutumia nafasi za kazi zao kufanya biashara kinyume na masharti ya kazi. Lakini je kweli hiyo ndiyo iliyokuwa sababu pekee? Wizi wa mabilioni ya fedha za umma kweli ni kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi? (b) Je tufanye nini sasa ili kurekebisha makosa hayo?
Kichuguu, wenye lugha zao wanasema 'The buck stops with president'Mkuu Nguruvi, uliyosema ni kweli kabisa. Ila lile swala la rais anayeteua watu hao naye kutojali wakati yeye ni mtanzania mweneztu aliyepewa dhamana ya kulea taifa hili ndilo jambo la kujiuliza tena kuwa Wataznaia tulikosea wapi basi hadi tukawa na viongozi wa aina hiyo?
...Ni kweli, tatizo hapo si elimu, kwao wao. Tatizo ni mwajiri wao -kwa maana ya aliyewapigia kura- amechukua hatua gani ya kuwarejesha kwenye mstari?. Na ndipo tunarudi kule kule!.(1) Je ni kweli kuwa watu wote wanofanya mambo hayo ya kutowajibika hawana elimu ya kujua mabaya na mazuri kwa taifa? Mbona watu wtote walliowahi kushukliwa kuliingiza taifa hili kwenye hasara kubwa sana za kimataifa ni wasomi tena wa hali ya juu? Hilo linoanonyesha kuwa ignorance siyo tatizo central. Wala rushwa wote na wanoongoza kwa kutowajibika ni wasomi walio kwenye nafasi za juu sana serikalini.
...Jamii hii haijawahi kuwa huru -kimawazo na tena hadharani- toka tupate uhuru. Na kama hauko huru, ni gharama sana kufuta ujinga katika jamii hii changa. Bahati ya jamii nyingine -wachina wanaweza kuwa mfano- zilielimika miaka mingi nyuma, na kuwa huru katika vipindi fulani fulani. Hii imewafanya wajue wanahitaji kitu gani na namna gani wakipate, bila longo longo nyingi kuwa na nafasi.(2) Je hiyo ignorance ilianguka ghafla ikajaza matope ndani ya jamii yote au ilianguka kidogo kidogo hadi taifa zima likafunikwa na hayo matope kama ilivyo leo? Iwapo ilianguka ghafla, je ilitokea lini, na ni sababu zipi zilizofanya ianguke? Iwapo ilianguka kidogo kidogo, je ilianza kuangukia wapi, na ni kwa nini ilianzia hapo? Swali hili lenye vipande viwili ndiyo jambo kubwa sana ambalo litatusaidia kuangalia wapi wa kusahihisha iwapo tatizo ndilo hilo.
...Ujinga ndio kosa letu. Lazima tukubali tu wajinga, ili, tuwe tayari kujifunza na kuelewa.Ila lile swala la rais anayeteua watu hao naye kutojali wakati yeye ni mtanzania mweneztu aliyepewa dhamana ya kulea taifa hili ndilo jambo la kujiuliza tena kuwa Wataznaia tulikosea wapi basi hadi tukawa na viongozi wa aina hiyo?
Zakumi,
Hata mimi ni muumini mkubwa sana wa all politics is local; lakini nimewahi kuishi katika vijiji ambavyo vina local politics nikakuta kuwa bado viongozi hawajibiki tena. Yaani wananchi wanakuwa wanamhusudu yule kiongozi waliyemchagua anapokuwa anajineemesha kwa raslimali zao. Kumpinga inakuwa kama vile ni kumuonea wivu!
Ni mawazo mazuri sana lakini sio kwa Maskini na Mjinga.. Umuhimu wa kuweka Umaskini na UJINGA kua vipaumbele ndio njia pekee ya kumkomboa Mtanzania. Pasipo elimu tutaendelea kuvaa mitumba, madawa feki, na households ktk fikra za kimtoni (kama Ulaya) badala ya kukabili mahitaji yetu ktk standard ya juu kulingana na mazingira..Tunaagiza juice ya machungwa, tende na hata nazi kutoka Dubai ni kwa sababu ya UJINGA na huwezi kumweleza kitu Mdanganyika aliyezoea juice ya embe kutoka Dubai.
Zakumi mkuu wangu karibu usipotee hivyo.. Kitu kimoja nakubaliana na wewe kuwa tatizo la Tanznaia ni sisi Watanzania wenyewe lakini sidhani kuwa ni swala la fedha na malipo sawa na thamani ya kitu. Nijuavyo interaction ya supply and demand ndio kutupa bei ama thamani ya kitu. Huwezi kumchukua maskini ombaomba kumuuzia elimu ambayo kwake sio priority ya siku wlaa maisha maana hana hata hela ya kuweka mkate mezani unafikiri kweli ataithamini elimu?. Hivyo as long as price is derived by demand and supply, the resultant market price ya mwalimu (supplier) haiwezi kuwepo ikiwa maskini hana demand na elimu hiyo.Samahani kwa kupotea. Majukumu mengi.
Point yangu ya mwanzo ni kuwa tuna matatizo makubwa. Na taaluma ya kutatua matatizo mengine ni sawa na kuuliza Kuku na yai nani wa kwanza.
Tukisema watanzania tatizo letu ni elimu, ni lazima ujiulize je unaweza kupata waalimu wazuri bila ya kuwa na uchumi wa kulipa mishahara mizuri kwa walimu?
Ukisema all politics is local, ni lazima vilevile ukubali kuwa wananchi wachague viongozi wao na watoe kodi za kugharimia shughuli zao za maendeleo. Mtu akitoa mchango wake, haogopi kiongozi.
Wanachama wa Simba na Yanga wako passionate na clubs zao na wako tayari kuchapana bakora kwa sababu wanatoa michango ya kuendesha clubs hizo.
Similarly, watanzania wakichangia huduma zao watakuwa tayari kupigania ubora wake.