Tulia Ackson aandika historia mpya ya kuwa Spika wa kwanza kubariki Rushwa bungeni

Samson Kwayu

Member
Jun 9, 2022
18
90
Bunge letu la Tanzania leo limeingia kwenye historia nyingine ya kuwa kitu cha ajabu sana kwa kauli za Spika Dokta Tulia kuita rushwa kuwa ni kitu cha kawaida kufanyika.

Spika akijua kabisa siyo sawa leo amekitetea kwa nguvu sana kitendo cha wabunge kukubali rushwa ya mitungi ya gesi 100 kila mbunge kutoka wizara ya nishati na waziri wa nishati na Spika anadiriki kusema eti wao ni wawakilishi wa wananchi hivyo wamepokea hiyo mitungi kwa niaba ya wananchi.

Spika anatetea kitendo hiki na kuita ni cha kawaida, lakini sisi ni watu wenye akili na ufahamu tunajiuliza kama ni kawaida mbona wizara ya kilimo ya Bashe haitoi mifuko 100 ya mbolea ya ruzuku kwa kila mbunge akagawe jimboni kwake? Au basi Ummy Mwalimu mbona hagawi maboksi ya kondomu, au P2 au vyandarua 100 kwa kila mbubge akagawe jimboni kwake? Mbona wizara ya ujenzi hawagawi mifuko ya sementi au nondo 100 kwa kila mbunge akagawie wananchi huko majimboni?

Kilichostua zaidi Spika anasema fedha hiyo imetoka kwenye bajeti ya 2022/23 lakini tumetafuta kwenye mafungu yote ya fedha za bajeti iliyopita hatujaona hii bajeti ya kununua na kugawa mitungi 100 kwa kila mbunge.

Hatujaishia hapo tumepiga hesabu na kugundua kuwa jumla ya 1.2bn TZS zimetumika kwa jambo hili. Hivi kweli sisi ni taifa tunalojielewa kweli? Kuna rushwa zaidi ya hii tunaweza kuielezea?

Hesabu zake ni nyepesi sana. Mitungi ya gesi 100 x wabunge 320 x 40,000/= ni sawa na 1.28 bn TZS. Hii hela imetoka kwenye bajeti ipi? Na kama ni kweli basi CAG kwa nini hukuona hili?

Tunajua hii hela ilikotoka na hatutasema sana kwa sababu tuna kawaida ya kutunza silaha kwa ajili ya baadaye.

Spika Tulia leo umeliingiza bunge tukufu kwenye sifa mbaya na ya hovyo sana kuwahi kudhaniwa unaweza kuifanya ukiwa spika wa chombo kikubwa namna hiyo.
 
Wanaume wa "kitengo" ni kama wanaume wa dar tuu.... mnashindwaje kuyachoma moto haya majizi wakati mnadugange pamoja kwenye Guest za hapo mjini. Hivi hakuna kijana mmoja wa kitengo ajitoe muhanga hapo hata ayachome hayo mabonge humo mjengoni na vikao vyao vya wizi.
 
Wanaume wa "kitengo" ni kama wanaume wa dar tuu.... mnashindwaje kuyachoma moto haya majizi wakati mnadugange pamoja kwenye Guest za hapo mjini. Hivi hakuna kijana mmoja wa kitengo ajitoe muhanga hapo hata ayachome hayo mabonge humo mjengoni na vikao vyao vya wizi.
 
Back
Top Bottom