Tukumbushane wanawake(Jifunze kuishi bila yeye)

Tukumbushane wanawake(Jifunze kuishi bila yeye)

Gentlewoman

Senior Member
Joined
Aug 13, 2018
Posts
192
Reaction score
393
Kama unataka mume wako au mchumba akuheshimu ni lazima umuonyeshe kua unaweza kuishi bila yeye

kwamba pamoja na kumpenda sana lakini mwisho wa siku unaweza kuishi bila yeye na kuwa na furaha.

Wanaume wengi siku hizi hawajiamini na kuona ufahari kuwanyanyasa wanawake,wakiamini wanaweza kuwafanya chochote na hawawezi kuondoka au kuwaacha kwa kuwa wanawategemea kwa kila kitu
Kwa maana hiyo basi kwanza hakikisha kuwa unakuwa huru kwa kipato,unakuwa na kazi au biashara ambayo unaweza kukufanya kujitegemea.

Lakini hiyo haitoshi acha kuwa mtu wa huzuni,mtu wa kulalamika lalamika,na kumfatilia kila saa,usiku anapochelewa kurudi anakukuta umekaa macho unalia na kulalamika lalamika

Unaweza kuwa unaumia lakini kila Mara unapolia na kulalamika ndiyo unazidi kumpa nafasi ya kuendelea kukuumiza,atakufanyia makusudi ili uzidi kuumia.

Jifanye kama huumii,acha kulalamika lalamika unapomuona.Lia na umia akiwa hayupo lakini akiwepo kuwa sawa

Kumbuka jitengenezee ujasiri hata kama si kuondoka,lakini kuwaza maisha bila yeye.
Kwamba ushavumilia sana,ushamuomba MUNGU sana na bado habadiliki anaendelea kukudharau kukupiga na kukuonyeshea wanawake wake hadharani,sasa kwa nini uendelee kusubiri mpaka akuue kwa presha,akuletee UKIMWI

jifunze kuwa huru na kujitegemea kabla haja kuharibia maisha yako
Usemi wangu siku zote

"Nakupenda ila naweza kuishi bila wewe".
Gentlewoman.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu uwe unasoma vizuri tena kwa umakini,huo ni ushauri wangu kama ukumbusho kwa wanawake wenzangu,kuna sehemu nimesema nimeachwa???!!!!,

Sent using Jamii Forums mobile app
Si lazima useme umeachwa, kuna mambo mengi yanayojulisha kuwa umeachwa hivi karibuni au miaka ya hivi karibuni. Mojawapo ni hiyo Avatar yako. Avatar inaniambia kuwa unajitahidi kushindana na ukweli ulio moyoni mwako kuwa bado jamaa unampenda.
 
Ushauri wako nimzuri ila nikiuchambua kamavile unawapotosha wanawake namaanisha kuwa nyumba inafahari mmoja sasa wakiwa wawili hvi neno ndoa litakamilika kweli hapa wakati mwngine sio sahihi kwakuwa mwanamke kwenye familia anabaki kuwa mwanamke na mwanaume anabaki kuwa mwanaume tu na mwanamke uwezi kuishi peke yako ukakamilisha sifa ya kuwa mwanamke na mwanaume uwezi kuishi peke yako ukakamilisha sifa ya kuwa mwanaume labda ngane na mjane otherwise uwe na mapunguvu wanawake mmepewa akili unalo ambiwa changanya na zakwako pengine uyu mwenyewe anadharau na kiburi sasa kazinguliwa na mumewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sinyanyaswi ila nimeandika kwa ajili ya wanawake wanaonyanyasika ktk ndoa au mahusiano,si kila mwanamke ana wa kumuelezea shida zake au matatizo ya ndoa yake au uchumba ndo maana nimeandika ili kuwaamsha kifikra nao waone wanaweza kutoka hapo walipo na kupiga hatua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamekuja kukwambia wananyanyasika mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si lazima useme umeachwa, kuna mambo mengi yanayojulisha kuwa umeachwa hivi karibuni au miaka ya hivi karibuni. Mojawapo ni hiyo Avatar yako. Avatar inaniambia kuwa unajitahidi kushindana na ukweli ulio moyoni mwako kuwa bado jamaa unampenda.
Hahaha kumbe umeangalia avatar hahaha pole kwa kukalili mkuu,sidhani kama ni sababu ya muhimu,sina haja ya kujielezea saaanaaa, baki na jibu hilohilo ulonalo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha kumbe umeangalia avatar hahaha pole kwa kukalili mkuu,sidhani kama ni sababu ya muhimu,sina haja ya kujielezea saaanaaa, baki na jibu hilohilo ulonalo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitetee hoja yangu kwa kutumia nukuu toka ndani ya Biblia.
Mathayo 12:34 inasomeka ifuatavyo.
Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake.
Hivyo basi, kile unachoshauri ndicho kimejaa moyoni mwako, na hakiwezi kujaa pasi na sababu.
 
Back
Top Bottom