Tukumbushane maneno haya kuhusu maisha

Tukumbushane maneno haya kuhusu maisha

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2021
Posts
484
Reaction score
547
Tunakumbushana tu wala sina jipya sana!
__________________________________________________________
Moja
Wema na ubaya vyote ni mbegu na vyote ukivipanda vinaota na mvunaji ni wewe uliyevipanda! Tunakumbushana kwamba ukipanda bangi huwezi kuvuna mahindi!

Mbili
Unaweza kuishi miaka mingi ukiteseka kwa sababu kuna watu uliwatesa sasa unavuna ulichopanda pia unaweza kuishi miaka mingi ili ushuhudie wale waliokutesa wanavyoteseka. Tunakumbushana tu kwamba kila mtu huvuna alichopanda na siyo alikopanda!

Tatu
Watu wenye ujasiri mkubwa katika kufeli wakipata changamoto hulia hadi Kingereza huku wakijiuliza "why me" na kisha kuendelea kulia, washindi yakiwakuta hujiuliza why me na kujijibu "It is me because I'm the one who can control it" huku wakiwa na faraja ndani yao. Tunakumbushana tu ili tufike salama!

Nne
Kutenda ubaya ni sawa na kutema mate juu, lazima ya kurudie, tena yanarudi yametawanyika kujaza uso wote! Tunakumbushana tu kwamba imeandikwa katika vitabu vyote vya dini, “usimtendee mwenzako kile usichopenda wewe kutendewa!”

Tano
Juhudi za kutumia nguvu nyingi bila akili hazitakufikisha popote zaidi ya kusaidia wengine kufanikiwa kupitia wewe. Tunakumbushana tu kuwekeza kwenye akili hata maana nguvu zina ukomo, akili haina ukomo!

Sita
Unapozinguana na mpenzi wako usiwe na tabia ya kumshitaki kwa ndugu zako maana siku utakapomsamehe ndugu zako hawatamsamehe! Tunakumbushana tu kwamba kama ukiona mahusiano hayasongi, songa wewe!

Saba
Kupanga matumizi kwa pesa za watu ni utapeli, kumbuka cha mtu mavi walisema wahuni, ipo siku kitakutokea puani! Tunakumbushana tu kwamba ukila vya watu usilalamike na vyako vikiliwa maana lazima viliwe tu!

Nane
Utajiri hauji kwa ubahili, utajiri unakuja kwa utoaji ndiyo maana wanaotoaga misaada mikubwa wanaendelea kutajirika na mabahiri waneendelea kukaukiana tu! Tunakumbushana tu kwamba asiyepoteza haokoti.

Tisa
Hakuna matumizi mabaya ya pesa, shida ni kwamba pesa hazipo, kama hauna pesa hata ukiona mtu kanunua kigari cha watoto wake utasema ni matumizi mabaya ya pesa bora angenunua debe la unga na maharage. Tunakumbushana tu kutafuta pesa ili tuache kuumia kwa matumizi ya watu!

Kumi
Kumbuka Mungu ni wa kila kitu, siyo magumu tu hivyo jenga mahusiano mazuri na Mungu wako hata wakati wa raha na siyo wakati wa shida tu. Tunakumbushana tu kumkumbuka Mungu wakati wa magumu tu magumu yatakuwa sehemu ya maisha yako maana akiyaondoa utamkimbia!

Wako

Muhenga wa Karne ya 21!
 
Makonda anajisikiaje anapoona Rizmoko amepewa shavu, Nape kala shavu, Chongolo kala shavu na list inaendelea ?

Yaani kimsingi Ile team aliyokuwa anaitunishia misuli ambayo ndio waliomshika mkono na kumnyanyua akaja kuwageuka na kuwatishia pistol na wengine akawaweka ndani kwa kuwatuhumu kwamba ni wauza ngada??

Arudi kijijini aisee, nasikia Kuna muda alijificha njiro kwa wakwe zake.
 
Back
Top Bottom