Tukumbushane mambo haya muhimu kuhusu mikopo

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,915
3,407
1. Usichukue mkopo kwa ajili ya kufanya sherehe..
2. Usichukue mkopo kwa ajili ya kujenga nyumba ya kuishi...
3. Usichukue mkopo kwa ajili ya kununua gari ya kutembelea...
Hivi ni vitu unavyotakiwa kufanya kwa fedha ya faida, sio mkopo.
Chukua mkopo na fanya biashara, lipa mkopo na faida inayobaki ndiyo unaweza kutumia kwa hayo mambo matatu hapo juu.
Fanya kinyume na hapo na utauona uchungu wa mikopo.
Kila la kheri.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
 
Unapochukua mkopo, unatakiwa kulipa riba, yaani kama umekopa milioni kumi, utalipa zaidi ya milioni kumi.
Sasa kitu pekee kitakachokuwezesha uwe na fedha ya ziada ya kulipa ni biashara.
Hivyo vingine havizalishi, na hivyo utaumia kwa kulipa hela nyingi kuliko uliuokopa.
Ndiyo maana nashauri ni vyema kama unakopa basi iwe kwa kufanyia biashara.
Ila hizo nilizotaja hapo juu, fanya kwa faida ya biashara au kwa akiba zako binsfsi.
Mkopo kwa matumizi hayo utakuumiza, ni sawa na kuwafanyia kazi wengine.
 
Asante kwa ushauri mkuu lakini ningependa unitoe tongotongo hapa, mfano gharama ya pango ni Tzs milioni saba kwa mwaka na gharama(Riba) ya mkopo ni milioni tatu kwa mwaka, huoni hapo unafuu unakuja kukopa kwa ajili ya ujenzi hasa ukizingatia ukimaliza kulipa mkopo hutalipia pango tena!
 
Kwel kabisa mkuu uko sahihi sana.
 
Asante kwa ushauri mkuu lakini ningependa unitoe tongotongo hapa, mfano gharama ya pango ni Tzs milioni saba kwa mwaka na gharama(Riba) ya mkopo ni milioni tatu kwa mwaka, huoni hapo unafuu unakuja kukopa kwa ajili ya ujenzi hasa ukizingatia ukimaliza kulipa mkopo hutalipia pango tena!
Kwa hesabu kama hizi ni rahisi,
Lakini kumbuka yafuatayo,
1. Hata utakapochukua mkopo na kujenga, bado mwaka mzima utakuwa umepanga.
2. Ukipiga mahesabu yote mpaka uje kumaliza kulioa mkopo huo, utakuwa umelipa kiasi kikubwa sana.
Sasa kwa nini usichukue mkopo huo na kujikita nao kwenye biashara, ndani wa mwaka mmoja ukiwa active na kujitoa kweli biashara inasimama, hiyo miaka inayofuata tayari unakuwa unatengeneza faida, na unajenga bila stress.
 
Kitu kingine muhimu kuwa nacho makini kwenye mikopo ni kujua kwamba taasisi za fedha zinazotoa mikopo nao pia wanafanyabiashara.
Hivyo wakishajua una njia ya kuwalipa, watakushawishi uchukue mkopo hata kama hautakuwa na manufaa zaidi kwako.
Fikiri vyema kabla ya kuingia kwenye mkopo.
 
Kwa hesabu kama hizi ni rahisi,
Lakini kumbuka yafuatayo,
1. Hata utakapochukua mkopo na kujenga, bado mwaka mzima utakuwa umepanga.
2. Ukipiga mahesabu yote mpaka uje kumaliza kulioa mkopo huo, utakuwa umelipa kiasi kikubwa sana.
Sasa kwa nini usichukue mkopo huo na kujikita nao kwenye biashara, ndani wa mwaka mmoja ukiwa active na kujitoa kweli biashara inasimama, hiyo miaka inayofuata tayari unakuwa unatengeneza faida, na unajenga bila stress.

Ushauri wako siyo sasa kabisa hasa baada ya kuwaasa watu waachane na mikopo kwa ajili ya ujenzi napata wasiwasi na weledi wako katika masuala ya biashara na uchumi. Mfano mtu ni kijana ana umri wa miaka 25 na amepanga nyumba analipa TZS 300,000 kwa mwezi anaamua kuchukua mkopo wa miaka 5 ili ajenge nyumba na kweli anajinyima anaweza kujenga nyumba na kuhamia baada ya miaka 5 ijayo. Pamoja na interest na Principal kulipwa which is obvious kwa wote biashara na yeyote anaetaka kitu asichonacho kwa wakati huo.

Baada ya muda huo kuisha faida itakuwa double, umemaliza mkopo na umehamia kwako kama mtaalamu wa biashara na mchumi compute saving ya mkopaji huyo baada ya kukamilisha mkopo wake.
 
Kwa hesabu kama hizi ni rahisi,
Lakini kumbuka yafuatayo,
1. Hata utakapochukua mkopo na kujenga, bado mwaka mzima utakuwa umepanga.
2. Ukipiga mahesabu yote mpaka uje kumaliza kulioa mkopo huo, utakuwa umelipa kiasi kikubwa sana.
Sasa kwa nini usichukue mkopo huo na kujikita nao kwenye biashara, ndani wa mwaka mmoja ukiwa active na kujitoa kweli biashara inasimama, hiyo miaka inayofuata tayari unakuwa unatengeneza faida, na unajenga bila stress.

Asante mkuu,
Lakini kuna uwezekano wa kununua nyumba iliyokamilika kama tatizo litakuwa muda wa kungoja ujenzi. Kuhusu kwa nini usichukue mkopo na kuzungushia kwenye biashara ili ujenge, kwanza kuna watu wanachukua mkopo ilhali dhamana yake ya kulipia mkopo ni ajira yake hivyo hawezi kuacha ajira kwa ajili ya biashara hivyo anakaribisha asilimia kubwa ya kufeli kwani hataweza kujitoa 100%.

Pili kuna watu biashara hawazimudu vyema hivyo kujaribu kwa pesa za mkopo inaweza kuwa hatari zaidi, kulipia mkopo wa biashara iliyofeli kwa kipato cha kawaida na ugharamie majukumu mengine ni tatizo kubwa hivyo kupendekeza kuchukua mkopo kwa ajili ya biashara pekee inaweza kuwagharimu.
 
Mawazo yaliyopitwa na wakati haya! Bila mkopo wengi hasa watumishi wa serikali nyumba na magari wangebakia kuvisikia kwa wengine . Saving hadi uweze kununua gari au kujenga inaweza kukuchukua robo tatu ya umri wako kuifikia, hii ni % kubwa ya watanzania
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Hapo umechemka co wte wanaochukua mikopo ni wasio nazo wengne n watumish so n halali ajenge/anunue gari na marejesho anacover vzr tu,labda ungetofautisha man
 
Acheni woga wa maisha mkopo ni pesa kama pesa nyingine mkumbuke life is how u make it
Wapo waliochukua mkopo wakajengea wanafurahia maisha
Wapo waliochukua mkopo wakaenda lipa mahali wanafurahia maisha
Wapo waliochukua mkopo wakafanye biashara leo wanalia kilio

Nachotaka sema
Usiongelee yepi ni matumizi sahihi ya pesa wakati ujawahi chukua mkopo au huna vigezo vya kukopesheka

Namkumbuke hakuna hesabu sahihi yakufuata ili utoboe kimaisha ikiwa umefanikiwa kimaisha sema asante mungu usilete ujuaji Kuna watu wamekaza nakufuata principles zote za matumizi ya pesa ila mpaka leo wapo choka mbaya
 
Wakuu mimi huwa nafikiria sana hiki kitu mimi ni mtumishi lakini inaniuma sana kuchukua mkopo wa million 12 alafu nijengee nyumba na makato ya huo mkopo ni miaka sita, japo sijajenga lakini huwa natamani sana huo mkopo niongezee pesa ni nunue gari kama mitsubish canter nipige kazi ndani ya mwaka niweze kujenga kwa faida ya gari sijui kama watalaam mnaweza kunisaidia zaidi napenda sana magari hasa ya biashara
 
Ndiyo maana mimi kuna siku nilishauri kuondoa neno "kocha wako" kwenye utambulisho wa mleta mada. Lakini bahati mbaya hakunielewa. Point yangu ilikuwa kwamba ukijiita (au kuitwa) kocha maana yake ni kwamba wewe unajua kila kitu na wengine wanabaki kuwa "coached". Lakini hapa tuna share mawazo kutoka kwa kila mmoja na hivyo hakuna "kocha" na wengine kuwa "wachezaji wa kawaida".
 
Back
Top Bottom