Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,403
- 23,579
Ninayo sababu ya kuanzisha uzi huu. Kuna mambo matano nitayaongelea katika kukumbushana tu na leo naanza na namba moja nayo ni kivuko, MV Dar es Salaam...naomba uvumilivu wenu.
Flashback...January, 2012
Sakata la nauli za vivuko: Magufuli achafua hali ya hewa Dar, awaambia wakazi wa Kigamboni,"asiye na nauli ya Sh. 200 apige mbizi".
Fastforward to September, 2014...
1. MV DAR ES SALAAM
Jumatatu, tarehe 6/9/2014 - Breaking Nyuzz...!!!
KIVUKO KIPYA (MV DAR ES SALAAM) CHAWASILI.
Ile ahadi ya Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli ya kununua kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao wa Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo imetimia.
Taarifa za uhakikia tulizozipata hivi punde ni kuwa kivuko hicho (Mv Dar es Salaam) kilichokuwa kinajengwa huko Denmark leo kimeshuka majini na tayari kuanza safari ya kuja Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa kufika/kutua Dar es Salaam kati ya wiki tatu mpaka nne zijazo.
Kivuko cha MV Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko kivuko chochote Afrika ya Mashariki na hasa mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika ya Kusini.
Kivuko hiki ni muendelezo wa juhudi za Wizara ya Ujenzi za kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam...
Kivuko cha MV Dar es Salaam kama kilivyoonekana juu ya Meli kabla ya kushushwa majini katika bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki Meli kubwa ya mizigo iliyobeba Kivuko kipya cha MV Dar es Salaam ilipokuwa inakaribia kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionesha furaha yake ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.
Mpaka hapo maswali yenye utata kuhusu hiki kivuko ni haya;
KIVUKO KIPYA (MV DAR ES SALAAM) CHAFANYIWA UKAGUZI.
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli amekagua safari ya kivuko cha Mv Dar es Salaam kwa mara ya kwanza hadi Bagomoyo, huku kukiwa na changamoto kadhaa miezi michache kabla ya uzinduzi rasmi wa huduma hiyo.
"Mbali na kuongeza pato la taifa, pia kivuko hiki kitapunguza kwa namna moja ama nyingine foleni za jiji la Dar es Salaam na kukuza utalii," alisema Magufuli
“Kulikuwa na maneno mengi kuwa kivuko hakipo… na wale waliokuwa hawaamini kimekuja, wakitaka wakiguse,” alisema Dk Magufuli na kushangiliwa na umati uliokuwa feri kabla ya kuanza ukaguzi.
“Hiki kivuko ni cha aina yake hata maegesho yake ni tofauti. Niwapongeze wenzetu wa jeshi na nina uhakika wataifanya kazi ya kujenga kwa haraka,” alisema Dk Magufuli.
Kivuko cha Mv Dar es Salaam kimejengwa kwa ustadi wa hali ya juu na huduma nzuri za kukaa kama meli ya kitalii.
Kivuko cha MV Dar es Salaam kikiwa njiani kuwasili eneo la Magogoni kwa ajili ya kuanza safari ya kwanza ya majaribio ya kwenda Bagamoyo mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli akiongoza wakaazi wa jiji kwenye majaribio ya uzinduzi wa kivuko cka MV Dar es Salaam kitakachofanya kazi kati ya DSM na Bagamoyo.
Waziri wa Ujenzi John Magufuli akifanya ukaguzi wa MV Dar es Salaam alitoa ahadi kuwa atahakikisha nauli itakuwa nafuu kwa wananchi wote.
Mpaka hapo kuna maswali kadhaa yanayozua utata;

- Kilikuwa kipya?
- Kilijengwa Denmark?
- Kiligharimu kiasi gani?

- Ufanisi na uimara wake
- Gharama za uendeshaji
- Lengo kufikiwa.