Habari wana jf.? Leo ningependa tujikumbushe kazi au biashara zilizo kushinda na zina maslahi mazuri.
Yawezekana ilikushinda kwasababu haukufanya utafiti juu ya hiyo biashara au uvivu ulichangia. Naimani katika harakati za maisha mtu anapitia kazi na biashara tofauti ila mwisho wa siku anasimama sehem moja.
Binafsi::
1# Nilikutanaga na tangazo la kazi kwenye gazeti ila nilijiuliza hii ni kazi gani ambayo inahitaji hadi std 7 ila nikasema poa nikawapigia simu hatima wakaniambia niende bhana ile kazi ni zile za kusambaza vitu kama dawa, sabuni na vyombo aaah asikwambie mtu ile kazi ni ngumu mno mwisho nikapiga chini.
Nikaingia gereji tatizo likaja kawaida ya gereji hadi uje uthaminiwe inatakiwa uwe na ukaribu na fundi mkuu laa sivyo utaendelea kuwa mfanyakazi hapo kwa siku nikuwa nalipwa 2000 napo nikapiga chini.
2# Nikaingia kwenye masai sandals hapa ingawa palikuwa pagumu ila kidogo niliona afadhali hata hela yake ilikuwa inategemea na ufanyaji wako pia hata nilikuwa nikipiga picha ya mbele naona ni kitu ambacho naweza kukimudu kwani haikuhitaji mtaji mkubwa.
3# Hii biashara sikuamini kilicho niitokea ila ilikuwa biashara nzuri sana kwani kama hesabu ya faida unaijua mapema sana. Hii ni biashara ya kusafirisha mazao kutoka shamba kuja sokoni mimi nilikuwa nachukua machungwa kutokea Tanga na kuleta dar hii biashara iko vizuri ila ni hatari vibaya sana hasara yake huwa inakuwa ni kubwa sana.
Ilikuwa hivi wakati nipo tanga dalali akanipigia simu na kuniambia leo siku ya pili sokoni hakuna machungwa ni fanye juu chini kesho nipeleke mzigo kweli tukaingia shamba tukachuma machungwa ya kutosha usiku safari ikaanza kweli asubuhi mida ya saa 11 nikawa nimefika sokoni buguruni nilicho kiona hapana sikuamini kulikuwa na gari nyingi sana zimeleta machungwa mwisho tukauza machungwa kwa Tsh 35 na shamba nilinunua kwa Tsh 40 ambapo nilitakiwa kuuza kwa Tsh 80 hadi 70.
Hii biashara kama unajijua umekopa hela usije ukajaribu ni hatari.